Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)
23-Unyenyekevu Wake Akipanda Punda Na Akiitikia Mwaliko Wa Mtumwa
عَنْ مُعَاذِ بْنِ جَبَلٍ (رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ) قَالَ: كُنْتُ رَدِيفَ اَلنَّبِيِّ (صَلَّى اَللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) عَلَى حِمَارٍ فَقَالَ لِي: ((يَا مُعَاذُ؟ أَتَدْرِي مَا حَقُّ اَللَّهِ عَلَى الْعِبَادِ، وَمَا حَقُّ الْعِبَادِ عَلَى اَللَّهِ؟)) قُلْتُ اَللَّهُ وَرَسُولُهُ أَعْلَمُ، قَالَ: ((حَقُّ اَللَّهِ عَلَى الْعِبَادِ أَنْ يَعْبُدُوهُ، وَلاَ يُشْرِكُوا بِهِ شَيْئًا، وَحَقُّ الْعِبَادِ عَلَى اَللَّهِ أَنْ لاَ يُعَذِّبَ مَنْ لاَ يُشْرِكُ بِهِ شَيْئًا)) قُلْتُ يَا رَسُولَ اَللَّهِ أَفَلاَ أُبَشِّرُ اَلنَّاسَ؟ قَالَ: ((لاَ تُبَشِّرْهُمْ فَيَتَّكِلُوا)) أَخْرَجَاهُ فِي اَلصَّحِيحَيْنِ
Imepokelewa kutoka kwa Mu’aadh bin Jabal (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: Nilikuwa nyuma ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) juu ya punda akasema: ((Ee Mu’aadh! Unajua nini haki ya Allaah juu ya waja Wake, na nini haki ya waja juu ya Allaah?)) Nikajibu: Allaah na Rasuli Wake wanajua zaidi: Akasema: ((Haki ya Allaah kwa waja wake ni kwamba wamwabudu na wasimshirikishe na chochote. Na haki ya waja kwa Allaah ni kwamba Hatomwadhibu yeyote ambaye hamshirikishi na chochote)). Nikasema: Ee Rasuli wa Allaah! Niwabashirie watu? Akasema: ((Usiwabashirie wasije kuitegemea)) [wakaacha kufanya juhudi katika ‘ibaadah])) [Al-Bukhaariy na Muslim]
Na pia:
عن أنس بن مالك ان النبي صلى الله عليه وسلم كان يُرْدِفُ خلْفَهُ ، ويضعُ طعامَهُ على الأرضِ ، ويُجِيبُ دعوةَ المملوكِ ، ويركَبُ الحمارَ
Kutoka kwa Anas bin Maalik (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akimpandisha nyuma yake (kwenye kipando) na akiweka chakula chake ardhini na akiitikia mwaliko wa mtumwa na akipanda punda. [Swahiyh Al-Jaami’ (4945)]
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni