Kulipa Deni kwanza au Kufunga Sita Shawwaal
✅Naam, Ukweli ni kwamba hivyo ndivyo khaswa inavyotakiwa kwamba mtu alipe kwanza deni lake la Ramadhaan kisha ndio afunge Sita Shawwaal.
➡Ama kusema haifai kufunga kamwe katika siku sita, kama unakusudia kusema haifa kufunga katika mwezi huu wa Shawwaal, ndio mtu alipe deni, basi hivyo sio sahihi.
➡Bali ni hivi ifuatavyo⤵
1⃣Ikiwa mtu ana deni na anataka kufunga Sita Shawwaal basi kwanza lazima afunge deni lake mwanzo katika mwezi huu wa Shawwaal ili awahi kupata siku Sita za mwezi huu wa Shawwaal kabla ya kumalizika.
2⃣Ikiwa mtu hana nia ya kufunga Sita Shawwaal na analo deni la swawm na anataka kulilipa deni, basi ni khiari yake kama atapenda kulilipa deni katika mwezi huu wa Shawwaal au mwezi wowote mwingine.
Lakini akilipa (akifunga) katika mwezi wa Shawwaal deni lake haimaanishi kwamba atapata fadhila za kufunga Sita Shawwaal kwani hivyo ni kulipa deni tu.
Na Allaah anajua zaidi
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni