Nini Fadhila Za Sitta Shawwaal?
Jibu
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) amesema:
"Swiyaam za Siku Sita Za Shawwaal baada ya Swiyaam za Ramadhwaan ni kama Swiyaam ya mwaka."
[Al-Fataawaa (20/17)]
Je, Swiyaam Za Sitta Shawwaal Zinapaswa Kwa Wanaume Na Wanawake?
Jibu
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) amesema:
"Ni kwa wanaume na wanawake."
[Al-Fataawaa 20/17)]
Swiyaam Za Siku Sita Za Shawwaal Ni Lazima Kuanza Baada Tu Ya 'Iydul-Fitwr?
SWALI
Je, swiyaam za Sitta Shawwaal ni lazima kuanza kufunga siku ya pili tu baada ya 'Iydul-Fitwr au inaruhusiwa kuanza baada ya siku chache?
JIBU
Si lazima kwa mtu kuanza Swiyaam baada ya siku ya kwanza ya 'Iyd, bali anaweza kuanza siku ya pili au ya tatu au hata zaidi ya masiku ndani ya mwezi huo wa Shawwaal.
Vile vile anaweza kufunga moja kwa moja bila ya kusita au kufunga na kupumzika kwani jambo hili ni dhahiri kuwa si fardhi bali ni Sunnah.
[Al-Lajnah Ad-Daaimah Lil Buhuwth Al-‘Ilmiyyaa Wal Iftaa Fatwa 3475 – Fataawaa Ramadhwaan – Majalada 2, Ukurasa 693, Fatwa Namba 698]
Kulipa Ramadhwaan Au Siku Sita Za Shawwaal? Inafaa Kulipa Jumatatu Na Alkhamiys
SWALI
Je, inafaa kufunga siku sita za Shawwaal kabla ya kulipa deni la Ramadhwaan? Na inaruhusiwa kulipa kwa kufunga siku za Jumatatu na Alkhamiys katika mwezi wa Shawwaal kwa niyyah ya kulipa deni na niyyah ya kupata thawabu za Swiyaam za Sunnah ya Jumatatu na Alkhamiys?
JIBU
Thawabu za kufunga Sittatu Ash-Shawwaal hazipatikani ila baada ya kukamilisha mwezi wa Ramadhwaan. Kwa hiyo kama mtu ana deni la Ramadhawan basi kwanza alipe deni kisha ndio afunge Siku Sita Za Shawwaal, kwani Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
مَنْ صَامَ رَمَضَانَ ثُمَّ أَتْبَعَهُ سِتًّا مِنْ شَوَّالٍ كَانَ كَصِيَامِ الدَّهْرِ
((Atakayefunga Ramadhwaan, kisha akafuatia na Sitta za Shawwaal Swiyaam zake zitakuwa kama ni Swiyaam za mwaka)) [Muslim, Abuu Daawuwd, At-Tirmidhiy, Ibn Maajah, Ahmad, Ad-Daarimiy].
Kutokana na Hadiyth hiyo tunasema kwamba, yeyote mwenye deni la Swawm ya Ramadhwaan alipe kwanza kisha ndio afunge Siku Sita Za Shawwaal. Na ikiwa Siku Sita za Shawwaal zimeangukia siku ya Jumatatu na Alkhamiys atapata thawabu zote (thawabu za Swiyaam ya Siku Sita Za Shawwaal na thawabu za Swiyaam ya Jumatatu na Alkhamiys) kwa niyyah hizo kutokana na Hadiyth ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):
(إِنَّما الأَعْمَالُ بالنِّيَّاتِ وإنَّما لكُلِّ امْرِىءٍ ما نَوَى ))
((Hakika (kusihi kwa) ‘amali kunategemea niyyah, na kila mtu atapata kwa mujibu wa kile alichokinuia))
[Imaam Ibn ‘Uthaymiyn - Fiqhul Ibaadaah, ukurasa 222, Maktabatul Iymaan]
Swiyaam Za Siku Za Sita Za Shawwaal, Je, Ni Lazima Mtu Kufunga Kila Mwaka?
SWALI
Ikiwa mtu alikuwa akifunga Sitta Shawwaal, kisha akaumwa au hakuweza kufunga kwa sababu aliona ngumu kufunga mwaka mmoja. Je, ni dhambi kwake kuacha Swiyaam hizo? Kwa sababu amesikia kwamba anayeanza kufunga Swiyaam za Sitta Shawwaal inakuwa ni lazima aendeleze kila mwaka na akiacha ni dhambi kwake. Je, ni kweli?
JIBU
Swiyaam za Siku Sita Za Shawwaal baada ya 'Iydul-Fitwr ni Sunnah.
Hivyo si fardhi kwa anayefunga mwaka mmoja au zaidi (Akiweza anafunga na asipoweza anaacha kufunga) Na si dhambi kwa anayeacha kufunga.
[Al-Lajnah Ad-Daaimah Lil-Buhuwth Al-‘Ilmiyyah Wal Iftaa Fatwa Namba 7306 - Fataawaa Ramadhwaan – Mjalada 2, ukurasa 696, Fatwa namba 702]
Swawm Za Sita Za Shawwaal Zikiangukia Jumatatu Na Alkhamiys Kunapatikana Thawabu Kwa Zote?
Jibu
Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) amesema:
"Inapoafikiana kuwa Swawm katika masiku haya sita (siku sita za mwezi wa Shawwaal) na (yakukutana) na siku ya Jumatatu au Alkhamiys, basi (mtu) hupata ujira wa (Swawm) mbili (anapofunga) kwa niyyah ya (kupata) ujira wa masiku sita (ya Shawwaal) na kwa niyyah ya (kupata) ujira wa siku ya Jumatatu au Alkhamiys, kwa kauli yake (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):
"Hakika matendo (hulipwa) kwa niyyah, na hakika kila mtu (hulipwa) kwa kile alichonuia."
[Fataawaa Islaamiyyah, mj. 2, uk. 154]
Mwenye Deni La Ramadhwaan Atapata Thawabu Za Sitta Shawaal Kabla Kufunga Deni Lake?
Imaam Ibn Baaz (Rahimahu Allaah) amesema:
"Ni waajib kukimbilia kulipa deni hata kama Sitta Shawwaal zitampita kutokana na Hadiyth iliyotajwa na kwa sababu fardhi inatangulizwa kabla ya naafil (Sunnah)."
[Al-Fataawaa (15/393)]
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) amesema:
Hawezi mtu kupata thawabu za Swiyaam za Sitta Shawwaal isipokuwa ikiwa amemaliza Swiyaam za mwezi wa Ramadhwaan.
[Al-Fataawaa (18/20)]
Vipi Kuzifunga Swiyaam Za Sitta Shawwaal?
Jibu
Imaam Ibn Baaz (Rahimahu Allaah) amesema:
"Muumini huchagua atakavo kuzifunga katika mwezi wote; akitaka afunge mwanzo wake, au katikati yake au mwishoni mwake, na akitaka afunge kwa kutofululiza, na akitaka afululize."
[Al-Fataawaa (15/390)]
Lipi Lililo Bora Katika Kufunga Sitta Shawwaal?
Jibu
Imaam Ibn Baaz (Rahimahu Allaah) Na Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah)wamesema:
"Akifanya hima kuzifunga mwanzoni mwa mwezi basi ni bora zaidi."
[Al-Fataawaa (15/390)]
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) amesema:
"Lililo bora kufanywa kuhusu Swiyaam za Sitta Shawwaal ni kuzifunga siku sita baada ya ‘Iyd na ziwe za kufufuliza."
[Al-Fataawaa (20/20)]
Je, Swiyaam Za Sitta Shawwaal Zinapaswa Kufungwa Mfulululizo?
Jibu
Imaam Ibn Baaz (Rahimahu Allaah) amesema:
"Inajuzu kuzifunga mfululizo au kutokufululiza."
[Al-Fataawaa 15/391)]
Je, Akifunga Sitta Shawwaal Atawajibika Kufunga Kila Mwaka?
Jibu
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) amesema:
"Akifunga baadhi ya miaka na akaacha baadhi ya miaka hakuna ubaya kwa sababu hiyo ni Sunnah na si fardhi."
[Al-Fataawaa (20/21]
Ni Lazima Kutia Niyyah Usiku Kwa Ajili Ya Swiyaam Za Sitta Shawwaal?
Jibu
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) amesema:
"Hakuna budi kutia niyyah kabla Alfajiri ili apate kutimiza siku hiyo."
[Al-Fataawaa (19/184)]
Vipi Kuhusu Wasemao Kuwa Swiyaam Ya Sitta Shawwaal Ni Bid’ah?
Jibu
Imaam Ibn Baaz (Rahimahu Allaah) amesema:
"Kauli hii ni batili."
[Al-Fataawaa (16/389)]
Je, Inafaa Kutanguliza Swiyyaam Za Sitta Shawwaal Kabla Ya Swiyaam Za Kafara?
Jibu
Imaam Ibn Baaz (Rahimahu Allaah) amesema:
"Lililo waajib ni kuhimiza Swiyyaam za kafara wala haijuzu kutanguliza Swiyaam za Sitta Shawwaal kabla yake kwa sababu hizo ni Naafil (Sunnah) na kafara ni fardhi ambayo ni waajib ipasayo kutimizwa haraka."
[Al-Fataawaa (15/394)]
Inafaa Kuunga Swiyaam Za Sitta Shawwaal Baada Ya Kumaliza Deni?
Jibu
Imaam Ibn Baaz (Rahimahu Allaah) amesema:
"Hakuna ubaya kufanya hivyo."
