Aayah Na Mafunzo
An-Nisaa
Maana Ya Al-Kabaair Dhambi Kubwa Na Mifano Yake
Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):
إِن تَجْتَنِبُوا كَبَائِرَ مَا تُنْهَوْنَ عَنْهُ نُكَفِّرْ عَنكُمْ سَيِّئَاتِكُمْ وَنُدْخِلْكُم مُّدْخَلًا كَرِيمًا ﴿٣١﴾
Mkijiepusha na madhambi makubwa mnayokatazwa Tutakufutieni madhambi yenu madogo na Tutakuingizeni katika mahali patukufu. [An-Nisaa: 31]
Mafunzo:
Al-Kabaair (dhambi kubwa): ni lile lililotajiwa ndani yake laana, au haddi (adhabu) hapa duniani, au limeahidiwa juu yake ghadhabu za Allaah au moto.
Na Nafiy’ bin Al-Haarith Ath-Thaqafiy Abuu Bakr (رضي الله عنه) amehadithia kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Je, nikujulisheni Al-Kabaair?” Tukasema: “Ndio ee Rasuli wa Allaah! Akasema: “Kumshirikisha Allaah, na kuwaasi wazazi wawili.” Alikuwa ameegemea, akakaa kitako akasema: “Tanabahi! Na kusema uongo na kushuhudia uongo!” “Tanabahi! Na kusema uongo na kushuhudia uongo!” Akaendelea kusema hayo mpaka nikadhani hatonyamaza. [Al-Bukhaariy (5976)].
Bonyeza kiungo kifuatacho kwa faida zaidi:
Madhambi Makubwa Na Madogo
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni