Translate
Jumatatu, 13 Mei 2019
Nywele za bandia na baruka
1008- Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Mwanamke yeyote ambaye ataingiza kwenye nywele zake nywele zisizokuwa zake basi si vyengine isipokuwa ameingiza hali ya uongo.”
Ameipokea Ahmad kupitia kwa Mu´aawiyah kwa cheni ya wapokezi iliotangulia. Ina mapokezi mengi yenye kuitolea ushahidi pamoja vilevile na kwa al-Bukhaariy na Muslim.
Ikiwa hii ndio hukumu kwa mwanamke ambaye ameingiza ndani ya nywele zake nywele zisizokuwa zake, ni ipi hukumu kwa mwanamke kuvaa baruka? Ni ipi hukumu kwa yule mtu mwenye kujuzisha kuivaa ima kwa njia isiyofungamana au kwa njia iliofungamana kwa ajili ya kufuata kichwa mchunga baadhi ya madhehebu na pasi na kujali kuwa anapingana na Hadiyth ambazo ni Swahiyh? Kwani Allaah amemwongoza kuona kuwa ni lazima kuzifuata Hadiyth japokuwa zitakuwa zinaenda kinyume na madhehebu yake, sembuse madhehebu ya wengiene. Tunamuomba Allaah atuzidishie uongofu juu ya uongofu na atutunuku elimu na uchaji.
from Firqatu Nnajia http://bit.ly/2YnPHbF
via IFTTT
Je, kutokwa na damu puani kunafunguza?
Swali 428: Je, kutokwa na damu puani kunafunguza?
Jibu: Kutokwa na damu puani hakufunguzi hata kama zitakuwa nyingi. Kwa sababu hakutokwa na damu kwa kutaka kwake mwenyewe.
from Firqatu Nnajia http://bit.ly/2W13pDM
via IFTTT
Makundi sabini na mbili yatadumishwa Motoni milele?
Swali: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Ummah wangu utafarikiana mapote sabini na tatu. Yote yataingia Motoni isipokuwa moja tu.”
Je, mapote yote haya yatadumishwa Motoni milele?
Jibu: Kinachotambulika kwa wanachuoni ni kwamba watu hawa ni miongoni mwa waliopewa matishio na kwamba ni katika wazushi. Kwa ajili hii wamesema kwamba Jahmiyyah ni wenye kutoka nje ya makundi haya sabini na mbili kwa sababu ni makafiri.
from Firqatu Nnajia http://bit.ly/2E5DP6x
via IFTTT
“Nyoa ndevu ili baadaye ziwe nyingi”
Swali: Mama yangu ananiamrisha kuzinyoa ndevu zangu ili baadaye zimee kwa wingi. Je, inafaa kumtii katika hilo?
Jibu: Hapana, asimtii katika hilo. Hii ni dhambi na mama yake ni mjinga. Asimtii katika hili. Aziache ndevu kama alivyoziumba Allaah na wala asiziguse eti ili ziwe nyingi. Aridhie yale aliyomwandikia Allaah.
from Firqatu Nnajia http://bit.ly/2WKwsc4
via IFTTT
Mwanakamati wa kitengo cha Da´wah ambaye hakusoma
Swali: Inafaa kwa mzungu ambaye hakusoma chini ya wanachuoni na wala hatambuliki kuwa na elimu awe mmoja wa wanakamati wa Da´wah ya Kiislamu?
Jibu: Kamati jambo lake ni jepesi. Hata hivyo asifundishe na wala asitoe fatwa midhali hakusoma chini ya wanachuoni.
from Firqatu Nnajia http://bit.ly/2E6qgnr
via IFTTT
Jumapili, 12 Mei 2019
Kama kweli wewe ni mja wa Allaah
1568- Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Kama wewe kweli ni mja wa Allaah, basi kipandishe kikoi chako.”
Ameipokea Ahmad (2/141): Muhammad bin ´Abdir-Rahmaan at-Twafaawiy ametuhadithia: Ayyuub ametuhadithia, kutoka kwa Zayd bin Aslam, kutoka kwa Ibn ´Umar ambaye amesema:
“Niliingia kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) nikiwa nimevaa kikoi chenye kuburutaburuta. Akasema: “Ni nani huyo?” Nikasema: “Ni ´Abdullaah bin ´Umar.” Akasema: “Kama wewe kweli ni mja wa Allaah, basi kipandishe kikoi chako.” Nikakipandisha kikoi changu mpaka nusu ya muundi. Hakuacha kuendelea kukaa kikoi chake hivo mpaka alipofariki.”
Mlolongo wa wapokezi ni Swahiyh na ni kwa masharti ya al-Bukhaariy na Muslim.
Katika Hadiyth kuna dalili ya wazi kabisa yenye kuonyesha kuwa haijuzu kwa muislamu kurefusha kikoi chake kikaenda chini ya kongo mbili za miguu. Bali ni lazima kwake kukipandisha juu ya kongo mbili za miguu. Haijalishi kitu hata kama lengo lake yeye sio kiburi. Hapa kuna Radd ya wazi kwa baadhi ya wanachuoni ambao wanayarefusha majuba yao mpaka yanakaribia kugusa chini. Wanadai kwamba hawafanyi hivo kwa kiburi. Ni kwa nini basi wameiacha amri ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa Ibn ´Umar? Je, wao mioyo yao ni misafi zaidi kushinda wa Ibn ´Umar?
from Firqatu Nnajia http://bit.ly/2vVrSvv
via IFTTT
20-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Isti’aadhah Kwa Asiyekuwa Allaah
إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيم Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! 20 - Isti’aadhah (Kuomba Kinga) Kwa Asiyekuwa Allaah ...
-
إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيم Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! 20 - Isti’aadhah (Kuomba Kinga) Kwa Asiyekuwa Allaah ...
-
Dalili 18 zinazoashiria una ujauzito wa mtoto wa kiume Awali ya yote nitoe pongezi kwa mama K na Baba K wote popote walipo kwa kazi nzuri ...