Swali
Ni ipi hukumu ya kubakiza kucha zaidi ya siku arubaini?
Jibu
Hili linahitajia upambanuzi. Ikiwa yule mfugaji anataka kuwaiga makafiri waliopinda kutokamana na maumbile yaliyosalimika, basi kitendo hicho ni haramu.
Kwa kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Mwenye kujifananisha na watu basi yeye ni katika wao.”
Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) amesema:
“Dogo liwezalo kusemwa kuhusu Hadiyth hii ni kwamba ni haramu japokuwa udhahiri wake unapelekea katika ukafiri wa yule mwenye kujifananisha.”
Rejea Kitab Majmuu´-ul-Fataawaa (11/132)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni