1.Aina ya kwanza ya majina ya haramu
Shari´ah imeharamisha kumpa mtoto majina yafuatayo:
1-Waislamu wameafikiana juu ya uharamu wa majina yote yanayoashiria kuwa mtu ni mja wa mwingine badala ya Allaah (Ta´ala). Haijalishi kitu ikiwa ni jua, mzimu, mtu au kitu kingine. Mfano wa majina hayo ya haramu ni kama ´Abdur-Rasuul, ´Abdun-Nabiy, ´Abdu ´Aliy, ´Abdul-Husayn, ´Abdul-Amiyr likiashiria kiongozi wa waumini ´Aliy bin Abiy Twaalib (Radhiya Allaahu ´anh) na ´Abdus-Swaahib likiashiria al-Mahdiy anayesubiriwa. Haya ni majina ya Raafidhwah.
Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliyabadilisha majina yote yaliyo na uja wa asiyekuwa Allaah. Baadhi ya majina hayo ni ´Abdul-´Uzza, ´Abdul-Ka´bah, ´Abdu Shams na ´Abdul-Haarith.
Ndani ya sampuli hii kunaingia vilevile jina kama Ghulaam-ur-Rasuul na Ghulaam Muhammad linaloashiria “mja wa Mtume”.
Kwa mujibu wa maoni sahihi vilevile imekatazwa kuitwa ´Abdul-Muttwalib.
Katika makosa haya kunaingia vilevile majina yenye uja ambayo mtu anafikiria makosa kwamba ni majina ya Allaah (Ta´ala). Mfano wa majina hayo ni ´Abdul-Maqswuud, ´Abdus-Sattaar, ´Abdul-Mawjuud, ´Abdul-Huwa, ´Abdul-Mursil, ´Abdul-Waahid na ´Abdul-Twaalib. Majina haya yana makosa kwa mitazamo miwili:
Wa kwanza: Haijuzu kumwita Allaah (Ta´ala) kwa jina lisilokuwa na dalili katika Qur-aan na Sunnah.
Wa pili: Haijuzu kutoa jina linaloonyesha kuwa uja anafanyiwa Allaah ikiwa Allaah hakujiita nalo Mwenyewe wala Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).
Tazama “Maraatib-ul-Ijmaa´”, uk. 154, ya Ibn Hamz na “Majmuu´-ul-Fataawaa” (01/378-379) ya Ibn Taymiyyah.
Rejea Kitab Tasmiyat-ul-Mawluwd, uk. 21-22
2.Aina ya pili majina ya haramu
2- Majina ya Allaah (Tabaarak wa Ta´ala). Haijuzu kutoa jina kwa jina ambalo ni maalum kwa Mola (Subhaanahu wa Ta´ala). Mfano wa majina hayo ni ar-Rahmaan, ar-Rahiym, al-Khaaliq na al-Baariy. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alibadilisha majina ya sampuli hiyo.
Katika Qur-aan tukufu:
هَلْ تَعْلَمُ لَهُ سَمِيًّا
“Je, unamjua mwengine mwenye Jina kama Lake?” (19:65)
Bi maana hana anayefanana Naye anayestahiki mfano wa jina Lake kama ar-Rahmaan.
Tazama “al-Jaami´ li Ahkaam-il-Qur-aan” (11/130) ya al-Qurtwubiy
Rejea Kitab Tasmiyat-ul-Mawluwd, uk. 22
3.Aina ya tatu ya majina ya haramu
3- Majina ya kigeni ambayo ni aina ya makafiri. Muislamu ambaye ana uhakika juu ya dini yake anatakiwa kujitenga nayo mbali na asiyakaribie. Leo fitina imekuwa ni kubwa katika suala hili. Majina yanatolewa Ulaya, Marekani na sehemu nyenginezo. Hii ni katika sababu baya zaidi za madhambi na udhalilishaji. Mfano wa majina hayo ni Pita, George, Diana, Rose na Susan.
Ikiwa kufuata kichwa mchunga huku kunatokamana tu na matamanio na upumbavu, basi ni dhambi kubwa. Ikiwa kunatokamana na kuoenela kuwa majina ya makafiri ni bora kuliko majina ya waislamu, basi mtu huyo yuko katika khatari kubwa ambapo msingi wa imani yake ni wenye kutikiswa. Katika hali zote mbili ni wajibu kutubia. Moja katika masharti ya tawbah ni kubadilisha jina hilo.
Rejea Kitab Tasmiyat-ul-Mawluwd, uk. 23-24
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni