Mashahidi katika talaka
Allaah (Subhaana wa Ta´ala) amesema kwamba:
فَإِذَا بَلَغْنَ أَجَلَهُنَّ فَأَمْسِكُوهُنَّ بِمَعْرُوفٍ أَوْ فَارِقُوهُنَّ بِمَعْرُوفٍ وَأَشْهِدُوا ذَوَيْ عَدْلٍ مِّنكُمْ وَأَقِيمُوا الشَّهَادَةَ لِلَّـهِ
“atakapokaribia kufikia muda wao, basi wazuieni kwa wema au farikianeni nao kwa wema na mshuhudishe mashahidi wawili wenye uadilifu katika nyinyi na simamisheni ushahidi kwa ajili ya Allaah. “65:02
Ameamrisha kuwepo mashahidi wakati mume atapomrejea mke. Ummah umeafikiana juu ya kwamba mashahidi wanatakiwa kuwepo. Wako waliosema kwamba maamrisho ni kwa njia ya uwajibu na wengine wamesema maamrisho ni kwa njia ya mapendekezo tu.
Baadhi ya watu wamedhani kuwa ushahidi ni kwa ajili ya talaka na kwamba talaka haipiti isipokuwa mpaka kuwepo mashahidi. Haya yanakwenda kinyume na maafikiano, Qur-aan na Sunnah. Hakuna yeyote katika wanachuoni wanaotambulika aliyesema hivo. Mara ya kwanza talaka iliruhusiwa kwa kuwepo mashahidi. Kuliamrishwa kuwepo kwa mashahidi wakati aliposema:
فَإِذَا بَلَغْنَ أَجَلَهُنَّ فَأَمْسِكُوهُنَّ بِمَعْرُوفٍ
“atakapokaribia kufikia muda wao, basi wazuieni kwa wema.”
Makusudio ya mtengamano katika Aayah ni kumwacha pindi eda yake itakapokwisha. Hii sio talaka, kumrejea wala kumuoa. Ni lazima wawepo mashahidi juu ya mambo haya matatu kwa maafikiano ya waislamu.
Hekima ya hilo ni kwamba shaytwaan anaweza kumshawishi mwanaume ambapo akamtaliki mwanamke kwa mara ya tatu na akalificha hilo pasi na yeyote kujua. Matokeo yake mwanamke huyo akabaki kuishi pamoja naye ilihali amekwishaharamika kwake. Ndipo Allaah akaamrisha pindi atapomrejea awashuhudishe mashahidi ili watu wajue ni mara ngapi amemwacha.
Hilo ni tofauti na talaka. Pindi mwanaume atapomtaliki mke wake itawadhihirikia watu ya kwamba sio mwanamke wake tena.
Rejea Kitab Majmuu´-ul-Fataawaa (33/33-34)
Na Allaah anajua zaidi
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni