Baadhi ya maimamu wanasema:
“Allaah haitazami safu iliyopinda.”
Hii sio Hadiyth. Haijuzu kuwaambia watu maneno haya. Kwa kuwa ni kitu hakikuthibiti kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na wala hakina msingi. Msemo:
“Allaah hatazami… “
ni katika sifa za Allaah. Kwa ajili hiyo haijuzu kulithibitisha isipokuwa kwa dalili. Inatosheleza kusema yale yaliyosemwa na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Tukiona mtu amesogea mbele kidogo au amebaki nyuma kidogo tuseme:
“Waja wa Allaah! Mtazisawazisha safu zenu au Allaah atatofautisha kati ya nyuso zenu.”
Bi maana nyoyo zenu.
Kuhusu kusema:
“Allaah haitazami safu iliyopinda.”
hata kama yanasemwa na baadhi ya maimamu, lakini hata hivyo ni jambo lisilokuwa na msingi na wala haijuzu kulisema watu wakaja kuitakidi kuwa ni Hadiyth kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ilihali hayatoki kwa Mtume wa Allaah.
Rejea Kitaab al-Liqaa' ash-Shahriy (16)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni