Translate

Jumatatu, 24 Juni 2019

Kuoga Hedhi kwa Mwanamke

                                                KUOGA  HEDHI  KWA  MWANAMKE



Assallaam Aleykum WarahmatulLaah Wabarakatuh

BismiLLaah wa AlhamduliLLaah was-Swalaatu wa Salaamu ‘alaa Muhammad wa ‘alaa  aalihi wa Aswhaabihil Kiraam, wa ba’ad.

Naam Siku ya Leo tutakumbushana kuhusiana na Kuoga josho la Hedhi kwa Wanawake, Kwasababu Baadhi ya Wanawake wanafanya Makosa mengi katika Kuoga kwao baada ya kukata kwa Hedhi na KOSA kubwa baadhi wa wanawake HAWAOGI  KICHWANI hiyo wengi wanaswali hali ya kuwa bado hawapo TWAHARA (Yaani bado wapo na Hedhi na wengine wanakuwa na JANABA kwa sababu hawaogi KICHWANI).

Ni wajibu kwa mwanamke mwenye hedhi pale anapotwaharika kuosha mwili wake wote. Mtume Muhammad(Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema kumwambia Faatwimah bint Abiy Hubaysh:
“Wakati hedhi inapokuja acha swalah. Pindi hedhi yako inapoisha jisafishe na uswali.”Al-Bukhaariy (306)


Uwajibu wa chini kabisa katika kuoga ni kulowa mwili mzima ikiwa ni pamoja na mashina ya kichwa. 

Hata hivyo bora zaidi ni iwe kwa mujibu wa Hadiyth ya Mtume Muhammad(Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wakati Asmaa´ bint Shakl alipomuuliza namna gani mwanamke ataoga baada ya kutwaharika na hedhi:
“Mmoja wenu atachukua maji na mkunazi wake ajitwaharishe vizuri. Kisha ajimiminie maji kichwani mwake na akisugue kichwa msuguo wa nguvu mpaka afikilie mashina ya kichwa chake. Halafu atamwagia juu yake maji. Baada ya hapo atachukua kitambaa kilichotiwa miski ajitwaharishe nacho.” Asmaa´ akasema: “Atajitwaharisha nacho vipi?” Akasema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): “Ametakasika Allaah!” ´Aaishah akamwambia: “Utapitisha mahali palipokuwa damu.”Muslim (332).



Sio wajibu kufumua nywele ikiwa hazikukazwa sana kiasi cha kwamba kunachelea juu yake maji yasifike kwenye mashina ya nywele. Muslim amepokea kupitia kwa Umm Salamah (Radhiya Allaahu ´anhaa) ya kwamba alimwambia Mtume Muhammad(Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
Mimi ni mwanamke mwenye misuko. Je, nizifumue kwa ajili ya kuoga janaba?” Katika upokezi mwingine imekuja “kwa ajili ya kuoga hedhi na janaba? Akasema: “Hapana. Hakika yakutosha kumwagia kichwa chako mateko matatu ya maji kisha utajimiminia maji mwilini na hapo unakuwa umetwaharika.”Muslim (330).


Mwanamke akitwaharika hedhi yake katikati ya wakati wa swalah basi ni wajibu kwake kuharakisha kuoga ili aweze kuwahi kutekeleza swalah kwa wakati wake.
Na akiwa katika safari na hana maji au ana maji lakini anaogopa madhara endapo atayatumia au ana maradhi na maji yanaweza kumdhuru, basi badala yake atafanya Tayammum mpaka pale kizuizi kitapoondoka. Baada ya hapo ni wajibu kwake kuoga.
Kuna wanawake ambao wanatwaharika na hedhi katikati ya wakati wa swalah na wanachelewesha kuoga mpaka wakati wa swalah nyingine. Hoja yao ni kwamba hawawezi kujitwaharisha vizuri katika wakati huu. Hii sio hoja wala udhuru. Anaweza kuoga kwa wajibu wa chini kabisa na kuswali kwa wakati. Kisha pale atapopata wakati wa kutosha anaweza kujitwaharisha vizuri.



Rejea Kitaab Ad-Dimaa' at-Twabiy´iyyah lin-Nisaa' 



Ukiwa na Maoni/Ushauri au Swali Tafadhali wasiliana na Imaam Masjid Tawbah kwa simu +255714974397



Na  Allaah  anajua  zaidi


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

20-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Isti’aadhah Kwa Asiyekuwa Allaah

  إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيم   Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!   20 - Isti’aadhah  (Kuomba Kinga) Kwa Asiyekuwa Allaah   ...