Translate

Jumatatu, 10 Juni 2019

Aina ya nane ya majina yaliyochukizwa

8.Aina ya nane ya majina yaliyochukizwa





8- Aina ya nane ya majina yaliyochukizwa ni kila jina lililo na neno “ad-Diyn” (dini) au “al-Islaam” (uislamu) kama mfano wa Nuur-ud-Diyn (nuru ya dini), Dhiyaa´-ud-Diyn (mwanga wa dini), Sayf-ul-Islaam (upanga wa Uislamu), Nuur-ul-Islaam (nuru ya Uislamu) na kadhalika. Hilo ni kwa sababu neno “ad-Diyn” na “al-Islaam” ni kubwa na majina yaliyo na tamko hili ni madai ya kina yenye kunuka uongo. Kwa ajili hiyo baadhi ya wanachuoni wameharamisha majina kama hayo ilihali wengi wao wanaonelea kuwa ni yenye kuchukizwa. Majina kama hayo yanatoa maana isiyokuwa sahihi ambayo haijuzu kuitamka. Mwanzoni yalikuwa yakitumiwa kama jina la utani, halafu baadae yakaja kuwa kama majina ya kawaida.
Isitoshe majina kama haya yanaweza kuwa yamekatazwa kwa njia mbili. Mfano wa majina hayo ni Shihaab-ud-Diyn (moto wa dini). Indonesia wamefikia kiasi cha kwamba watu wanaitwa Dhahab-ud-Diyn (dhahabu ya dini) na Maas-ud-Diyn (almasi ya dini).
an-Nawawiy alikuwa akichukia jina lake la utani Muhyiy-ud-Diyn (muhuishaji wa dini) na Shaykh-ul-Islaam (Rahimahumaa Allaah) alikuwa akichukia jina lake la utani Taqiyy-ud-Diyn (mchaji Allaah wa dini) na akisema:
“Lakini familia yangu ndio ilinipa jina hilo na likawa maarufu.”
Mtu wa kwanza aliyepata laqabu kama hiyo katika Uislamu alikuwa ni Ibn Buuyah aliyekuwa akiitwa “Rukn-ud-Diyn” (nguzo ya dini). Ilikuwa katika karne ya nne.
Mfano mwingine wa majina ya kupindukia ni “Zayn-ul-´Aabidiyn” (uzuri wa wenye kuabudu), walilokuwa wakilifupisha kwa “Zaynal”, na “Qasaam ´Aliy” (uzuri wa ´Aliy), walilokuwa wakilifupisha kwa “Qasamliy”. Na khaswa wakazi wa Baghdad wanafupisha majina “Sa´d-ud-Diyn”, “´Izz-ud-Diyn” na “´Alaa-ud-Diyn” kwenda Sa´diy, ´Izziy na ´Alaaiy.
Raafidhwah wanataja kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimpa ´Aliy bin al-Husayn bin ´Aliy bin Abiy Twaalib (Rahimahu Allaah) laqabu “Sayyid-ul-´Aabidiyn” (kiongozi wa wenye kuabudu). Hata hivyo halina asli, kama alivyosema Ibn Taymiyyah katika “Minhaj-us-Sunnah” na Ibn-ul-Jawziy katika “al-Mawdhuu´aat”. ´Aliy bin al-Husayn alikuwa ni katika waliokuja baada ya Maswahabah – ni vipi Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliweza kumpa laqabu? Allaah awaue Raafidhwah! Ni waongo wakubwa waliyoje na ni wahamnazo waliyoje!
Katika majina mabaya kabisa niliyosikia ni majina yao “Jalbullaah” ikiwa na maana ya “Kalbullaah” (mbwa wa Allaah) kwa lahja ya kiiraki. Baadhi ya Raafidhwah wanaitwa “Jalb ´Aliy”, bi maana “Kalb ´Aliy” (mbwa wa ´Aliy). Malengo ya jina hilo ni yule mpewaji jina awe ni mwaminifu kama jinsi mbwa ilivyo aminifu kwa bwana wake.



9.Aina ya tisa ya majina yaliyochukizwa




9- Aina ya tisa ya majina yaliyochukizwa ni yale majina yaliyo pamoja kama Muhammad Ahmad na Muhammad Sa´iyd. Katika hali hii Ahma ndio jina ilihali Muhammad liko kwa dhumuni la kutabaruki. Majina kama haya yanasababisha utatizi na ndio maana hayakuwa yakitambulika wakati wa Salaf. Yamejitokeza katika karne zilizokuja nyuma.
Vivyo hivyo inahusiana pia na majina yaliyo na jina “Allaah” kama Hasbullaah, Rahmatullaah na Jabrullaah. Katika hayo kunavuliwa “´Abdullaah” kwani ndio jina linalopendwa zaidi na Allaah.
Hali kadhalika inahusiana na majina yaliyo na Mtume kama Hasb-ur-Rasuul na Ghulaam-ur-Rasuul.



10.Aina ya kumi ya majina yaliyochukizwa



10- Kuna kundi la wanachuoni wameonelea kuchukizwa wanaume kuitwa kwa majina ya Malaika kama Jibraa-iyl, Mikaa-iyl na Israafiyl (´alayhimus-Salaam). Kuhusu wanawake kuitwa kwa majina ya Malaika, udhahiri ni kwamba ni haramu kuwapa majina ya Malaika kwa sababu ni kujifananisha na washirikina waliowafanya Malaika kuwa ni mabanati wa Allaah – Allaah ametakasika na wayasemayo! Majina yaliyo vilevile karibu na haya ni kumpa msichana jina la Malaak na Malakah.



11.Aina ya kumi na moja ya majina yaliyochukizwa



Wanachuoni wengi wanaonelea kuchukizwa kuitwa kwa majina ya Suurah za Qur-aan kama mfano wa Twaa Haa, Yaa Siyn, Haa Miym na kadhalika. Kuhusiana na mtazamo wa ´Awwaam kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anaitwa Twaa Haa na Yaa Siyn sio sahihi.


Rejea Kitab Tasmiyat-ul-Mawluwd, uk. 27-28-29


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

20-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Isti’aadhah Kwa Asiyekuwa Allaah

  إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيم   Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!   20 - Isti’aadhah  (Kuomba Kinga) Kwa Asiyekuwa Allaah   ...