Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)
22-Unyenyekevu Wake Alipendelea Kuketi Chini Na Mto Wake Ulikuwa Duni
عن عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عَمْرٍو أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم ذُكِرَ لَهُ صَوْمِي فَدَخَلَ عَلَىَّ، فَأَلْقَيْتُ لَهُ وِسَادَةً مِنْ أَدَمٍ، حَشْوُهَا لِيفٌ، فَجَلَسَ عَلَى الأَرْضِ، وَصَارَتِ الْوِسَادَةُ بَيْنِي وَبَيْنَهُ. فَقَالَ " أَمَا يَكْفِيكَ مِنْ كُلِّ شَهْرٍ ثَلاَثَةُ أَيَّامٍ ". قَالَ قُلْتُ يَا رَسُولَ اللَّهِ. قَالَ " خَمْسًا ". قُلْتُ يَا رَسُولَ اللَّهِ. قَالَ " سَبْعًا ". قُلْتُ يَا رَسُولَ اللَّهِ. قَالَ " تِسْعًا ". قُلْتُ يَا رَسُولَ اللَّهِ. قَالَ " إِحْدَى عَشْرَةَ ". ثُمَّ قَالَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم " لاَ صَوْمَ فَوْقَ صَوْمِ دَاوُدَ ـ عَلَيْهِ السَّلاَمُ ـ شَطْرَ الدَّهْرِ، صُمْ يَوْمًا، وَأَفْطِرْ يَوْمًا ".
‘Abdullaah bin ‘Amr amehadithia kwamba alitajiwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kuhusu Swawm yangu, akanijia nikamwekea mto wa ngozi uliojazwa nyuzinyuzi za mtende, lakini aliketi chini na mto ukawa baina yake na yangu, akasema: ((Je, haikutoshelezi (Swawm) siku tatu kwa mwezi?)) Nikasema: Ee Rasuli wa Allaah (naweza Swawm zaidi ya hizo). Akasema: (([Siku] Tano)). Nikasema: Ee Rasuli wa Allaah. Akasema: ((Saba)), nikasema: Ee Rasuli wa Allaah. Akasema: ((Tisa)), nikasema: Ee Rasuli wa Allaah. Akasema: ((Kumi na moja)). Nikasema Ee Rasuli wa Allaah. Kisha Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: ((Hakuna Swawm zaidi ya Nabiy Daawuwd, ni nusu mwaka, kwa hiyo funga siku moja na kula siku moja)) [Al-Bukhaariy, Muslim]
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni