Aayah Na Mafunzo
Aal-‘Imraan
Allaah Hana Sifa Ya Makri Isipokuwa Ni Kulipiza
Kauli ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kuhusu makafiri:
وَمَكَرُوا وَمَكَرَ اللَّـهُ ۖ وَاللَّـهُ خَيْرُ الْمَاكِرِينَ ﴿٥٤﴾
54. Na wakapanga makri lakini Allaah Akapanga kulipiza makri. Na Allaah ni Mbora wa kulipiza mipango ya makri.
Mafunzo:
Sifa ya makri (njama) huthibitishwa kwa Allaah (سبحانه وتعالى) kwa njia ya muqaabalah; huthibitishwa kwa Allaah kwa maana inayoendana na Allaah (عزّ وجلّ), kwa hiyo, Allaah Anamfanyia makri (njama) yule anayestahiki na pia ambaye anayefanya makri kwa waja wake.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni