Translate

Jumapili, 16 Juni 2019

Virutubisho vilivyomo kwenye matunda ya tende

Anas bin Malik amesimulia kuwa, Mjumbe wa Allah (rehema za Allah na zimshukie) amesema: “Atakayekuwa na tende kavu, afungue swaumu kwazo, na asiyekuwa nazo, afungue swaumu kwa maji, hakika maji ni twahara.” [Rejea: ‘JamiatTirmidhi, Juzuu 2, Hadithi na. 694, Tafsiri ya Abu Khalyl].

Kupitia elimu ya viumbe na tiba ya sasa, Allah Aliyetukuka ametuwezesha kufahamu kuwa, tende ni miongoni mwa matunda bora kabisa zilizojaa nguvu na virutubisho vingi.

Miongoni mwa hakika za virutubisho ambavyo Allah Aliyetukuka amevikadiria kuwamo kwenye tende ni nyuzinyuzi za lishe na baadhi ya madini muhimu, mathalan potasi, kalisi, na magnesi.

Mchanganuo

Takribani gramu 100 za tende zinaweza kutoa gramu 75 za kabohaidreti, gramu nane za nyuzinyuzi za lishe, gramu mbili za protini, na gramu 0.39 za mafuta.

Kwa nyongeza, matunda haya ni chanzo kizuri sana cha kemikali asilia za rangi za aina mbalimbali kama vile anthrocyanin, phenolics, carotenoids. Kemikali hizi hufanya tende kuwa na rangi mbalimbali; na ndizo husimama kama malighafi ya vitamini A.

Kwa ufafanuzi zaidi, kuhusu mjumuiko wa kemikali hizi asilia za rangi mbalimbali gramu 100 za tende zimejumuisha takribani IU 10 za vitamini A, miligramu 0.4 za vitamini C, maikrogramu 2.7 za vitamini K, miligramu 0.05 za vitamini E, maikrogramu 19 za folet, miligramu 0.05 za thiamini, miligramu 0.066 za riboflavin, miligramu 1.27 za niasin na miligramu 0.165 za vitamini B6.
Kuhusu madini

Pia, miligramu 100 za tende zinaweza kukupa miligramu takribani 39 za kalisi, miligramu 656 za potasi, miligramu 43 za magnesi, 62 za fosfeti, miligramu 2 za sodiamu, miligramu 1 ya chuma, miligramu 0.29 za zinki, miligramu 0.2 za kopa. Miligramu 0.26 za manganisi, na maikrogramu 3 za seleniamu.

Nguvu/nishati

Gramu 100 za tende hutoa kalori (kilo-kalori) 277. Kalori ni kipimo cha nguvu zinazotolewa baada ya kuunguzwa kwa chakula. Nguvu joto inayoweza kupasha joto kilogramu 1 ya maji kwa nyuzi 1 ya sentigredi.



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

20-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Isti’aadhah Kwa Asiyekuwa Allaah

  إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيم   Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!   20 - Isti’aadhah  (Kuomba Kinga) Kwa Asiyekuwa Allaah   ...