[Al-Fataawaa (15/396)]
Je, Inajuzu Kufunga Sitta Za Shawwaal Katika Mwezi Wa Dhul-Qa’dah?
Jibu
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) amesema:
"Ikiwa mfano mtu alikuwa ana deni la mwezi mzima wa Ramadhwaan kwa sababu ya kuwa safarini, au kuuguwa au kutokana na kuzaa, kisha akafunga kulipa deni mwezi wa Shawwaal na ukamalizika mwezi wote kulipa tu, basi anaweza kufunga Swiyyaam za Sitta katika mwezi wa Dhul-Qa’dah... Ama ikiwa amefanya upuuzi katika kulipa deni kisha siku zikampita asiweze kufunga deni la Ramadhwaan hadi ikafika mwisho wa Shawwaal kisha akataka kufuatilia Sitta za Shawwaal basi hii haijuzu kwake."
[Liqaat Al-Baab Al-Maftuwh (117)]
Je, Inafaaa Swiyaam Za Sunnah Bila Ya Kutanguliza Niyyah?
Jibu
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) amesema:
"Ikiwa mtu hakutia niyyah kufunga Swiyaam za Sitta Shawwaal isipokuwa akatia niyyah mchana, basi hatoandikiwa kuwa amefunga siku kamili. Basi akitia niyyah siku ya kwanza wakati wa Adhuhuri, kisha baada ya hapo akafunga siku tano, basi atakuwa hakuzipata siku sita kwa sababu amefunga siku tano na nusu, kwa vile thawabu haziandikwi isipokuwa kwa niyyah kutokana na kauli ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):
“Hakika kusihi kwa ‘amali huzingatiwa na niyyah. Na hakika kila mtu atalipwa kwa kile alichokinuia.”
Na hivyo yeye mchana wa siku hiyo hakutia niyyah kufunga kwa hivyo hapati ukamilifu wake. Naam."
[Fataawaa Nuwr ‘Alad-Darb, kanda (296)
Zipi Zinapaswa Kutangulizwa Swiyaam Za Nadhiri Au Za Sitta Shawwaal?
Jibu
Imaam Ibn Baaz (Rahimahu Allaah) amesema:
"Linalokupasa kwanza ni kufunga Swiyaam zilobakia za nadhiri kisha ndio ufunge Sitta za Shawwaal utakapoweza kwa sababu Swiyaam za Sitta Shawwaal ni mustahabb (Sunnah). Ama Swiyaam za nadhiri ni waajib.
[Mawqi’ Shaykh bin Baaz]
Nini Hikmah Ya Swiyaam Za Sitta Shawwaal?
Jibu
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) amesema:
"Hikmah yake ni kukamilisha fardhi, basi atakapofunga Swiyaam za Sitta Shawwaal ni kama vile Swalaah za Sunnah ambazo zinakuwa ni kukamilisha humo kilichopungua katika fardhi."
[Fataawaa Nuwr ‘Alad-Darb, kanda (75)]
Je, Mtu Akifunga Siku Tatu Au Tano Kwa Ajili Ya Sitta Shawwaal Atapata Thawab?
Jibu
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) amesema:
"Naam, atapata thawabu lakini hatopata thawabu ambazo ameziainisha Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) katika kauli yake:
“Atakayefunga Ramadhwaan kisha akafuatiliza na Sitta Shawwaal itakuwa kama ni Swiyaam ya mwaka” [Muslim]."
[Fataawaa Nuwr ‘Alad-Darb, Kanda (75)]
Je, Inafaa Kujumuisha Niyyah Ya Sitta Shawwaal Na Swiyaam Za Jumatatu Na Alkhamiys?
Jibu
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) amesema:
"Itakapowafikiana kuwa Swiyaam za Masiku ya Sitta Shawwaal yameangukia Jumatatu na Alkhamiys, basi atapata thawabu mbili kwa niyyah ya Swiyaam za Sitta Shawwaal pamoja na niyyah ya Jumatatu na Alkhamiys kutokana na kauli ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):
“Hakika kusihi kwa ‘amali huzingatiwa na niyyah. Na hakika kila mtu atalipwa kwa kile alichokinuia.”
[Al-Fataawaa (20/18-19)]
Je, Inafaa Kuzifanya Swiyaam Za Sitta Shawaal Kuwa Ni Kulipa Deni La Ramadhwaan?
Jibu
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) amesema:
"Swiyaam za Sitta Shawwaal hazifai kufanywa ni deni la Ramadhwaan kwa sababu siku sita hizo zinafutilia baada ya Ramadhwaan, zinafanana na Swalaah za Sunnah za Raatibah (zile Sunnah za Qabliyyah na Ba'diyyah) katika Swalaah za fardhi."
[Fataawaa Nuwr ‘Alad-Darb (175)
Na Allaah anajua zaidi
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni