Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)
23-Rasuli Pekee Aliyetumwa Kufunza Na Kutakasa Ummah
Kwa Kitabu Cha Allaah Na Sunnah Zake.
Ni Rasuli pekee ambaye Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Amemtuma kufunza na kutakasa watu wake si kwa kutokana na Kitabu cha Allaah pekee, bali na kwa Sunnah zake (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kwa sababu Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anasema:
وَمَا يَنطِقُ عَنِ الْهَوَىٰ ﴿٣﴾
Na wala hatamki kwa hawaa.
إِنْ هُوَ إِلَّا وَحْيٌ يُوحَىٰ ﴿٤﴾
Hayo si chochote isipokuwa ni Wahy unaofunuliwa. [An-Najm: 3-4]
Na imethibiti katika Hadiyth zake (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuwa amepewa Qur-aan na yanayofana nayo; Yaani ni Sunnah zake:
عَنِ الْمِقْدَامِ بْنِ مَعْدِيكَرِبَ، عَنْ رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم أَنَّهُ قَالَ (أَلَا إِنِّي أُوتِيتُ الْقُرْآنَ وَمِثْلَهُ، أَلَا يُوشِكُ رَجُلٌ يَنْثَنِي شَبْعَانًا عَلَى أَرِيكَتِهِ يَقُولُ: "عَلَيْكُمْ بِالْقُرْآنِ فَمَا وَجَدْتُمْ فِيهِ مِنْ حَلَال فَأَحِلُّوهُ وَمَا وَجَدْتُمْ فِيهِمِنْ حَرَامٍ فَحَرِّمُوهُ... ((رواه أبو داود والترمذي والحاكم وصححه وأحمد بسند صحيح
Kutoka kwa Miqdaad bin Ma’dikariby (Radhwiya Allaahu ‘anhu) ambaye amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Tanabahi! Hakika nimepewa Qur-aan na inayofanana nayo (Sunnah) Tanabahi! Utafika wakati mtu aliyeshiba mno ataegemea kwenye kochi na kusema: “Shikamaneni na Qur-aan, mtakayokuta humo ya halali halalisheni, na mtakayokuta ya haramu haramisheni.” [Imepokewa na Abu Daawuwd, na At-Tirmidhiy, na Al-Haakim na ameisahihisha Ahmad kwa isnaad Swahiyh].
Na Kauli za Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) zifuatazo zinathibitisha kupewa Kitabu na Sunnah:
لَقَدْ مَنَّ اللَّـهُ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ إِذْ بَعَثَ فِيهِمْ رَسُولًا مِّنْ أَنفُسِهِمْ يَتْلُو عَلَيْهِمْ آيَاتِهِ وَيُزَكِّيهِمْ وَيُعَلِّمُهُمُ الْكِتَابَ وَالْحِكْمَةَ وَإِن كَانُوا مِن قَبْلُ لَفِي ضَلَالٍ مُّبِينٍ ﴿١٦٤﴾
Kwa yakini Allaah Amewafanyia fadhila Waumini pale Alipomtuma kwao, Rasuli miongoni mwao, anawasomea Aayaat Zake na anawatakasa na anawafunza Kitabu na Hikmah (Sunnah); japokuwa walikuwa kabla katika upotofu bayana. [Aal-‘Imraan: 164]
‘Ulamaa wamekubaliana kwamba maana mojawapo ya Al-Hikmah ni Sunnah zake (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam).
Na Anasema pia Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):
وَاذْكُرْنَ مَا يُتْلَىٰ فِي بُيُوتِكُنَّ مِنْ آيَاتِ اللَّـهِ وَالْحِكْمَةِ ۚ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ لَطِيفًا خَبِيرًا ﴿٣٤﴾
Na kumbukeni yale yanayosomwa majumbani mwenu katika Ayaat za Allaah na Hikmah (Sunnah), hakika Allaah daima ni Mwenye kudabiri mambo kwa ulatifu, Mwenye upeo wa khabari za dhahiri na za kufichika. [Al-Ahzaab: 34]
Na Anasema pia Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):
هُوَ الَّذِي بَعَثَ فِي الْأُمِّيِّينَ رَسُولًا مِّنْهُمْ يَتْلُو عَلَيْهِمْ آيَاتِهِ وَيُزَكِّيهِمْ وَيُعَلِّمُهُمُ الْكِتَابَ وَالْحِكْمَةَ وَإِن كَانُوا مِن قَبْلُ لَفِي ضَلَالٍ مُّبِينٍ﴿٢﴾
Yeye Ndiye Aliyepeleka Rasuli kwa wasiojua kusoma wala kuandika miongoni mwao anawasomea Aayaat Zake na Anawatakasa, na Anawafunza Kitabu na Hikmah na japo walikuwa hapo kabla katika upotofu bayana. [Al-Jumu’ah: 2]
Na Anasema pia Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):
كَمَا أَرْسَلْنَا فِيكُمْ رَسُولًا مِّنكُمْ يَتْلُو عَلَيْكُمْ آيَاتِنَا وَيُزَكِّيكُمْ وَيُعَلِّمُكُمُ الْكِتَابَ وَالْحِكْمَةَ وَيُعَلِّمُكُم مَّا لَمْ تَكُونُوا تَعْلَمُونَ ﴿١٥١﴾
Kama Tulivyomtuma kwenu Rasuli anayetokana na nyinyi, anawasomea Aayaat Zetu na anakutakaseni na anakufunzeni Kitabu na Hikmah (Sunnah), na anakufundisheni mambo ambayo hamkuwa mkiyajua. [Al-Baqarah: 151]
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni