Translate

Jumatano, 12 Juni 2019

Haki za Mume kutoka kwa Mke

Haki za Mume kutoka kwa Mke


1-Mke amtii mumewe na atambue kwamba ni amri ilotiliwa nguvu na Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) kwa kuwa amesema:
((لَوْ كُنْتُ آمِراً أَحَداً أَنْ يَسْجُدَ لأِحَدٍ لأَمَرْتُ الْمَرْأَةَ أَنْ تَسْجُدَ لِزَوْجِهَا مِنْ عِظَمِ حَقَّهِ عَلَيْهاَ))
((Ningeliweza kumuamrisha mtu  amsujudie binaadamu mwenzake, ningeliamrisha mwanamke amsujudie mume wake kwa jinsi haki ya mume ilivyo tukufu kwa mke wake))Tuhfat Al-Ahwadhi 4.323  kutoka Tafsiyr ya Ibn Kathiyr

2-Mke inampasa kumuitikia mumewe anapomhitaji kujimai naye. Kutomtimizia haja yake bila ya sababu inayokubalika katika Shariy’ah ya Dini ni kulaaniwa na Malaika kwa dalili:
((إذا دَعَا الرَّجُلُ امْرَأتَهُ إِلىَ فِرَاشِهِ فَأَبَتْ عَلَيْه لَعَنَتْهَا الْمَلائِكَةُ حَتَّى تُصْبِحَ))
((Mume atakapomwita mkewe kitandani na mke akikataa, basi Malaika watakuwa wanamlaani huyo mke mpaka asubuhi))Imepokelewa na Imaam Al-Bukhaariy

3-Haimpasi mke kutoa swadaqah yoyote bila ya idhini ya mumewe; amekataza Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam):
((لاَ تُنْفِقُ الْمَرْأَةُ شَيْئًا مِنْ بَيْتِهَا إِلا بِإِذْنِ زَوْجِهَا)) قالوا: "يا رسول الله! وَلا الطَّعَامَ؟ قال: ((ذَاكَ أَفْضَلُ أَمْوَالِنَا)) صحيح ابن ماجه - حديث حسن الألباني
((Mwanamke asitoe kitu chochote kutoka nyumbani kwake ila kwa idhini ya mumewe)). Wakasema: “Hata chakula ee Mtume wa Allaah”? Akasema: ((Hicho ni mali bora yetu)).   Hadiyth imepokelewa na Ibn Maajah na Shaykh Al-Albaaniy kasema ni ‘Hasan’.
Lakini mke anayo haki kutoa swadaqah katika kipato chake mwenyewe.   
Pia mke anaweza kutoa swadaqah ikiwa anatambua kuwa hatoghadhibikiwa na mumewe:
عن همام (رضي الله عنه)  قال: سمعت أبا هريرة (رضي الله عنه) عن النبي صلى الله عليه وسلم قال: ((إِذَا أَنْفَقَتِ الْمَرْأَةُ مِنْ كَسْبِ زَوْجِهَا عَنْ غَيْرِ أَمْرِهِ فَلَهُ نِصْفُ أَجْرِهِ))  - البخاري
Kutoka kwa Hamaam (Radhiyya Allaahu ‘anhu) amesema: “Nimemsikia Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ‘anhu) kwamba Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) amesema: ((Mwanamke akitoa swadaqah kutoka katika kipato cha mumewe bila ya amri yake basi na yeye atapata thawabu nusu yake)) Al-Bukhaariy

4-Haimpasi mke kutoka nyumbani kwake bila ya idhini ya mumewe (hata kwenda kwa wazazi wake ila kwa makubaliaono).

5-Haimpasi mwanamke kumfanyia ujeuri, ufedhuli au usafihi mumewe. Atakapokuwa ni kinyume cha hivyo akamtii mumewe basi amepewa fadhila kubwa ya kuingia Peponi:
عن عبد الرحمن ابن عوف (رضي الله عنه) قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: ((إِذَا صَلَّتْ الْمَرْأَةُ خَمْسَهَا، وَصَامَتْ شَهْرَهَا، وَحَفِظَتْ فَرْجَهَا، وَأَطَاعَتْ زَوْجَهَا, قِيلَ لَهَا: ادْخُلِي مِنْ أَيِّ أَبْوَابِ الْجَنَّةِ شِئْتِ)) صحيح الترغيب
Kutoka kwa Abdur-Rahmaan bin 'Awf (Radhiya Allaahu ‘anhu) kwamba Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) amesema: ((Mwanamke atakaposwali Swalaah zake tano, akafunga Swawm mwezi wake (wa Ramadhaan), akahifadhi sehemu zake za siri (asifanye uzinifu), akamtii mume wake, ataambiwa ingia peponi kupitia mlango wowote autakao))  Swahiyh at-Targhiyb

Hizo ni baadhi ya haki tulizojaaliwa kuzinukuu, tukitaraji kwamba pindi zikitimzwa, basi ndoa itaendelea kudumua katika usalama na amani.


NA  ALLAAH  ANAJUA  ZAIDI


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

20-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Isti’aadhah Kwa Asiyekuwa Allaah

  إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيم   Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!   20 - Isti’aadhah  (Kuomba Kinga) Kwa Asiyekuwa Allaah   ...