1.Aina ya kwanza ya majina yaliyochukizwa
Imechukizwa kuwa na majina yafuatayo:
1- Majina yasiyokuwa yenye kuvutia katika maana yake, matamko yake na kimoja katika hayo. Majina kama hayo yanachochea mzaha, kuudhi na uchokozi seuze tusiseme kuwa yanaenda kinyume na uongofu wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Mfano wa majina hayo ni Harb, Murrah, Khanjar, Fadhwiyh, Fahiytw, Hutwayhitw, Fadghuush… Mara nyingi majina hayo yanapatikana kwa mabedui. Mwenye kutazama kwenye orodha ya simu ataona maajabu katika pande fulani!
Majina mengine ya kuchukiza ni Huyaam na Suhaam. Yote mawili ni majina ya ngamia.
Imechukizwa vilevile kuitwa Rihaab na ´Aflaq kwa sababu yote mawili yana maana ilio mbaya.
Kadhalika Naadiyah ambayo maana yake ni “kuwa mbali na maji”.
2.Aina ya pili ya majina yaliyochukizwa
2- Imechukizwa kuitwa kwa majina yaliyo na maana ya shahawa. Wasichana wengi wanaitwa hivo. Baadhi ya majina hayo ni:
1- Ahlaam (ndoto)
2- Ariyj (harufu)
3- ´Abiyr (harufu)
4- Ghaadah (mwanamke mrembo)
5- Fitnah (fitina)
6- Nihaad (mwanamke kijana aliye na matiti yalosimama)
7- Waswaal (jimaa)
8- Faatin (anayefitinisha kwa urembo wake)
9 na 10 – Shaadiyah na Shaadiy (mwimbaji)
Tazama “as-Silsilah as-Swahiyah” (216).
3.Aina ya tatu ya majina yaliyochukizwa
3- Imechukizwa kukusudia kupeana majina ya mafusaki wendawazimu katika wachezaji wa maigizo, waimbaji na wengine wasiokuwa na maana.
Kitu kinachowafichua baadhi ya ambao hawana imani ni kwamba pindi wanapomuona mchezaji mwanamke aliye na nguo nyepesi, wanakimbilia kuwapa watoto wao wenye kuzaliwa majina yao. Mwenye kutazama orodha ya watoto wachanga wanaozaliwa ataona ukweli wa hayo
4.Aina ya nne majina yaliyochukizwa
4- Imechukizwa kuitwa kwa jina lililo na maana ya dhambi au maasi. Dhaalim (dhalimu) bin Sarraaq (mwizi). Imepokelewa namna ´Uthmaan bin Abiyl-´Aasw alivyokataa kumuajiri mtu mwenye jina kama hilo, imepokelewa na al-Fasawiy katika “al-Ma´rifah wat-Taariykh” (03/102).
5.Aina ya tano majina yaliyochukizwa
5- Imechukizwa kuitwa kwa majina ya mafirauni na majina kama Fir´awn, Qaaruun, Haamaan…
6.Aina ya sita ya majina yaliyochukizwa
6- Imechukizwa kutoa majina yasiyotamanika kama vile Khabayan bin Kannaaz. Imepokelewa kuwa ´Umar (Radhiya Allaahu ´anh) amesema juu yake:
“Hatuna nae haja. Anaficha ilihali babake anakusanya kodi.” al-Mu´talif wal-Mukhtalif (04/1965) ya ad-Daaraqutwniy.
7.Aina ya saba ya majina yaliyochukizwa
7- Imechukizwa kuitwa kwa jina la mnyama anayejulikana kwa sifa twevu. Mfano wa majina haya ni kama Hanash (nyoka), Himaar (punda), Qunfudh, Qunayfidh (mnyama aina kama ya panya aliye na manyoa mengi), Qirdaan (ngedere wawili), Kalb (mbwa) na Kulayb (kijibwa kidogo). Pindi waarabu wa kale walipowapa watoto wao majina haya ilikuwa ni kwa sababu ya zile sifa nzuri zinazopatikana katika wanyama hawa.
Kwa mfano mbwa iko na umakini na bidii, punda iko na uvumilivu na subira. Kwa ajili hiyo ikawa matusi ya watu kwa waarabu yakawa yamepotea, yamesemwa na Ibn Durayd, Ibn Faariys na wengineo.
Rejea Kitab Tasmiyat-ul-Mawluwd, uk.25-26- 27
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni