أسْبابُ النُّزُول
Asbaabun-Nuzuwl
Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)
Imekusanywa na: Alhidaaya.com
017-Asbaab Nuzuwl Suwrah al-Israa Aayah 110
Kauli Yake Allaah (سبحانه وتعالى):
قُلِ ادْعُوا اللَّـهَ أَوِ ادْعُوا الرَّحْمَـٰنَ ۖ أَيًّا مَّا تَدْعُوا فَلَهُ الْأَسْمَاءُ الْحُسْنَىٰ ۚ وَلَا تَجْهَرْ بِصَلَاتِكَ وَلَا تُخَافِتْ بِهَا وَابْتَغِ بَيْنَ ذَٰلِكَ سَبِيلًا ﴿١١٠﴾
Sema; Muiteni Allaah au muiteni Ar-Rahmaan, vyovyote mtakavyomwita basi Yeye Ana Majina Mazuri kabisa. Na wala usisome kwa jahara Swalaah yako na wala usiifiche kimya kimya, bali shika njia ya wastani baina yake. [Al-Israa: 110]
Sababun-Nuzuwl:
حَدَّثَنَا مُسَدَّدٌ، عَنْ هُشَيْمٍ، عَنْ أَبِي بِشْرٍ، عَنْ سَعِيدِ بْنِ جُبَيْرٍ، عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ ـ رضى الله عنهما ((وَلاَ تَجْهَرْ بِصَلاَتِكَ وَلاَ تُخَافِتْ بِهَا)) قَالَ أُنْزِلَتْ وَرَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم مُتَوَارٍ بِمَكَّةَ، فَكَانَ إِذَا رَفَعَ صَوْتَهُ سَمِعَ الْمُشْرِكُونَ فَسَبُّوا الْقُرْآنَ وَمَنْ أَنْزَلَهُ وَمَنْ جَاءَ بِهِ. وَقَالَ اللَّهُ تَعَالَى: ((وَلاَ تَجْهَرْ بِصَلاَتِكَ وَلاَ تُخَافِتْ بِهَا)) لاَ تَجْهَرْ بِصَلاَتِكَ حَتَّى يَسْمَعَ الْمُشْرِكُونَ، وَلاَ تُخَافِتْ بِهَا عَنْ أَصْحَابِكَ فَلاَ تُسْمِعُهُمْ: ((وَابْتَغِ بَيْنَ ذَلِكَ سَبِيلاً)) أَسْمِعْهُمْ وَلاَ تَجْهَرْ حَتَّى يَأْخُذُوا عَنْكَ الْقُرْآنَ. البخاري
Ametuhadithia Musaddad kutoka kwa Hushaym kutoka kwa Abuu Bishr, kutoka kwa Sa’iyd bin Jubayr kutoka kwa Ibn ‘Abaas (رضي الله عنهما) kuhusu Kauli ya Allaah (عز وجل):
وَلَا تَجْهَرْ بِصَلَاتِكَ وَلَا تُخَافِتْ بِهَا
Na wala usisome kwa jahara Swalaah yako na wala usiifiche kimya kimya…
Amesema: “Aayah hii iliteremshwa ilhali Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amejificha Makkah. Alikuwa akiipandisha sauti yake katika kusoma Qur-aan, walipomsikia washirikina, wakaitukana Qur-aan na wakamtukana Aliyeiteremsha na aliyeileta. Basi Allaah (عز وجل) Akasema:
وَلَا تَجْهَرْ بِصَلَاتِكَ وَلَا تُخَافِتْ بِهَا
Na wala usisome kwa jahara Swalaah yako na wala usiifiche kimya kimya…
Yaani: Usiisome kwa sauti kubwa hadi kwamba washirikiana wakusikie (kisha waitukane).
وَلَا تُخَافِتْ بِهَا
na wala usiifiche kimya kimya
Yaani: Usiisome kimya kimya hadi kwamba Swahaba zako wasiisikie unapowasomea washindwe kujifunza kwayo,
وَابْتَغِ بَيْنَ ذَٰلِكَ سَبِيلًا
bali shika njia ya wastani baina yake.
Yaani: Wasikilizishe (Swahaba) kiasi cha kuisikia kwao.
[Al-Bukhaariy Kitaab At-Tawhiyd]
Pia,
عَنْ عَائِشَةَ ـ رضى الله عنها ـ قَالَتْ نَزَلَتْ هَذِهِ الآيَةُ وَلاَ تَجْهَرْ بِصَلاَتِكَ وَلاَ تُخَافِتْ بِهَا فِي الدُّعَاءِ.
Kutoka kwa ‘Aaishah (رضي الله عنها) kwamba Iliteremka Aayah hii:
وَلَا تَجْهَرْ بِصَلَاتِكَ وَلَا تُخَافِتْ بِهَا
Na wala usisome kwa jahara Swalaah yako na wala usiifiche kimya kimya...
Kasema: “Inahusiana na Du’aa.”
[Al-Bukhaariy - Kitaab At-Tawhiyd, Kitaab At-Tafsiyr, na Muslim – Kitaab Asw-Swalaah]
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni