Dalili 18 zinazoashiria una ujauzito wa mtoto wa kiume
Awali ya yote nitoe pongezi kwa mama K na Baba K wote popote walipo kwa kazi nzuri na baraka ambayo wanaisubiri kutoka kwa Mungu (mtoto).
Mojawapo ya mambo ambayo yanatia furaha katika maisha ya ndoa ni pale wanandoa wanapokuwa wapo kwenye kipindi cha kutegemea mtoto.
Mambo mengi huwa yanaleta hamasa na ushawishi kuhusiana na huyo mtoto. Mambo kama jinsia yake kama ni wa kiume au wa kike nk.
Maandalizi kadhaa huanza kufanywa kabla hata ya mtoto kuzaliwa, hii ikijumuisha manunuzi ya vitu kwa ajili ya mtoto na majina wakati atakapo zaliwa.
Madaktari wana uwezo wa kujua jinsia ya mtoto ambaye hajazaliwa kwa kutumia kipimo cha ULTRASOUND.
Watu wengi hawajuwi kuwa wanaweza kufahamu jinsia ya mtoto kutokana na dalili ambazo mama mjamzito anazionyesha, kuanzia mabadiliko ya kimwili, kulala na mpaka upendo wa vyakula fulani.
Soma hii pia > Dawa ya asili ya kupata mimba haraka
Utastaajabu kujua kuna uwezekano wa viashiria kuhusiana na jinsia ya mtoto anaetegemewa, bila kwenda hospitali na kutumia ULTRASOUND.
Kuna ishara kadhaa ambazo zinaweza kukujulisha kuhusiana na jinsia ya mtoto hata kabla hajazaliwa.
Kwa mjibu wa tafiti mbalimbali, yafutayo yanaweza kutumika kama viashiria vya kujua kama mama K ana mtoto wa kiume.
Dalili za mimba ya mtoto wa kiume
1) Umachachari wa mjamzito
Kwa kila jinsi mwili/tumbo la mjamzito linavyokua, umachachari hua haukosekani, ila unapopitiliza mipaka kuliko kawaida, basi kuna uwezekano mkubwa wa kujifungua mtoto mwenye jinsia ya KIUME.
2) Kukua kwa Maziwa
Katika kila hatua ya mimba, mwanamke hua anagundua ni jinsi gani maziwa/matiti yake hubadilika kwa kukua. Kama ziwa/titi lake la kulia likitokea kuwa kubwa kuliko la kushoto, basi kuna uwezekano mkubwa wa kujifungua mtoto wa KIUME. Na kama titi/ziwa la kulia likiwa kubwa kuliko la kushoto, basi kuna uwezekano mkubwa wa kujifungua mtoto wa KIKE.
3) Rangi ya Chuchu
Rangi ya chuchu kipindi cha ujauzito zinaweza kuashiri jinsia ya mtoto, rangi inapokua ya kiza (darker) kuliko kawaida ni dalili ya kujifungua mtoto wa KIUME, na kama rangi haijabadilika katika hatua za mimba ni dalili ya mtoto wa KIKE.
4) Aina ya Ulalaji
Kupendelea kulalia ubavu wa kulia ni dalili za kujifungua mtoto wa KIUME, na kupendelea kulalia ubavu wa kushoto ni dalili ya kujifungua mtoto wa KIKE.
5) Kuumwa Kichwa
Kama mjamzito atakua na matatizo ya kuumwa kichwa mara kwa mara, mtoto wa KIUME yupo njiani kuja. Na kama hatokua na matatizo ya kichwa, basi uwezekano wa mtoto wa KIKE kuzaliwa.
6) Uzito wa Baba
Kama mzazi wa kiume akiongezeka kilo, ni dalili za mama mjamzito kujifungua mtoto wa KIKE, na kama mzazi wa kiume asipo ongezeka kilo/au kupungua kilo ni dalili za mtoto wa KIUME.
7) Tumbo la Uzazi Kua Juu au Chini
Kama tumbo la mjamzito litakua juu, ni dalili za kuzaliwa mtoto wa KIKE, na kama tumbo la uzazi litakua chini basi inaashiria mtoto wa KIUME.
8) Tamaa ya Chakula
Tamaa ya kupendelea vyakula vya chumvi/ukali basi ni dalili ya kupata mtoto wa KIUME, na kupendelea kula vyakula vya sukari ni dalili ya mtoto wa KIKE.
Soma hii pia > Jinsi ya kupata mtoto wa jinsia ya kiume
9) Miguu Kuvimba
Kama miguu ya mjamzito haivimbi, basi inaashiria mtoto wa KIKE, kwani mtoto wa KIUME ana uwezo wa kumwongezea mjamzito uvimbaji wa miguu, mara mbili ya size ya huyo mjamzito miguu yake.
10) Joto la Nyayo za Miguu
Kama nyayo za miguu zitakua za baridi, kuna dalili ya kujifungua mtoto wa KIUME, na kama nyayo hazijabadilika joto lake halisia ni dalili za mtoto wa KIKE.
11) Kugawanyika Kwa Uzito Mwilini
Kama mjamzito ataongezeka kilo/uzito mwili mzima, ni dalili za kujifungua mtoto wa KIKE. Na kama ataongezeka uzito kwenye tumbo tu ni dalili za mtoto wa KIUME kuwa njiani.
12) Nywele za Mwilini
Nywele za mwilini kukua kwa haraka na kua imara, ni dalili za mtoto wa KIUME kuzaliwa, wakati dalili za mtoto wa KIKE hua nywele hazioti mwilini.
13) Unawiri wa Nywele Kichwani
Nywele nzito na zenye mafuta/kunawiri ni kiashiro cha kujifungua mtoto wa KIUME, na nywele kavu/kukatika/kukosa mvuto/rough ni dalili ya kujifugua mtoto wa KIKE.
14) Kipimo Cha BAKING-SODA
Chukua vijiko viwili vya baking soda na kisha changanya na mkojo wa mjamzito, kama baking soda itatoa mapovu ya gas na mliokama wa kuchemka (fizzes), ni mtoto wa KIUME anakuja. Kinyume na hapo basi atakua wa KIKE.
15) Mstari Tumboni
Huu ni msitari ambao hutokea katika tumbo la mjamzito, mstari huu ukitokea na kuishia chini ya kitovu, basi inaashiria ujio wa mtoto wa KIKE, na kama ukipitiliza mpaka juu ya kitovu, ni kiashirio cha kuja kwa mtoto wa KIUME.
16) Furaha
Ni mtoto wa KIUME pekee ndio ambae humpa muwako/sura ya furaha/kunawiri kwa uso wa mama mjamzito. Mtoto wa kike humchosha sura mama yake muda wote.
17) Chunusi
Kubemba mimba ya mtoto wa KIKE huwaletea wajawazito chunusi usoni, ni dalili moja wapo. Vinginevyo, atakua mtoto wa KIUME.
18) Mabadiliko Ya Ngozi
Kama ngozi ya mjamzito ikibadilika na kua yenye mafuta (oily skin) ni dalili za kuashiria mtoto ajae ni wa KIKE, na kama ngozi ikibakia kua kavu (dry skin) ni dalili za ujio wa mtoto wa KIUME.
Kama unatafuta dawa ya asili kwa ajili ya kupata ujauzito, niachie tu ujumbe WhatsApp +255714800175
Pokea dondoo nyingine za afya kama hii kupitia facebook BURE. Jiunge na mimi na watu wengine zaidi ya 94000 kwenye ukurasa wangu wa facebook kwa kubonyeza hapa .
Tafadhali SHARE post hii kwa ajili ya wengine.
Soma hii pia > Mimba huanza kuonekana baada ya siku ngapi
Imehaririwa
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni