Translate
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Muislamu Blog. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Muislamu Blog. Onyesha machapisho yote
Jumamosi, 11 Mei 2019
Jumatano, 8 Mei 2019
Makosa Yafanywayo Na Wenye Kufunga Katika Mwezi Wa Ramadhwaan
Yafuatayo ni makosa ambayo yameonekana yakitendeka katika mwezi wa Ramadhwaan ima wanapokuwa Waislamu katika Swawm au baada ya kufuturu na katika Swalah za Qiyaamul-Layl. Hivyo inapasa tuyazingatie na kujiepusha nayo ili tubakie katika usalama wa Swawm zetu, Swalah zetu na mengine yote yanayohusu mwezi huu mtukufu:
1. Kutia niyyah kwa kutamka:
Baadhi wanaamini kuwa niyyah usipoitamka basi haijawa niyyah. Na pia huwafunza watoto kutamka maneno ya kutia niyyah, au kuwaamrisha wasikose kwenda kunuizwa Msikitini na mashekhe. Itambulike kuwa niyyah mahali pake ni moyoni na kutamka ni uzushi.
2. Kufunga bila kuswali:
Baadhi ya watu wanafunga bila ya kuswali au kutimiza Swalah ipasavyo. Watu kama hawa Swawm zao hazifai kwani Swalah ni nguzo ya Dini ya Kiislamu.
3. Kudhani kwamba Swalah ya Taraawiyh inaanzwa siku ya kwanza ya Ramadhwaan:
Hali inaanza usiku ule unaoandama mwezi. Sunnah ni Waislamu waanze kuswali usiku huo na si baada ya kufunga siku ya kwanza.
4. Kuchelewa kufuturu/kufutari:
Baadhi ya watu husubiri hadi adhana imalizike na wengine husubiri hadi kiza kiingie na hali tumehimizwa tukimbilie kufuturu. Matokeo yake ni kukiuka Sunnah ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na pia huenda kufanya hivyo wakachelewa Swalah ya Magharibi. Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) anasema:
لا تزال أمتي بخير ما عجَّلوا الإفطار - رواه الإمام أحمد
((Ummah wangu utabakia katika khayr watakapokimbilia kufuturu)) [Imaam Ahmad]
5. Kuomba du'aa zisizo sahihi wakati wa kufuturu:
Wengi wameizoea du’aa hii na kuisoma wakati wa kuanza kufuturu, ingawa ni du’aa yenye mapokezi dhaifu yasiyo sahihi:
اللَّهمَّ! لك صُمتُ، وعلى رِزقك أفطرتُ
Allaahumma Laka Swumtu wa 'alaa Rizqika aftwartu.
Wanachuoni wa Hadiyth wanaeleza kuwa hakuna du’aa yoyote iliyothibiti wakati wa kufuturu.
7. Kufuturu kwa vitu vya haraam kama kuvuta sigara n.k.
Wanakosa kutambua kwamba hii fursa kubwa kwa waliozoea kuvuta sigara kuacha moja kwa moja kuanzia mwezi wa Ramadhwaan, kwani ikiwa wameweza kufunga siku nzima na kujizuia kuvuta, vipi washindwe kujizuia na usiku?
8. Kula Futari kupita kiasi:
Utakuta mtu akifuturu huwa anafanya kisasi, anataka ale kulipiza ile njaa ya siku nzima, matokeo yake anashiba kiasi kushindwa hata kwenda kuswali Taraawiyh.
9. Kukithirisha Michezo na Upuuzi:
Utakuta watu wakati uingiapo mwezi wa Ramadhwaan, ndio wanaanza kutoa ile michezo waliyoiweka pembeni mwaka mzima, au kwenda kununua michezo mipya kama karata, carrum (keram), drafti, domino (dhumna) n.k. wakicheza mchana kutwa ili kupitisha muda uende haraka. Na kisha ifikapo usiku badala ya kwenda kuswali Taraawiyh.
Wanakesha kwa kuangalia televisheni, filamu na mipira.
Na wengine wakiyaambatanisha hayo kwa kula mirungi na kuvuta sigara. Hayo ni mambo ya haramu na yenye kuwapotezea fadhila na ujira upatikanao katika Ramadhwaan, wakati ambapo wangeutumia mchana wao kuchuma kwa kusoma Qur-aan sana na kuhudhuria darsa za Dini au kusoma vitabu vya Dini, kusikiliza mawaidha, Qur-aan n.k. Na ifikapo jioni wangeutumia muda wao kusimamisha Swalah za usiku (Taraawiyh), na pia kupumzika ili waweze kuwahi Swalah ya Alfajiri. Gumzo lisilokuwa katika mas-ala ya Dini jambo lililochukizwa na Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kama usimulizi ulivyopokelewa kutoka kwa ‘Abdullaah bin Mas-uwd (Radhiya Allaahu 'anhu):
عن عبد الله بن مسعود: ((لا سمر إلا لمصل أو مسافر))
السلسلة الصحيحة - المحدث: الألباني
((Hakuna kupiga gumzo la usiku isipokuwa kwa mwenye kuswali au msafiri)) [As-Silsilat Asw-Swahiyhah – Al-Muhaddith Al-Albaaniy]
وعن أبي برزة "أن رسول الله صلى الله عليه وسلم كان يكره النوم قبل
العشاء والحديث بعدها" رواه البخاري، ومسلم
Na kutoka kwa Abu Barzah kwamba Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akichukia kulala kabla ya 'Ishaa na gumzo baada yake) [Al-Bukhaariy na Muslim]
10. Kusengenya, kudanganya, kupiga porojo na kukaa mabarazani kupoteza wakati:
Wanajisahau wengi wetu kwa kupiga soga zisizo na maana na pia kusema wenzao, kutukana, kulaani na kuongea mambo ya uongo n.k. Pia wengi wetu wakifunga huwa na khasira sana. Huko kunapelekea mtu kupoteza ujira wa funga yake na pia hata kuibatilisha (kwa maoni ya Maulamaa wengine), Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) anasema: ((Ambaye hatoacha maneno ya uongo na matendo yake, basi ajue kwamba Allaah hana haja ya yeye kuacha chakula chake na kinywaji chake)) [ameisimulia Imaam al-Bukhaariy]
11. Kuwachukua watoto wadogo Misikitini ambao wanafanya fujo na kusababisha kushawishi Maimaam na Maamuumiyn (wanaoswali) washindwe kupata khushuu (unyenyekevu) katika Swalah.
Kuwazoesha watoto Msikiti ni jambo zuri kabisa, lakini panapoonekana kuna matatizo kama hayo, basi ni bora kuwaepusha ili wasiharibu Swalah za wengi.
12. Kutokukamalisha Swalah ya Taraawiyh na Imaam ili kupata fadhila za Qiyaamul-Layl kwani Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
((مَنْ قَامَ مَعَ الإِمَامِ حَتَّى يَنْصَرِفَ كَتَبَ اللَّهُ لَهُ قِيَامَ لَيْلَةٍ))
رواه الترمذي وصححه الألباني في صحيح الترمذي
((Atakayesimama (kuswali) na Imaam hadi amalize ataandikiwa (fadhila za) Qiyaamul-Layl)) [Imesimuliwa na at-Tirmidhiy na kaipa daraja ya Swahiyh al-Albaaniy katika Swahiyh at-Tirmidhiy]
13. Kushika Mus-haf na kumfuatiliza Imaam anaposwalisha:
Kufanya hivyo, kunamkosesha mtu kuipata Sunnah ya kufunga mikono yake na pia kupoteza fadhila za kuisikiliza Qur-aan kutoka kwa Imaam ambayo tumeamrishwa kuisikiliza inaposomwa, Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala):
((وَإِذَا قُرِىءَ الْقُرْآنُ فَاسْتَمِعُواْ لَهُ وَأَنصِتُواْ لَعَلَّكُمْ تُرْحَمُونَ))
((Na isomwapo Qur-aan isikilizeni na nyamazeni ili mpate kurehemewa)) [Al-A'raaf:2 04]
14. Kusoma tasbiyh fulani kila baada ya rakaa nne ya mapumziko:
Hakuna dalili ya kufanya hivyo. Lililothibiti ni kusoma tasbiyh mwisho kabisa unapomaliza Swalah ya Witr kwa kusema mara tatu:
سُبْحَانَ الْمَلِكِ الْقُدُّوسِ
Subhaanal-Malikul-Qudduus
(Kisha ya tatu utaivuta na kuisema kwa sauti ya juu)
15. Kuharakisha kula Daku:
Utakuta baadhi ya watu wanawahisha Daku na kuila saa sita za usiku au hata baada tu ya Taraawiyh, ima kwa kutaka walale moja kwa moja hadi Alfajiri au kwa sababu ya uvivu wa kuamka kwa ajili ya Daku. Kufanya hivyo ni makosa kwa sababu kunakwenda kinyume na mafunzo ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), na pia kunapelekea kuikosa ile baraka iliyojaaliwa kwenye Daku. Na Daku si lazima kula mlo mzito, japo tende au maji yatosha. Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) anasema:
((عجلوا الإفطار، وأخروا السحور)) صحيح الجامع - صححه الآلباني
((Harakisheni kufuturu na chelewesheni daku)) [Swahiyh al-Jaami' na kaipa daraja ya Swahiyh Shaykh Al-Albaaniy]
16. Kudhani mwisho wa kula daku ni dakika kumi kabla ya adhana ya Alfajiri:
Hivyo mtu akichelewa kula daku na ikawa karibu na dakika chache tu kabla ya Alfajiri hujinyima daku kwa khofu kuwa Swawm yake itabatilika. Wengine wameweka mipaka ya dakika kumi, hivyo si sawa. Mtu anaweza kula daku hadi karibu na Alfajiri hata kunapoadhiniwa. Na pindi Muadhini akiadhini ndipo unapoanza kufunga na Swawm yako inasihi. Na hata Muadhini akiadhini na kama una tonge au fundo la maji mdomoni usiliteme, kamilisha kulimeza kisha ndio uanze kufunga. Haya yamethibiti katika Sunnah kama inavyoonyesha Hadiyth ifuatayo:
Kutoka kwa Sufyaan bin ‘Uyaynah kutoka Az-Zuhriy, naye kutoka kwa Saalim naye kutoka kwa baba yake, kwamba Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) anasema: ((Hakika Bilaal anaadhini usiku (adhana ya mwanzo), basi kuleni na mnywe hadi aadhini Ibn Ummi Maktuwm)) [At-Tirmidhiy]
17. Kudhani kwamba mtu anapoamka na janaba huwa Swawm yake haifai:
Dhana hiyo si sahihi, bali sahihi ni kuwa mtu anaweza kujitwaharisha hata baada ya kuingia Alfajiri mradi tu aiwahi Swalah ya Alfajiri isije kumpita. Na Swawm yake ni sahihi.
18. Kufunga ukiwa safarini:
Walioko safarini kujikalifisha na kujitia katika mashaka ya kufunga na kuacha kuchukua rukhsa iliyotolewa kufuturu; si jambo jema kufanya hivyo kama ilivyo dalili ya Hadiyth:
عن جابر بن عبد الله أن رسول الله صلى الله عليه وسلم رأى رجلا يظلل عليه والزحام عليه فقال: ((لَيْسَ مِنَ الْبِرِّ الصِّيَامُ فِي السَّفرَ)) صحيح أبي داود
Kutoka kwa Jaabir bin 'Abdillaah ambaye amesema: "Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alimuona mtu akiwa amewekwa chini ya kivuli hali yake taabani baada ya kudhoofika kutokana na Swawm akamwambia: ((Sio katika wema (ucha Mungu) kufunga katika safari)) [Swahiyh Abiy Daawuud].
Lakini ikiwa hakutokuwa na taklifa wala mashaka, mtu anaruhusiwa kufunga.
19. Kutokujua Hukmu za Swawm:
Baadhi ya watu hawajui Hukmu sahihi za funga kisha huwa hawaulizi, ima kwa kuona hayaa au wakidhani wanajua. Ni vizuri mtu aulize lile asilo na hakika nalo kwa wale wenye elimu, ile asije akakosa fadhila na khayr hizi zipatikanazo kwa nadra mno. Na hali ya kutokujua Fiqh ya Swawm, kama kujua mambo yenye kufunguza na yale yasiyofunguza, kunaweza kumpelekea mtu kushinda na njaa bure huku Swawm yake ishabatilika, au kumfanya mtu afungue na hali Swawm yake bado ni sahihi. Mfano wa mambo yasiyobatilisha Swawm ni; kudungwa sindano, kung'oa jino, kujipulizia dawa ya pumu, wanawake kufanyiwa ukaguzi sehemu zao za siri na daktari (gynaecology checkup) - mtu ahakikishe anampata daktari wa kike na akiwa Muislam ndio bora zaidi, na akikosa kabisa hapo ni dharura tena na halaumiwi - na hili si katika Ramadhwaan tu, bali ni wakati wowote mwanamke anapokwenda Hospitali awe anafanya jitihada na kuuliza apatiwe daktari wa kike.
20. Kumjua Allaah katika Ramadhwaan pekee:
Baadhi ya watu humkumbuka Allaah katika mwezi huu tu, utakuta wanafunga na kuswali katika Ramadhwaan kisha baada ya Ramadhwaan kila kitu kinasimama kana kwamba Allaah Hayupo tena! Ni vyema watu wajue kuwa Allaah ni wa miezi yote na si mwezi wa Ramadhwaan pekee.
21. Kutamani Ramadhwaan iishe:
Baadhi ya watu wanahesabu masiku na wakiwa wanaomba Ramadhwaan imalizike upesi ili warejee katika hali yao ya kawaida ambayo wanaiamini kuwa ina uhuru wa kufanya wanayoyataka. Lau angelijua mja fadhila na khayr zilizo katika mwezi huu, hakika angetamani usiishe.
Katika mwezi ambapo tendo dogo lakuingizia ujira zaidi ya maradufu.
Katika mwezi huu kuna usiku ambao ni bora kuliko miezi elfu.
Katika mwezi huu vishawishi na balaa za Shaytwaan vimewekwa mbali.
Katika mwezi huu Malaika wametapakaa kukusanya ‘amali zako za khayr hata za udogo wa sisimizi
Tunamuomba Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala Atuongezee elimu ya Dini Yake Tukufu ili tuzidi kutoka katika kiza na kuingia katika mwanga utuongoze katika Swiraatwul-Mustaqiym.
from Muislamu Blog http://bit.ly/302daAZ
via IFTTT
Jumamosi, 4 Mei 2019
Tafsiyr Ya Imaam As-Sa'dy: Kufaridhiswa Swawm
Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anasema:
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا كُتِبَ عَلَيْكُمُ الصِّيَامُ كَمَا كُتِبَ عَلَى الَّذِينَ مِن قَبْلِكُمْ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ ﴿١٨٣﴾
Enyi walioamini! Mmefaridhishwa Swiyaam kama ilivyofaridhishwa kwa walio kabla yenu mpate kuwa na taqwa. [Al-Baqarah: 183]
Allaah Anajulisha katika Aliyoyafadhilisha kwa waja Wake kwamba Amewajibisha Swawm kama Alivyowajibisha ummah zilizopita kwa sababu ni shariy’ah (hukmu) na amri zinazomnufaisha bin Aadam katika kila zama.
Nayo ni changamoto ya kumhuisha mtu nafsi yake kwani inapasa kushindana na wengine katika mambo ya khayr ili mkamilishe 'amali zenu na mkimbilie (kuchuma) sifa njema na hakika hayo si katika mambo mazito mliyohusishwa nayo.
Kisha Allaah Anataja hikma Yake kuhusu Shariy’ah ya Swawm, Anasema:
لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ
mpate kuwa na taqwa
kwamba Swawm ni sababu kuu ya taqwa (kumcha Allaah) kwa kuwa ni kutekeleza amri za Allaah na kujiepusha na yaliyokatazwa.
Kwa hiyo katika Swawm yanapatikana yafuatayo:
- Taqwa ya asw-swaaim (anayefunga swawm) huacha yote Aliyoyakataza Allaah; kula, kunywa, kujimai na kama hayo, na yote yanayoelemea nafsi yake kuyatamani; hapo basi hujikurubisha kwa Allaah kwayo akitaraji thawabu kwa kujiepusha nayo. Haya yote ni kutokana na taqwa.
- Na Swawm pia inamfunza mtu kumcha Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) basi hujiepusha na hawaa ya nafsi yake, kwa (kutegemea) Uwezo Wake (Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) kwa kuwa anatambua kwamba Allaah Anamuona (ayatendayo yote).
- Swawm pia inamzuia mtu na shaytwaan kwani hakika shaytwaan anatembea katika mishipa ya damu ya mwana Aadam. Kwa hiyo Swawm inamvunja nguvu shaytwaan (na uchochezi wake), hivyo madhambi hupunguka.
- Swawm pia aghalbu humfanya mtu azidishe utiifu na utiifu ni katika sifa za taqwa.
- Swawm pia inamfanya tajiri anaposhikwa na njaa inayombidi imshike (kwa kuwa ni fardhi kwake, huwafikiria na) huwahurumia masikini na mafuqara na hii ni miongoni mwa sifa za taqwa.
from Muislamu Blog http://bit.ly/2WvN9I9
via IFTTT
TAARIFA YA MWANDAMO WA MWEZI: Ramadhwaan 1440H Mwezi Haukuonekana tarehe 29 Sha'baan
Baada ya kufuatilia sana maeneo mbalimbali na nchi tofauti, hakuna taarifa zozote kuwa kuna nchi mwezi umeonekana tarehe 29 Sha’baan 1440H.
Kwa hivyo, Jumapili In Shaa Allaah tutakamilisha tarehe 30 Sha’baan na hivyo basi, Ramadhwaan itaanza Jumatatu (6 Mei 2019M)
Tunawaombea Ramadhwaan yenye Baraka na yenye kughufuriwa madhambi ndani yake na yenye kuchumwa thawabu tele.
from Muislamu Blog http://bit.ly/2LpdeHH
via IFTTT
Ijumaa, 3 Mei 2019
Maandalizi Ya Ramadhwaan Kwa Faida Mbali mbali
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
Ramadhwaan 1440H Mwezi Umeonekana
اللهُ أَكْـبَر، اللّهُمَّ أَهِلَّـهُ عَلَيْـنا بِالأمْـنِ وَالإيمـان، والسَّلامَـةِ والإسْلامِ، وَالتَّـوْفيـقِ لِما تُحِـبُّ وَتَـرْضَـى، رَبُّنـا وَرَبُّكَ اللهُ.
Allaah ni Mkubwa zaidi, Ee Allaah, Uanzishe kwetu kwa amani na iymaan, na usalama na Uislamu, na tawfiyq ya kile Unachokipenda na kukiridhia, Rabb wetu na Rabb wako ni Allaah. [Swahiyh At-Tirmidhiy (3/157)]
Kwa Munaasaba wa mwezi mtukufu wa Ramadhwaan, Uislamu wangu Blog imewakusanyia faida mbalimbali za Ramadhwaan na yanayohusiana na hukmu za Swiyaam kwa ujumla.
from Muislamu Blog http://bit.ly/2WoR49h
via IFTTT
Alhamisi, 2 Mei 2019
Jumatano, 1 Mei 2019
Hiwsnul-Muslim: Utangulizi Wa Mwandishi
بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمن الرَّحيم
Hakika Himdi ni za Allaah, tunamsifu, tunamuomba msaada na tunamuomba maghfirah, tunajikinga kwa Allaah kutokana na shari za nafsi zetu, na maovu ya matendo yetu. Anayemhidi Allaah hapana wa kumpoteza, na Anayempoteza, hapana wa kumhidi. Nashuhudia kwamba, hapana mwabudiwa wa haki ila Allaah, hali ya kuwa Peke Yake, Hana mshirika, na nashuhudia kwamba Muhammad ni mja Wake na ni Rasuli Wake. Rahmah na amani zimfikie pamoja na ahli zake na Maswahaba zake na wanaowafuata hao kwa wema mpaka Siku ya malipo na Amsalimishe kwa amani nyingi.
Baada ya yaliyotangulia huu ni mukhtasari wa kitabu changu kiitwacho Hiswnul-Muslim min Adhkaaril-Kitaabi was-Sunnah.
Ninamuomba Allaah عزَّوجلَّ kwa Majina Yake mazuri, na Sifa Zake zilizotukuka, Ajaaliye kazi hii yenye ikhlaasw kwa ajili ya Radhi Zake, na Aninufaishe kwa hayo katika uhai wangu huu, na baada ya kufa, na Amnufaishe atakayekisoma, kukichapisha, au aliyekuwa ni sababu ya kukisambaza, hakika Yeye Allaah سبحانه Ndiye Mlinzi na Muweza.
Rahmah na amani zimfikie Nabiy wetu Muhammad na ahli zake na Maswahaba wake na wanaowafuata hao, kwa wema mpaka siku ya malipo.
from Muislamu Blog http://bit.ly/2ZQqc48
via IFTTT
Imaam Ibn 'Uthaymiyn: Aliyekuwa Na Deni La Ramadhwaan Iliyopita Ni Lazima Ailipe Kabla ya Ramadhwaan Nyingine Kuingia
Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) amesema:
"Hairuhusiwi kuahirisha ulipaji deni wa Swawm (ya Ramadhwaan iliyopita) hadi ikaingia Ramadhwaan nyingine bila udhuru (unaokubalika kishariy'ah).
Hiili ni kwa sababu ya maelezo ya mama wa Waumini 'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa): 'Nilikuwa na deni la Swawm ya Ramadhwaan na sikuweza kulipa ila katika Sha'baan.' [Al-Bukhaariy]
[Majaalis Shahr Ramadhwaan, uk. 59]
from Muislamu Blog http://bit.ly/2UUu28W
via IFTTT
Shaykh Fawzaan: Nasiha Kuomba Du'aa Unapokaribia Mwezi Wa Ramadhwaan
SWALI:
Nini Nasiha yenu kuhusu kukaribia mwezi wa Ramadhwaan?
JIBU:
“Ni waajib kwa Muislamu kumuomba Allaah Amfikishe Ramadhwaan au Amsaidie katika Swiyaam zake na Qiyaam (kisimamo cha usiku kuswali), na katika ‘amali zake, kwa sababu ni fursa ya uhai wa Muislamu. Anasema Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):
((مَنْ صَامَ رَمَضَانَ إِيمَانًا وَاحْتِسَابًا غُفِرَ لَهُ مَا تَقَدَّمَ مِنْ ذَنْبِهِ)) البخاري ومسلم
Amesema (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): ((Atakayefunga Ramadhwaan kwa iymaan na kutaraji malipo ataghufuriwa madhambi yake yaliyotangulia)) [Al Bukhaariy na Muslim]
Na pia,
((مَنْ قَامَ رَمَضَانَ إِيمَانًا وَاحْتِسَابًا غُفِرَ لَهُ مَا تَقَدَّمَ مِنْ ذَنْبِهِ)) رواه البخاري 37 ومسلم 759
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Atakayesimama kuswali Ramadhwaan kwa iymaan na kutaraji malipo, ataghufuriwa madhambi yake yaliyotangulia)) [Al-Bukhaariy na Muslim]
Basi Muislamu afurahie kwa kukurubia Ramadhawan na ashangalie na aupokee kwa furaha na atumie fursa katika uttifu wa Allaah katika usiku wake kwa Qiyaam (kisimamo cha kuswali usiku) na mchana wake kwa Swiyaam na kusoma Quraan na kumdhukuru Allaah, kwani hayo ni chumo la faida kwa Muislamu.
Ama wale ambao inapokaribia Ramadhwaan wanaandaa vipindi vya ufisadi na misalsalaat (michezo ya tamthilia ya televisheni) na na mishindano (ya michezo) ili wawashughulishe Waislaumu, basi hao ni askari wa mashaytwaan na mashaytwaan ni askari wao. Hivyo Muislamu atahadhari nao na ajiepusha nao. Ramadhwaan si wakati wa upuuzi wala mchezo wala misalsalaat, wala) mashindano (ya michezo) ya zawadi na upotezaji wa wakati.
from Muislamu Blog http://bit.ly/2ZQq84o
via IFTTT
Imaam Ibn Taymiyyah: Kutamka Niyyah Katika ‘Ibaadah Ni Upungufuu Katika Akili Na Dini
Amesema Shaykhul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu-Allaah):
Kutamka niyyah ni upungufu katika akili na Dini.
Ama katika Dini kwa sababu ni bid’ah, na katika akili ni kwa sababu ni sawa na ambaye anataka kula chakula husema: “Nanuia kuweka mkono wangu katika chombo hiki kwa kutaka nichote humo tonge la chakula niweke mdomoni mwangu kisha nimeze ili nishibe.”
Basi huu ni ujinga na upumbavu.
[Al-Fataawaa Al-Kubraa (2/213)]
from Muislamu Blog http://bit.ly/2USjmYl
via IFTTT
Jumamosi, 27 Aprili 2019
Hiwsnul-Muslim: Utangulizi Wa Muislamu blog
Hiwsnul Muslim (Toleo Lilohaririwa)
Utangulizi Wa Muislamu Blog
بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمن الرَّحيم
Himdi Anastahiki Allaah (سبحانه وتعالى ) Rabb wa walimwengu, Rahmah na amani zimshukie kipenzi chetu Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم ) na ahli zake, na Swahaba zake (رضي الله عنهم) na wote waliotangulia kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.
Tunamshukuru Allaah (سبحانه وتعالى) kutuwezesha kukifanyia kazi upya kitabu cha Hiswnul-Muslim ili kizidi kuleta manufaa kwa jamii yetu. Tumeonelea kwamba kuna umuhimu mkubwa wa kukifanyia kazi upya kwa kufanya yafuatayo:
1. Kuweka Aayah na Suwrah zote kamilifu ili imtosheleze msomaji kutimiza nyiradi zake zote. Mfano Suwrah ya Aliyf Miym As-Sajdah, Al-Mulk, Al-Ikhlaasw, Al-Mu’awwidhataan n.k., ambazo anatakiwa Muislamu azisome kabla ya kulala.
2. Kutaja Hadiyth ya Nabiy (صلى الله عليه وسلم) kwa ukamilifu katika baadhi ya nyiradi au du’aa yenyewe na pia katika marejeo chini ya ukurasa pamoja na kuweka tarjama yake.
3. Kuweka marejeo bayana ya Hadiyth; Raawiy (msimulizi) na Muhaddithuwna (wakusanyaji wa Hadiyth) kwa kunukuu marejeo yao. Tumebainisha marejeo ya mjalada na ukurasa katika mabano ya ( ) na tumebainisha nambari ya Hadiyth katika mabano ya [ ]. Baadhi ya sehemu tumeweza kuongezea marejeo zaidi ya yale yaliyotajwa katika kitabu cha asili.
4. Kuweka sauti za Adhkaar na Du’aa hizo pamoja na matamshi yake ili msomaji aliye na udhaifu wa kusoma Kiarabu aweze kusikiliza na kuweza kufuatilia kutamka vizuri Adhkaar na Du’aa hizo.
5. Kubainisha Ahaadiyth na Adhkaar ambazo baadhi ya ‘Ulamaa wameona kuwa hazijathibiti hivyo ni dhaifu, na badala yake kutaja ambazo zilizo Swahiyh.
6. Kubainisha nyiradi au du’aa ambazo si za Nabiy (صلى الله عليه وسلم) bali ni Athar (za Salafus-Swaalih).
7. Kuzitaja Adhkaar au Du’aa (khasa zile ambazo aghlabu hutumika kusomwa), kwa kubadilisha sarufi mfano; inapokuwa ni mwanamke au hali ya wingi, mfano Du’aa ya maiti, au Du’aa Ukiwa Na Wahka Na Huzuni (namba 120), ambayo mwanamke anapaswa aseme:
أللَّهُمَّ إنِّي أَمَتُك، بِنْتُ عَبْدِك، بنتُ أَمَتِك
Allaahumma inniy amatuka, bintu ’abdika, bintu amatika ...
Ee Allaah, hakika mimi mja Wako mwanamke, binti wa mja wako, binti wa mja Wako mwanamke...
Pia mfano wa du’aa namba (79) ya Sayyidul-Istighfaar iliyopo katika Nyiradi za Asubuhi Na Jioni ambayo inataja kwa kumkusudia mwanamume, hivyo mwanamke aseme:
اللّهـمَّ أَنْتَ رَبِّـي لا إلهَ إلاّ أَنْتَ، خَلَقْتَنـي وَأَنا أَمَتُكَ
Allaahumma Anta Rabbiy laa ilaaha illaa Anta Khalaqtaniy wa ana amatuka...
Ee Allaah, Wewe ni Rabb wangu, hapana mwabudiwa wa haki ila Wewe, umeniumba mimi na mimi ni mja Wako mwanamke...
Na kadhaalika .
8. Kumwekea msomaji asiyefahamu lugha ya Kiarabu kwa kutaja du’aa au nyiradi kamilifu kutokana na kubadilika wakati mfano du’aa namba (80) katika Nyiradi za Asubuhi Na Jioni pale inapotakiwa kubadilisha neno la
أَصْبَحْنا
Aswbahnaa (Tumeingia asubuhi)
Liwe badala yake:
أَمْسَيْنا
Amsaynaa (Tumeingia jioni)
9. Kuipa maana sahihi baadhi ya misamiati khasa ambazo zinahusiana na mas-ala ya ‘Aqiydah.
10. Kufanya ulinganifu wa misamiati na kufafanua zaidi baadhi ya maana.
11. Kutanabahisha makosa yanayotendwa na baadhi ya watu katika kutamka yasiyopasa ilhali yapasayo kutamkwa yamo katika kitabu hiki. Pia, kuongezea faida na fafanuzi ya baadhi ya maneno na kuweka tanbihi kadhaa.
Kwa ujumla tumejaribu kadiri Alivyotuwezesha Allaah (سبحانه وتعالى) kukifanyia kazi upya kwa kukiboresha ili kitoe faida kwa wingi kwa kila upande.
Marekebisho yetu hayo, hatumaanishi kwamba tutakuwa kamilifu katika kukiweka sawa kitabu hiki, kwani ukamilifu pekee ni wa Allaah (سبحانه وتعالى). Mwandishi wa Kitabu hiki amechukua juhudi kubwa kabisa kuaandaa kitabu kama hiki. Tunamuombea Allaah (سبحانه وتعالى) Amlipe malipo mazito kabisa katika Miyzaan yake ya hasanaat. Tunaomba vilevile thawabu ziwafikie pia kila atakayekifanyia kazi na kila atakayekitumia kitabu hiki.
Tunawaomba wasomaji pindi watakapoona kosa lolote lile watujulishe kupitia muislamublog@gmail.com
Tunamuomba Allaah (سبحانه وتعالى) Atusamehe makosa yetu na Atutaqabalie hii kazi iwe kwa ajili ya kupata Radhi Zake Pekee na Atulipe malipo mema kwayo.
وبِالله التَّوْفيق وَصَلَّى اللهُ وَسَلَّمَ وَبَارَكَ عَلى نَبِيِّنَا مُحَمَّدٍ وَعَلى آلِهِ وَأَصْحَابِهِ أَجْمَعِينَ
from Muislamu Blog http://bit.ly/2V15rUB
via IFTTT
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)
20-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Isti’aadhah Kwa Asiyekuwa Allaah
إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيم Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! 20 - Isti’aadhah (Kuomba Kinga) Kwa Asiyekuwa Allaah ...
-
إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيم Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! 20 - Isti’aadhah (Kuomba Kinga) Kwa Asiyekuwa Allaah ...
-
Fadhila Za Nabiy ( صلى الله عليه وآله وسلم ) 58-Masiyh Dajjaal Haingii Katika Mji Wake Wa Madiynah Alhidaaya.com Pi...
-
Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy ( صلى الله عليه وآله وسلم ): Huruma Na Upole Wake: 02-Mwenye Moyo Laini Si Mkali Wala Si Mjeuri Alhid...












