Itikadi Ya Ahlus-Sunnah Wal-Jamaa'ah Kuhusiana Na Qur-aan - 05
Je, Qur-aan Imeumbwa?
Abuu Rabiy’
Bado tunaendelea kuzitaja hoja za watu waliopinda kuhusiana na Qur-aan na twatarajia In Shaa Allaah hii kuwa ndio makala ya mwisho kuhusiana na hii maudhui adhiym.
Na ifahamike kuwa lengo si kushindana au kuumbuana kama wanavyodhani wengine, bali ni kuufahamisha ummah kuhusiana na itikadi sahihi juu ya Qur-aan, Allaah Atuwafikishe katika yale Anayoyapenda na Kuyaridhia.
Amma kauli yao kusema kuwa:
“Imegaiwa kwa vituo au kuhifadhiwa”
Majibu Yetu:
Naam kugaiwa kwa vituo, kwa sababu hii Qur-aan haikuteremshwa kwa Rasuli wetu Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) mara moja, hapana! Bali imeteremshwa kwa mnasaba na matukio.
Na hii ni kwa hikma Yake Allaah ambayo Ameibainisha katika Maneno Yake pale Aliposema:
وَقُرْآنًا فَرَقْنَاهُ لِتَقْرَأَهُ عَلَى النَّاسِ عَلَىٰ مُكْثٍ وَنَزَّلْنَاهُ تَنزِيلًا ﴿١٠٦﴾
106. Na Qur-aan Tumeigawanya sehemu mbali mbali ili uwasomee watu kwa vipindi mbali mbali; na Tumeiteremsha mteremsho wa kidogo kidogo. [Al-Israa: 106]
Hii yote inajulisha kuwa ni Maneno ya Allaah na wala Hayakuumbwa. Sasa nyinyi kwanini mwasema imeumbwa? Kwa hoja gani hapo? Au kwa kuwa kwake imeteremshwa kidogo kidogo? Je, Allaah hakuizungumza hii Qur-aan? Na Jibriyl hakumsikia Allaah akiizungumza?
Amma kushushwa kidogo kidogo, basi na’am, ni kwa lengo la kumakinika zaidi kwa wale wanaoshushiwa, na hili liko wazi sana.
Ama kusema kwenu kuwa:
“Imehifadhiwa”
Ndio imehifadhiwa kuepukikana na kubadilika na kukosolewa na viumbe Wake, na huu ni muujiza wake mkubwa kabisa Rasuli wetu Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam).
Na mtakumbuka kuwa Allaah Amewafanyia tahaddi (changamoto) wale wote wanaodai kuwa haya si Maneno Yake walete japo sura kumi au moja au mfano wa hii Qur-aan na walishindwa kuileta! Kwanini?
Kwa sababu Allaah Ameahidi kuyahifadhi Maneno Yake.
Kwa hiyo, kuhifadhiwa Maneno Yake haina maana ya kuwa yameumbwa na hii ni hoja isiyokuwa na dalili!
Ama kusema kuwa:
“Akitaka anaweza kuyaondoa”
Na’am anaweza kuyaondoa kwa sababu Yeye ndiye Mzungumzaji, na haina maana kuwa Maneno Yake yameumbwa; laa hashaa!
Anasema Allaah:
وَإِذَا بَدَّلْنَا آيَةً مَّكَانَ آيَةٍ ۙ وَاللَّـهُ أَعْلَمُ بِمَا يُنَزِّلُ قَالُوا إِنَّمَا أَنتَ مُفْتَرٍ ۚ بَلْ أَكْثَرُهُمْ لَا يَعْلَمُونَ﴿١٠١﴾
101. Na Tunapobadilisha Aayah mahala pa Aayah nyingine, na Allaah Anajua zaidi Anayoyateremsha, husema: “Hakika wewe (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) ni mtungaji (uongo).” Bali wengi wao hawajui. [An-Nahl: 101]
Na’am Allaah ndiye Aliyebadilisha ahkaam zake kwa maslahi yetu sisi wenyewe! Pana mahusiano gani ya kuwa Maneno Yake yameumbwa? Ilhali Yeye Allaah ndiye Aliyezungumza?
Amma hoja ya kusema kuwa:
“Imesifika kwa sifa ya Nuur”
Ni kweli kabisa Qur-aan ni nuru, unajua kwa sababu gani?
Kwa sababu siku zote sifa imefungamana na yule mwenye kusifiwa. Allaah Amejisifu kuwa Yeye ni nuru, sasa vipi Maneno Yake Anayoyazungumza yasiwe ni nuru?
Anasema Allaah:
اللَّـهُ نُورُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۚ…﴿٣٥﴾
35. Allaah ni Nuru ya mbingu na ardhi.
Amesema Imaam Ibn Baaz (Allaah Amrehemu):
معنى الآية الكريمة عند العلماء: أن الله سبحانه منورها، فجميع النور الذي فى السموات والأرض ويوم القيامة كله من نوره سبحانه، والنور نوران:
نور مخلوق وهو مايوجد فى الدنيا والآخرة وفى الجنة وبين الناس الآن ونور القمر والشمس والنجوم وهكذا نور الكهرباء والنار، كله مخلوق وهو من خلقه سبحانه.
أما النور الثاني فهو غير مخلوقة بل هو من صفاته سبحانه وتعالى،. والله سبحانه وبحمده بجميع صفاته هو الخالق وما سواه مخلوق، فنور وجهه عز وجل ونور ذاته سبحانه وتعالى كلاهما غير مخلوق بل هما. صفة من صفاته جل وعلا، وهذا النور العظيم وصف له سبحانه وليس مخلوقا بل هو صفة من صفاته، كسمعه وبصره ويده وقدمه وغير ذلك من صفاته العظيمة سبحانه وتعالى. وهذا هو الحق الذي درج عليه أهل السنة والجماعة.
Maana ya Aayah tukufu kwa Wanachuoni:
Kwamba Allaah ndiye mwenye kuzing’arisha nuru zote ambazo zipo samawini (mbinguni) na ardhini na nuru ya siku ya Qiyaamah, zote hizo ni katika nuru Zake Subhaanah. Na nuru ni mbili:
Nuru ambayo imeumbwa nayo ni ile iliyopo duniani na Aakhirah na katika Pepo na iliyopo kwa watu sasa, kutokana na nuru ya mwezi na jua na nyota pia nuru ya umeme na moto, zote hizi zimeumbwa, nazo ni katika uumbaji wake Subhaanah.
Ama nuru ya pili nayo ni ile ambayo haikuumbwa bali ni katika sifa Zake Subhaanahu wa Ta'aalaa, Allaah Subhaanahu na sifa nzuri ni Zake, kwa sifa Zake zote ndiye Muumba na asiyekuwa Yeye ameumbwa. Nuru ya uso Wake na nuru ya dhati Yake Subhaanahu wa Ta’aalaa zote hazikuumbwa, bali ni sifa katika sifa Zake Mtukufu Aliyekuwa juu, na hii nuru kubwa ni sifa Yake wala haikuumbwa bali ni sifa katika sifa Zake, kama kusikia Kwake na kuona Kwake na mkono Wake na nyayo Zake na zisokuwa hizi katika sifa Zake kubwa Subhaanahu wa Ta’aalaa, na hii ndio haki ambayo wameizoea Ahlus Sunnah wal Jamaa’ah.
Sasa ikiwa yeye mwenyewe ni nuru vipi Maneno Yake yasiwe ni nuru?
Na kwa dalili gani kuwa Qur-aan imeumbwa kwa sababu ni nuru?
Ama kudalilisha kwa kauli yake Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):
كان الله ولم يكن قبله شيئ
Alikuwa Allaah na hakikuwepo kabla Yake chochote.
Tunasema ni kweli kabisa hii Hadiyth kuwa Allaah Alikuwepo, lakini kama mnakumbuka katika makala ya mwanzo tulisema kuwa: Hivi vilivyokuwepo havitoki katika hukmu mbili:
Imma awe Muumba ambaye ni dhati.
Au muumbwa ambae ni dhati pia.
Na tukasema haiwezekani kuwepo dhati ambayo haina sifa, sasa kuwepo kwa Allaah ni pamoja na sifa Zake, kwa sababu sifa zake si kitu kingine na wala si Yeye, bali zinafungamana na Yeye. Ikiwa ndio hivi twasema:
Allaah Alikuwepo pamoja na sifa Zake, na katika sifa Zake ni sifa ya kuzungumza kwa sababu Allaah si bubu, na wala hatusemi kuwa Allaah Alikuwa Hazungumzi kisha akaumba sifa ya kuzungumza!!
Kwa hiyo uwepo Wake ni pamoja na sifa Zake na katika sifa Zake ni sifa ya kuzungumza na katika yale Aliyoyazungumza ni Qur-aan; sasa vipi iwe imeumbwa?
Hoja Yao Ya Saba:
Sisi sote tunaamini kuwa miongoni mwa vitabu vya Allaah ni Tawraat na Zabuwr na Injiyl na Qur-aan. Na tunaamini kuwa maneno ya Vitabu vyote hivi ni Maneno ya Allaah. Sasa hawa wanaojiita ni masalaf Maimaam wao wamepokea Hadiyth na wakaisahihisha ya kuwa Allaah Hakuumba kwa mkono Wake isipokuwa vitu vitatu; na kimoja wapo katika hivyo vitu vitatu ni Tawraat, au na Tawraat si maneno ya Allaah??
Majibu Yetu:
Kwanza riwaya zilizokuja si kuumbwa kwa Tawraat, bali riwaya zilizokuja ni kuiandika Tawraat na si kuiumba kama ilivyokuja katika Hadiyth ambayo ameipokea Imaam Al-Bukhaariy (Allaah Amrehemu) amesema:
حدثنا علي بن عبد الله حدثنا سفيان قال حفظناه من عمرو بن دينار عن طاوس سمعت أبا هريرة رضي الله عنه عن النبي صلى الله عليه وسلم:
احتج آدم وموسى فقال له موسى: يا آدم أنت أبونا خيبتنا وأخرجتنا من الجنة، قال له آدم: يا موسى اصطفاك الله بكلامه وخط لك بيده أتلومني على أمر قدره الله علي قبل أن يخلقني بأربعين سنة؟ فحج آدم موسى، فحج آدم موسى ثلاثا.
قال سفيان حدثنا أبو الزناد عن الأعرج عن أبي، هريرة.
Ametuhadithia 'Aliy ibn 'Abdillaah (bila shaka huyu ni Al-Madiyniy Shaykh wa Imaam Al-Bukhaariy) amesema: Ametuhadithia Sufyaan (huyu ni Ibn 'Uyaynah Imaam Muhaddith) amesema: Tumehifadhi kutoka kwa 'Amr (huyu ni Ibn Diynaar) Kutoka kwa Twawuws amesema nimemsikia Abuu Hurayrah (Radhi za Allaah ziwe juu yake), kutoka kwa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): Walishindana kwa hoja Aadam na Muwsaa ('Alayhimas Salaam), akasema Muwsaa (‘Alayhis Salaam): Ee Adam! Umeturusha patupu na umetutoa Peponi! Akasema Aadam (‘Alayhis Salaam): Ee Muwsaa! Amekuchagua Allaah kwa Maneno Yake, na Amekuandikia kwa mkono Wake, hivi unanilaumu kwa jambo ambalo Allaah Amenikadiria kabla ya kuniumba kwa miaka arobaini? Aadam akamshinda Muwsaa, Adam akamshinda Muwsaa mara tatu. Akasema Sufyaan: Ametuhadithia Abuu Zinaad kutoka kwa Al-A’raj kutoka kwa Abuu Hurayrah.
Kwa hiyo, katika riwaya hii hakuna mahala kunaonesha kuwa Allaah Ameumba Tawraat kwa mkono Wake! Bali Ameiandika.
Na hata riwaya ambayo huyu mteteaji wa baatwil anayetetea kuwa hata Tawraat imeumbwa! Ilhali hayo ni maneno ya Allaah, tunamwambia kuwa hakuna ndani yake neno kuumbwa Tawraat!
Kama ilivyokuja Hadiyth ambayo ameipokea Imaam Al-Bayhaqiy katika Asmaau wasw-Swifaat kutoka kwa 'Abdullaah ibn Al-Haarith ibn Nawfal amesema:
إن الله عز وجل خلق ثلاثة أشياء بيده، وخلق آدم بيده وكتب التوراة بيده وغرس جنة عدن بيده.
Hakika Allaah mwenye nguvu na utukufu ameumba vitu vitatu kwa mkono wake:
Amemuumba Adam kwa mkono wake.
Ameiandika Tawraat kwa mkono wake.
Ameipanda pepo ya 'Adan kwa mkono wake.
Na katika sanad ya Hadiyth hii kuna Isma'iyl ibn Abiy ‘Uways, yeye na baba yake wote ni madhaifu.
Na pia huyu 'Abdullaah ibn Al-Harith An-Bawfal ni taabi'iy hakumsikia Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), kwa hiyo, Hadiyth ni dhaifu.
Haya tukubalianeni na nyie bora yaishe kuwa Hadiyth hii ni sahihi (na umejua kuwa Hadiyth ni dhaifu).
Ehe wapi katika Hadiyth hii kuwa Allaah Ameumba Tawraat?
Au kitendo “KATABA” Kwenu nyinyi kina maana ya kuumba? Hebu rejea makala namba nne kwani tumebainisha neno hili kwa hoja na burhaan.
Hoja Yao Ya Nane Na Ya Mwisho
Dalili yetu nyingine kuwa Qur-aan imeumbwa ni pale itakapokuja siku ya Qiyaamah kumtetea Yule aliyeifanyia kazi, kama ilivyokuja katika Hadiyth ambayo ameipokea Imaam Muslim (Allaah Amrehemu) kutoka kwa Nawwaas Ibn Sam'aan (Radhi za Allaah ziwe juu yake) amesema:
سمعت رسول الله صلى الله عليه وسلم يقول:
يؤتى يوم القيامة بالقرآن وأهله الذين كانوا يعملون به فى الدنيا تقدمه سورة البقرة وآل عمران تحاجان عن صاحبهما.
Nimemsikia Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: Inaletwa Qur-aan na watu wake waliokuwa wakiifanyia kazi hapa duniani, inatangulia Suwratul-Baqarah na Aali 'Imraan zikimtetea aliyekuwa nazo.
Hii ni dalili ya wazi kuwa Qur-aan imeumbwa!!
Majibu Yetu:
Tunasema hivi, kufeni kwa uchungu wenu enyi wapotofu!
Wanachuoni wametuwekea msingi madhubuti sana ambao hauumizi kichwa:
إن أمور الآخرة لا تقاص بأمور الدنيا
Kwamba mambo ya Aakhirah hayafananishwi na mambo ya duniani.
Kweli kabisa! Na wala hakuna Shaka katika hilo! Sasa nyie vipi mfananishe mambo ya Aakhirah kwa mambo ya duniani?
Siku ya Qiyaamah mikono itasema ngozi zitasema n.k. Haya si mambo ya kawaida Bali matendo yako haya unayoyafanya yatapimwa!!
Kwa hiyo tunasema kuwa Hadiyth ni sahihi tena ipo mahala pake lakini kumbuka kuwa hii ni Aakhirah.
Pili: Uadilifu ni kunukulu kile ambacho kimetajwa, Hadiyth inasema Suwratul-Baqarah na Aali 'Imraan, basi mbona nyiye mnasema Qur-aan yote?
Pamoja na kuwa hata hizo Suwrah mbili zilizotajwa katika Hadiyth hazijaumbwa!
Kwa sababu ni Maneno Yake Ar-Rahmaan, ambayo Ameyazungumza na wala Hakuyaumba!
Na Wanachuoni wetu wamekhitalifiana sana kuhusiana na dalili kama hizi lakini hapa si mahala pa kutaja khilafu hiyo wa-Allaahul-Musta’aan.
Mjadala Wa Kielimu Kati Ya Imaam Ahmad ibn Hanbal As-Sunniy As-Salafiy Na Ibn Abiy Duaad Mwenye Kudai Kuwa Qur-aan Imeumbwa
Naam ndugu msomaji hapa si vibaya nikikaribia kukhitimisha hii makala yangu kwa kukunukulia huu mjadala wa kielimu, ili uweze kuyakinika zaidi na zaidi kuwa Qur-aan haijaumbwa. Angalia hoja zilizomo ndani ya huu mjadala kwa pande zote mbili kisha hukumu kwa uadilifu nani kapinda na nani yupo sawa sawa!
Na hiyo ndio itakuwa hukmu yako katika jambo hili mpaka Allaah Akufishe, usikubali kuhukumu kinyume cha hivyo.
Ndugu yangu msomaji hiki kisa ni kirefu na nitakinukulu chote kwa ajili ya faida.
Anasema Imaam Ibn Battwah (Allaah Amrehemu):
حدثنا أبو الحسن أحمد بن مطرق القاضي البستي وحدثني أبو صالح بن ثابت وأخبرني أبو بكر محمد بن الحسين قالوا حدثنا أبو عبد الله جعفر بن إدريس القزويني قال حدثنا أحمد بن الممتنع بن عبد الله القرشي التيمي قال أخبرنا أبو الفضل صالح بن علي بن يعقوب بن المنصور الهاشمي وكان من وجوه بني هاشم وأهل الجلالة والسن منهم. قال:
حضرت المهتدي بالله أمير المؤمنين رحمة الله عليه، وقد جلس ينظر فى أمور المسلمين فى دار العامة، فنظرت إلى قصص الناس تقرأ عليه من أولها إلى آخرها فيأمرنا بالتوقيع فيها، وإنشاء الكتب لأصحابها وتختم وتدفع إلى صاحبه بين يديه، فيسرني ذلك وجعلت أنظر إليه ففطن، ونظر إلي فغضضت عنه حتى كان ذلك مني ومنه مرارا ثلاثا، إذا نظر إلي غضضت وإذا اشتغل نظرت، فقال لي:ياصالح!
قلت: لبيك ياأمير المؤمنين وقمت قائما
فقال :فى نفسك منا شيئ تحب أن تقوله أو قال تحب أن تقوله؟
قلت: نعم يا سيدي يا أمير المؤمنين.
فقال: عد إلى موضعك. فعدت.
وعاد في النظر حتى إذا قام قال للحاجب: لايبرح صالح.
فانصرف الناس ثم أذن لي وقد همتني نفسي، فدخلت فدعوت له فقال لي: اجلس، فجلست.
فقال: ياصالح تقول لي مادار فى نفسك أو أقول أنا مادار فى نفسك أنه دار فى نفسك؟
قلت: ياأمير المؤمنين ماتعزم عليه وماتأمر به؟
فقال وأقول أنا كأني بك وقد اسحسنت مارأيت منا، فقلت: أي خليفة خليفتنا إن لم يكن يقول القرآن مخلوق، فورد على قلبي أمر عظيم وهمتني نفسي، ثم قلت: يانفس! هل تموتين إلا مرة واحدة وهل تموتين قبل أجلك وهل يجوز الكذب فى جد أو هزل؟
فقلت: والله ياأمير المؤمنين مادار فى نفسي إلا ماقلت!
أطرق مليا ثم قال: ويحك اسمع مني ماأقول لك، فوالله لتسمعن الحق.
فسري عني وقلت: ياسيدي! ومن أولى بالحق منك؟ وأنت خليفة رب العالمين وابن عم سيد المرسلين من الأولين والآخرين.
فقال لي: مازلت أقول إن القرآن مخلوق صدرا من خلافة الواثق حتى أقدم علينا ابن أبي دؤاد شيخا من أهل الشام من أهل أذنة.
فأدخل الشيخ على الواثق وهو جميل الوجه تام القامة حسن الشيبة.
فرأيت الواثق قد استحيا منه ورق له، فمازال يدنيه ويقربه حتى قرب منه.
فسلم الشيخ فأحسن السلام، ودعا فأبلغ وأوجز.
فقال له الواثق: اجلس! ثم قال له: ياشيخ! ناظر ابن أبي دؤاد على مايناظرك عليه!
فقال الشيخ: يا أمير المؤمنين! ابن أبي دؤاد يقل ويضعف عن المناظرة!
فغضب الواثق وعاد مكان الرقة له غضبا عليه!
فقال أبو عبد الله: ابن أبي دؤاد يصبو ويقل ويضعف عن مناظرتك أنت؟
فقال الشيخ: هون عليك ياأمير المؤمنين مابك؟ وأذن لي فى مناظرته.
فقال الواثق: ما دعوتك إلا لمناظرته.
فقال الشيخ: يا أحمد! إلى ما دعوت الناس ودعوتني إليه؟
فقال: أن تقول: القرآن مخلوق.
فقال الشيخ: يا أمير المؤمنين! إن رأيت أن تحفظ علي وعليه ما نقول؟
قال: أفعل.
فقال الشيخ: يا أحمد! أخبرني عن مقالتك هذه واجبة داخلة فى عقدة الدين، فلا يكون الدين، كاملا حتى يقال فيه ما قلت؟؟
قال الشيخ: يا أحمد! أخبرني عن رسول الله صلى الله عليه وسلم حين بعثه الله عز وجل إلى عباده، هل ستر رسول الله صلى الله عليه وسلم مما أمره الله به فى دينه؟؟
قال: لا
فقال الشيخ: فدعا رسول الله صلى الله عليه وسلم الأمة إلى مقالتك هذه؟؟
فسكت ابن أبي دؤاد!!!
فقال الشيخ: تكلم! فسكت!!!
فالتفت الشيخ إلى الواثق فقال: يا أمير المؤمنين واحدة!
فقال الواثق: واحدة.
فقال الشيخ: يا أحمد! أخبرني عن الله سبحانه حين أنزل القرآن على رسول الله صلى الله عليه وسلم فقال “ اليوم أكملت لكم دينكم وأتممت عليكم نعمتى ورضيت لكم الإسلام دينا”
كان الله عز وجل الصادق فى إكمال دينه أم أنت الصادق فى نقصانه، فلا يكون الدين كاملا حتى يقال فيه بمقالتك هذه؟؟
فسكت ابن أبي دؤاد!!!
فقال الشيخ: أجب يا أحمد، فلم يجبه!!!
فقال الشيخ: يا أمير المؤمنين! اثنتان
فقال: اثنتان
فقال الشيخ: يا أحمد! أخبرني عن مقالتك هذه علمها رسول الله صلى الله عليه وسلم، أم جهلها؟؟
فقال ابن أبي دؤاد: علمها.
فقال الشيخ: فدعا الناس إليها؟؟
فسكت ابن أبي دؤاد.
فقال الشيخ: يا أمير المؤمنين! ثلاث.
فقال الواثق: ثلاث.
فقال الشيخ: يا أحمد! فااتسع لرسول الله صلى الله عليه وسلم إذ علمها كما زعمت ولم يطالب أمته بها؟؟
قال: نعم!!!
قال الشيخ: واتسع لأبي بكر الصديق وعمر بن الخطاب وعثمان بن عفان وعلي بن أبي طالب رضي الله عنهم؟؟
فقال ابن أبي دؤاد: نعم!!!
فأعرض الشيخ عنه وأقبل على الواثق فقال: يا أمير المؤمنين! قدمت القول أن أحمد يصبو ويقل ويضعف عن المناظرة!.
يا أمير المؤمنين! إن لم يتسع لك من الإمساك عن هذه المقالة مااتسع لرسول الله صلى الله عليه وسلم ولأبي بكر وعمر وعثمان رضي الله عنهم!
فلا وسع الله على من لم يتسع له مااتسع لهم من ذلك.
فقال الواثق: نعم إن لم يتسع لنا من الإمساك عن هذه المقالة مااتسع لرسول الله صلى الله عليه وسلم ولأبي بكر وعمر وعثمان وعلي رضي الله عنهم فلا وسع الله علينا.
اقطعوا قيد هذا الشيخ.
لما قطع ضرب الشيخ بيده إلى القيد ليأخذه، فجاذبه الحداد عليه !
فقال الواثق: دع الشيخ ليأخذه
فأخذه الشيخ فوضعه فى كمه.
فقال الواثق: لم جاذبت عليه؟
قال الشيخ :لأني نويت أن أتقدم إلى من أوصى إليه إذا أنا مت، أن يجعله بيني وبين كفني حتى أخاصم به هذا الظالم عند الله يوم القيامة وأقول: يا رب! سل عبدك هذا لما قيدني وروع أهلي وولدي وإخواني بلا حق أوحب ذلك علي؟؟
وبكى الشيخ فبكى الواثق فبكينا، ثم سأله الواثق أن يجعله فى حل وسعة مما ناله.
فقال الشيخ: والله يا أمير المؤمنين! لقد جعلتك فى حل وسعة من أول يوم إكراما لرسول الله صلى الله عليه وسلم، إذ كنت رجلا من أهله.
فقال الواثق: لي إليك حاجة!
فقال الشيخ: إن كانت ممكنة فعلت.
فقال الواثق: تقيم قبلنا فينتفع بك فتياتنا.
فقال الشيخ: يا أمير المؤمنين! إن ردك إياي إلى الموضع الذي أخرجني منه هذا الظالم أنفع لك من مقامي عليك!
وأخبرك بما فى ذلك، أصير إلى أهلي وولدي فأكف دعاؤهم، فقد خلفتهم على ذلك.
فقال الواثق: فتقبل منا صلة تستعين بها على دهرك؟
فقال الشيخ: يا أمير المؤمنين! لا تحل لي أنا عنها غني. وذو مرة سوي.
قال: فاسأل حاجتك؟
قال: أوتقضيها يا أمير المؤمنين؟
قال: نعم
قال: تخلي سبيلي ساعة وتأذن لي فيه!
قال: قد أذنت لك.
فسلم عليه الشيخ وخرج.
قال صالح : قال المهتدي بالله :فرجعت عن هذه المقالة من ذلك اليوم وأظن الواثق بالله كان رجع عنها من ذلك الوقت.
Ametuhadithia Abul-Hasan ibn Muttwarif Al-Qaadhwiy Al-Bustiy, na Ametuhadithia Abuu Swaalih ibn Thaabit, na amenikhabarisha Abuu Bakr Muhammad ibn Al-Husayn, wamesema:
Ametuhadithia Abuu 'Abdillaah Ja'far ibn Idriys Al-Qazuwayniy, amesema: ametuhadithia Ahmad ibn Al-Mumtani' ibn ‘Abdillaah Al-Qurashiy At-Taymiy, amesema: Ametupa khabari Abul-Fadhwl Swaalih ibn ' Aliy ibn Ya'quwb ibn Mansuwr Al-Haashimiy, na alikuwa katika nyuso za Baniy Haashim na ni katika watu watukufu na umri miongoni mwao, amesema:
Nilimuhudhuria Muhtadiy BiLLaah, Amiyr wa Waumini (Allaah Amrehemu), amekaa akitazama mambo mbalimbali ya Waislamu ikulu.
