Swali: Mimi nimemuoa mwanamke ambaye anaasi amri zangu na wala hanitii kwa kitu. Na daima anatoka nyumbani bila ya idhini yangu nakwenda kufanya baadhi ya kazi ambazo zimenifanya kunighadhibisha na kufikiria kumtaliki. Ikawa nimeandika karatasi ambapo nimeandika kuwa “nimekutaliki Talaka mbili” na nikamtaja kwa jina lake na la baba yake. Wakati huo nilikuwa nyumbani peke yangu na sikuwa na yeyote. Lakini baada ya hapo nikawa nimeichana hiyo karatasi na wala hakuna yeyote aliyejua kilichokipitika wala yeye. Na wakati huo ili-kuwa ni kabla ya miezi mitano. Talaka imepita au hapana?
Jibu: Ndio, zimepita Talaka mbili. Ukimtaliki kwa kuandika au kwa kumtakia, Talaka inakuwa imepita hata kama hukushuhudisha. Lakini umebaki na Talaka moja, ikiwa ulikuwa hujamtaliki kabla ya hapo umebaki na Talaka moja. Unaweza kumrejea, na unaweza kumchumbia tena ikiwa kishatoka ndani ya eda. Muhimu ni kuwa kumebakia Talaka moja, ikiwa ulikuwa hujamtaliki kabla ya Talaka hii uliyoandika.
Muulizaji: Kulikuwa kumeshapita miezi mitano kuanzia muda ule ambapo aliandika. Siatakuwa kishatoka ndani ya eda?
Ibn Baaz: Ndio, mara nyingi ni kuwa atakuwa kishatoka ndani ya eda kwa kupata hedhi au kwa miezi mitatu ikiwa ni eda ya mwanamke aliyokoma hedhi. Isipokuwa tu ikiwa kama ni mjamzito na hajajifungua, ni juu yake (aendelee) kukaa eda.
Muulizaji: Vipi lakini kuhusiana na muda ule tangu aandike karatasi hiyo ya Talaka, ikiwa kwa mfano (alimtaliki) katika Twahara ambayo kamwingilia.
Ibn Baaz: Kauli ya sahihi ni kuwa, ikiwa ni katika Twahara aliyomjamii au ilikuwa ni wakati wa hedhi, kauli ya sahihi ni kuwa (Talaka) haipiti. Tofauti na kauli ya wanachuoni wengi (wanaoonelea kuwa inapita).
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni