Translate

Jumatatu, 3 Juni 2019

Je, Inanyanyuliwa Mikono Katika Kila Takbiyrah Ya Ziada Kwenye Swalah Ya 'Iyd?

Suala la kunyanyua mikono kwenye Swalah ya 'Iyd katika Takbira za ziada halijathabiti kwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) bali limefanywa na Maswahaba kama Ibn 'Umar (Radhiya Allaahu 'anhuma).

Na ndio Maulamaa wakasema kutokunyanyua mikono ndio sahihi zaidi kwa sababu Mtume hakufanya hivyo.

Lakini pia wamesema ikiwa mtu atanyanyua mikono hakuna tatizo kwani baadhi ya Maswahaba walifanya hivyo.
 
Kwa hiyo, utakapokuwa unaswali Swalah ya 'Iyd, utanyanyua mikono yako katika kufunga Swalah wakati wa Takbiyratul Ihraam, kisha baada ya hapo utaiacha mikono yako kifuani bila kuinyanyua wakati unapopiga hizo Takbiyrah saba za ziada katika rakaa ya kwanza na zile tano katika rakaa ya pili.
 
Na Allaah Anajua zaidi



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

20-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Isti’aadhah Kwa Asiyekuwa Allaah

  إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيم   Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!   20 - Isti’aadhah  (Kuomba Kinga) Kwa Asiyekuwa Allaah   ...