Nikatazama visa vya watu mbalimbali vikisomwa mbele yake, mwanzo mpaka mwisho, anatuamrisha kutia saini na kuziwasilisha barua kwa wenyewe, zinagongwa mihuri na zinapelekwa kwa wenyewe mbele yake. Likawa linanifurahisha sana jambo hilo. Nikawa namtazama yeye, akajua akanitazama na mimi, nikamuinamishia (macho yangu) chini, mpaka likawa jambo hili baina yangu na yeye mara tatu! Akinitazama nainamisha chini macho yangu, akiwa anashughulika na (mambo yake) namtazama.
Akasema kuniambia: Ee Swaalih!
Nikasema: Labbayka ewe Amiyr wa Waumini.
Na pale pale nikasimama!
Akasema: Una chochote katika nafsi yako unapenda kusema kuhusiana na sisi, au unapenda kulisema?
Nikasema: Ndio bwana wangu Amiyr wa Waumini.
Akasema: Rudi mahala pako, nikarudi, na akarudia kunitazama, mpaka aliposimama akamwambia mlinzi: Asiondoke Swaalih.
Watu wakaondoka, kisha akaniruhusu mimi, na ikapata shida nafsi yangu nikaingia na kumuombea yeye.
Akasema: Kaa, nikakaa.
Akasema: Ee Swaalih! Utaniambia yale yaliyokuwa yakizunguuka katika nafsi yako au mimi nikwambie yale yaliyokuwa yanazunguuka kwenye nafsi yako kuwa yalikuwa yanazunguuka?
Nikasema: Ee Amiyr wa Waumini! Nini umeazimia na nini unaamrisha?
Anasema, na mimi nasema kama wewe, umeyafanya vizuri yale uliyoyaona kwetu sisi, ukasema, kiongozi gani (alie mzuri) kuliko kiongozi wetu! Ikiwa hatosema kuwa Qur-aan imeumbwa.
Likapatikana katika nafsi yangu jambo kubwa na ikapata dhiki sana nafsi yangu (juu ya kusadikisha maneno yake na wakati ni ya ukweli).
Kisha nikasema (Kuilingania nafsi yangu) Ee nafsi! Hivi unakufa isipokuwa mara moja? Na haufi kabla ya muda wako na haijuzu uongo ima ukiwa makini au katika utani.
Nikasema (kumwambia Amiyr), naapa kwa Allaah ee Amiyr wa Waumini! Hayakupita katika nafsi yangu ila yale uliyoyasema!!
Akainiamisha kichwa chake muda kidogo kisha akasema: Ole wako! Nisikilize Mimi nini ninasema kukwambia wewe! Naapa kwa Allaah utaisikia haki!
Likanifurahisha sana na nikasema: Ee bwana wangu! Na ni nani aliyekuwa mbora zaidi wa haki kuliko wewe? Wewe ni Khaliyfah wa Maula wa ulimwengu wote, na ni mtoto wa ‘amiy wa bwana wa Mitume wa mwanzo na wa mwisho.
Akasema: Sikuacha kusema kuwa Qur-aan imeumbwa mwanzo wa utawala wa Al-Waathiq, mpaka alipokuja kwetu Ibn Abiy Duaad Shaykh kutoka Shaam katika mji wa Adhinah.
Akaingizwa Shaykh (anamkusudia Imaam Ahmad) kwa Al-Waathiq akiwa mzuri wa uso, umbile la sawa sawa mvi zake zinapendeza.
Nikamuona Al-Waathiq anamuonea haya na kumuhurumia, hakuacha kumsogeza kwake na kumuweka karibu.
Akamsalimia Shaykh, Shaykh akajibu kwa uzuri zaidi, na akamuombea yeye. Shaykh akazidisha zaidi (kumuombea) na kufupisha.
Al-Waathiq akamwambia Shaykh (Imaam Ahmad), kaa! Kisha akamuambia: Ee Shaykh! Jadiliana na Ibn Abiy Duaad katika yale ambayo yeye atajadiliana na wewe.
Akasema Shaykh: Ee Amiyr wa Waumini! Ibn Abiy Duaad anakuwa mdogo na anakuwa na udhaifu katika majadiliano.
Akachukia sana Al-Waathiq! Na akaondosha huruma (Kwa Imaam Ahmad) kwa kumchukia!!
Akasema Abuu ‘Abdillaah: Ibn Abiy Duaad anakuwa na mchezo na mapungufu na madhaifu katika kujadiliana na wewe?
Akasema Shaykh: jiwepesishie ee Amiyr wa Waumini! Nipe idhini nijadiliane nae.
Akasema Al-Waathiq: Sijakuita hapa ila kwa lengo la kujadiliana nae.
Akasema Shaykh (Imaam Ahmad): Ee Ahmad (Ibn Abiy Duaad), unawalingania kitu gani watu pamoja na mimi?
Akasema (Ibn Abiy Duaad), seme kuwa Qur-aan imeumbwa!!
Akasema Shaykh: Ee Amiyr wa Waumini! Ikiwa utaona kuhifadhi (kuyaandika) yangu mimi na yake katika yale tunayoyasema.
Akasema Al-Waathiq: Nitafanya.
Akasema Shaykh: Ee Ahmad (Ibn Abiy Duaad)! Hebu nikhabarishe kutokana na haya maneno yako (kuwa Qur-aan imeumbwa) ikiwa ni wajibu na inaingia katika vifungu vya dini, ikawa dini haiwi kamili mpaka yasemwe ndani yake haya unayoyasema?
Akasema Shaykh: Ee Ahmad! Hebu nikhabarishe kuhusiana na Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) wakati Allaah alipomtuma kwa waja wake; je, alificha Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) katika yale aliyoamrishwa na Allaah kufikisha katika dini yake?
Akasema: Hapana!!
Akasema Shaykh: Je, Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alilingania ummah wake kuhusiana na haya maneno yako??
Akanyamaza Ibn Abiy Duaad!
Akasema Shaykh: Zungumza! Akanyamaza!!
Shaykh akamgeukia Al-Waathiq akamwambia: Ee Amiyr wa Waumini! La kwanza hilo (ambalo Ibn Abiy Duaad ameshindwa kujibu).
Akasema Al-Waathiq: La kwanza hilo.
Akasema Shaykh: Ee Ahmad! Nikhabarishe kutoka kwa Allaah wakati Alipoiteremsha Qur-aan kwa Rasuli Wake (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) “Leo nimekukamilishieni dini yenu na nimewatimizieni neema Zangu na nimeridhia kuwa Uislamu ndio dini.” Allaah alikuwa ni Mkweli katika kuikamilisha dini Yake au wewe ni mkweli katika kuipunguza kwani haiwi kamili dini mpaka yasemwe hayo maneno yako?
Akanyamaza Ibn Abiy Duaad!
Akasema Shaykh: Jibu ee Ahmad?
Hakujibu!!!
Akasema Shaykh: Ee Amiyr wa Waumini la pili hilo.
Akasema Al-Waathiq: La pili hilo.
Akasema Shaykh: Ee Ahmad! Nikhabarishe kuhusiana na maneno yako haya; je, Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa anayajua au alikuwa hayajui?
Akasema Ibn Abiy Duaad: Alikuwa anayajua.
Akasema Shaykh: Je, aliwalingania watu?
Akanyamaza Ibn Abiy Duaad!
Akasema Shaykh: Ee Amiyr wa Waumini! La tatu hilo.
Akasema Al-Waathiq: La tatu hilo.
Akasema Shaykh: Ee Ahmad! Je, lilimuenea na kumpanukia Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kama alilijua kama ulivyodai na wala hakuwataka ummah wake waseme?
Akasema Ibn Abiy Duaad: Ndio. (Naona kajibu kwa khasira baada ya kushindwa hoja).
Akasema Shaykh: Ilimuenea Abuu Bakr Swiddiyq na kumpanukia na 'Umar ibn Al-Khattwaab na 'Uthmaan ibn 'Affaan (Radhi za Allaah ziwe juu yao)?
Akasema Ibn Abiy Duaad: Ndio (kajibu kwa khasira huyu).
Shaykh akampuuza na akamuelekea Al-Waathiq na kumuambia: Ee Amiyr wa Waumini! Nilitanguliza kauli kuwa Ibn Abiy Duaad ana mchezo na ni mpungufu na dhaifu katika mjadala, ee Amiyr wa Waumini!
Ikiwa haijakutosha wewe kujizuia kuepukikana na maneno haya basi pia haikumtosha Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) wala Abuu Bakr wala 'Umar wala 'Uthmaan wala 'Aliy (Radhi za Allaah ziwe juu yao). Basi asimtosheleze Allaah Yule ambae haikumtosha yeye yale ambayo yamewatosha wao.
Akasema Al-Waathiq: Ndio ikiwa haijatutosheleza sisi kutokana na kujizuia na haya maneno basi haikumtosha Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) wala Abuu Bakr na 'Umar na 'Uthmaan na 'Aliy, basi Allaah asitutosheleze sisi.
Hebu kateni pingu za huyu Shaykh, walipomkata akapiga Shaykh kwa mkono wake ile pingu, ili aichukue, wakaivuta wale watengeneza vyuma!
Akasema Al-Waathiq: Mwacheni Shaykh aichukue.
Shaykh akaichukua na kuiweka katika mkono wa kanzu.
Akasema Al-Waathiq: Kwanini uliivuta?
Akasema Shaykh: Kwa sababu Mimi nilinuia kuitanguliza kwa yule ambaye niliyemusia kuwa mimi nikifa aiweke baina yangu na sanda yangu ili nigombane nae huyu dhwaalim mbele ya Allaah siku ya Qiyaamah, na nitasema: Ee Rabb wangu! Hebu muulize mja Wako huyu kwanini alinifunga pingu na akawaogopesha familia yangu na mtoto wangu na ndugu zangu pasina haki ameiwajibisha juu yangu?
Akalia Shaykh na Akalia Al-Waathiq na tukalia sote!
Kisha akamtaka Al-Waathiq amjaalie katika uhuru na upana kwa yale aliyoyapata.
Akasema Shaykh: Naapa kwa Allaah ee Amiyr wa Waumini! Nimekujalia kuwa huru na upana tangia siku ya kwanza, kwa lengo la kumkirimu Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kwasabu wewe ulikuwa ni katika watu wake.
Akasema Al-Waathiq: Nina haja kutoka kwako?
Akasema Shaykh: Ikiwa inawezekana basi naifanya.
Akasema Al-Waathiq: Ukae kwetu wakanufaika kupitia wewe vijana wetu?
Akasema Shaykh: Ee Amiyr wa Waumini! Hakika kunirudisha kwangu mimi mahala aliponitoa huyu dhwaalim kuna manufaa makubwa zaidi kuliko kuishi hapa! Na nitakukhabarisha katika hili nitakavyokuwa nimefika kwa Ahli yangu na mtoto wangu nawazuia kuendelea na du’aa zao! Kwani nimewaacha wao wakifanya hivyo!
Akasema Al-Waathiq: Basi tukubalie sisi kiunga undugu ambacho kitakusaidia katika maisha yako?
Akasema Shaykh: Ewe Amiyr wa Waumini! Si halali kwangu mimi, mimi ni tajiri! Na tena mwenye nguvu na afya njema.
Akamwambia: Taja shida yako?
Akasema: Utakubali ee Amiyr wa Waumini?
Akasema Al-Waathiq: Ndio.
Akasema: Uniache niende saa nzima na unipe idhini.
Akasema: Nimekupa idhini.
Shaykh akatoa salaam na kuondoka!
Akasema Swaalih: Amesema Muhtadiy BiLLaah: Nikajirudi kuepukikana na haya maneno (na huu msimamo wa kuwa Qur-aan imeumbwa) tangia siku hiyo! Na nadhania kuwa Al-Waathiq BiLLaah alikuwa amejirudi tangia wakati ule.
Ndugu msomaji, utanisamehe sana kuunukulu huu mjadala wote, lakini lengo na dhamira ni kukutaka wewe ufahamu kuwa kati ya Imaam Ahmad na Ibn Abiy Duaad ni nani aliyekuwa na utambuzi na maarifa zaidi.
Na angalia kwa umakini namna gani Imaam Ahmad (Allaah Amrehemu) aliumaliza mzozo huu mbele ya Amiyr kwa kuzitaja hizi nukta tatu muhimu!
Na kwa nukta hizi twaweza kusema kuwaambia Maibadhi na mapote mengine ambayo yamepinda:
1. Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) maneno yenu haya aliyajua au hakuyajua? Na kama aliyajua; je, aliulingania ummah wake hii kauli?
2. Maneno yenu haya ni katika msingi wa dini kwa namna ambayo dini haiwezi kukamilika mpaka mtu aweze kuulingania na kuitakidi haya maneno yenu?
3. Ikiwa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Maswahaba wake hawakulingania maneno haya kwanini nyie mlinganie na kuandika na kurusha mitandaoni na kuungana wa bara na baharini kwa lengo la kutaka kuwanyamazisha Masalafi?
Na wala maswali haya hatuwezi kuulizwa sisi kwa sababu sisi tumebaki katika asli na dalili. Kuwa Allaah anasifika na sifa ya kuzungumza. Na Qur-aan ni katika Maneno Yake ambayo ameyazungumza na wala hakuyaumba kama msemavyo nyie!!
Sasa nyinyi mnayesema kuwa imeumbwa; mnayo hayo maswali matatu yanawasubiri myajibu!
Khaatimah:
Ndugu msomaji unatakiwa ufahamu kuwa hoja ya kuwa Qur-aan imeumbwa imekuja kwa lengo la kutaka kuzikanusha sifa za Allaah!
Na wala hili halikujulikana ila baada ya zile quruun (karne) tatu zilizokuwa bora!
Na wala usidhani kuwa wana dalili yoyote ambayo inawasapoti hapana Wa-Allaahi! Bali ni kujaribu kutumia akili zao na kujaribu kuzichomeka dalili mahala ambapo si pake!
Na ndio maana ukiwaambia turejeeni kwenye Qur-aan na Sunnah kwa ufahamu wetu! Utapigwa chenga na falsafa tele!
Unajua kwanini?
Kwa sababu akili kila mmoja ana zake, na rai kila mmoja anayo ya kwake, sasa lazima tuheshimiane katika matumizi ya akili na rai!
Na unapowaambia jamani turejeeni kwenye Qur-aan na Sunnah kwa ufahamu wa wema waliotangulia (Salafus-Swaalih)! We! Utaradiwa na kutukanwa wewe na hao wema waliotangulia pamoja na kudhalilishwa!
Unajua kwanini?
Kwa sababu wewe unawafungamanisha watu katika dini iliyokuwa sahihi ambayo imerithiwa kutoka kwa Rasuli watu Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), na hili wao hawalitaki, bali wanataka uhuru wa rai, fikra, na muono!!
Na ndio maana kila anayelingania hili wanakuwa mbele za watu hawa ni maadui wakubwa sana tena ni vibaraka wa Marekani na Uingereza!!
Kwa kosa gani?
Kosa lako ati umewarejesha watu katika dini iliyokuwa salama na usahihi.
Kwa hiyo, ndugu yangu Muisilamu, rejea katika dini yako mzima mzima wala usiwe mguu ndani mguu nje!
Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa):
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا ادْخُلُوا فِي السِّلْمِ كَافَّةً وَلَا تَتَّبِعُوا خُطُوَاتِ الشَّيْطَانِ ۚ إِنَّهُ لَكُمْ عَدُوٌّ مُّبِينٌ ﴿٢٠٨﴾
208. Enyi walioamini! Ingieni katika Uislamu kikamilifu, na wala msifuate hatua za shaytwaan. Hakika yeye kwenu ni adui wa wazi. [Al-Baqarah: 208]
Usizuzuke na maneno ya wazungumzaji wala makala zao na vipeperushi vyao!
Mpaka ufahamu kuwa wapi wameichukua hii dini yao.
Hii elimu ni dini basi atazame mmoja wenu wapi anaichukua dini yake.
Kama nitakuwa nimepatia basi inatoka kwa Allaah, na kama nitakuwa nimekosea basi kosa limetoka kwangu na shaytwaan.
Subhaanaka Allaahumma wa bihamdika ash-hadu alla Ilaaha illa Anta Astaghfiruka wa atuwbu Ilayka.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni