Swali
Ni ipi hukumu mfungaji kumeza mate?
Jibu
Hakuna neno kumeza mate. Sijui kama kuna tofauti yoyote juu ya hilo wanachuoni kutokana na ule uzito na ugumu wa kujiepusha na hilo.
Kuhusu makohozi ni lazima kwa mtu kuyatema pale yanapofika kinywani. Haijuzu kwa mfungaji kuyameza kwa sababu kuna uwezekano wa kuyaepuka tofauti na mate.
Rejea Majmuu´-ul-Fataawaa (15/313)
http://bit.ly/30hxs9H