Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)
21-Alikataa Kutukuzwa Mno Kama Walivyotukuzwa Manabii Wa Awali
Mojawapo wa sifa ya unyenyekevu wake Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ni kwamba hakupenda atukuzuwe kama walivyotukuzwa Manabii wa awali, na juu ya hivyo kumtukuza mno kupindukia mipaka ni kumshirikisha Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa), naye alikhofia hilo:
عن ابنِ عَبَّاسٍ رضي الله عنهما سَمِعَ عُمَرَ رضي الله عنه يَقُولُ عَلَى المِنْبَرِ: سَمِعْتُ النَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم يَقُولُ: لا تُطْرُونِي كَمَا أَطْرَتْ النَّصَارَى ابْنَ مَرْيَمَ فَإِنَّمَا أَنَا عَبْدُهُ فَقُولُوا عَبْدُ اللَّهِ وَرَسُولُهُ
Kutoka kwa ibn ‘Abbaas (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kwamba kamsikia ‘Umar (Radhwiya Allaahu 'anhu) katika minbari akisema: Nimemsikia Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: ((Msinitukuze kama Manaswara walivyomtukuza Masiyh mwana wa Maryam, hakika mimi na mja kwa hiyo semeni mja wa Allaah na Rasuli Wake)) [Al-Bukhaariy na Muslim]
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni