SUNNAH BAAYA YA WUDHUU
✅Naam,Ndugu zangu katika Imaani,Leo tutakumbushana kuhusiana na Swalah ya Sunnah baada ya Wudhuu.
✅Kwahiyo baada ya kutawadha ikiwa upo nyumbani Niyyah yake ni ya Sunnah ya kutawadha.
➡Ama ikiwa upo Msikitini ndio umetawadha kisha ukaingia ndani au ulikuwa na wudhuu Niyyah kwa Swalaah hiyo itakuwa ni Tahiyyatul-Masjid.
➡Kwa Maana ya Kwamba ikiwa upo Nyumbani na Ukswali Baada ya kufanya Wudhuu, basi hapo utakuwa Umeswali Sunnah baada ya Wudhuu. Utaswali Rakaa mbili
➡Ikiwa upo Msikitini baada ya Wudhuu ukiingia Msikitini kabla ya kukaa Utaswali Rakaa mbili ambayo inaitwa Tahiyyatul-Masjid.
FADHILA ZAKE
✅Naam,Fadhila ya Kuswali Sunnah ya Wudhuu (yaani baada ya kuchukua wudhuu) ni kubwa sana.
Al-Hadiythi
‘Uqbah bin ‘Aamir (Radhiwya Allaahu ‘anhu) amesema kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema⤵
“Mmoja akichukua Wudhuu vizuri kabisa na kuswali rakaa mbili kwa moyo wake wote na uso (ukiwa katika Swalaah kwa ukamilkifu), Jannah itakuwa yake”
↪Imepokelewa na Imaam Muslim, Abu Daawuwd, Ibn Maajah na Ibn Khuzaymah
Al-Hadiythi
Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Yeyote atakayechukua Wudhuu hivi (kwa ukamilifu wake na kama alivyofundisha) na baadaye akaswali rakaa mbili bila ya kuwa na mawazo yoyote akilini mwake, atasamehewa madhambi yake yote yaliyopita”
↪Imepokelewa na Imaam Al-Bukhaariy na Muslim
Na Allaah anajua zaidi
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni