4.Aina ya nne majina ya haramu
4- Majina ya masanamu yanayoabudiwa badala ya Allaah kama mfano wa al-Laat, al-´Uzzaa, Isaaf, Naa-ilah na Hubal.
5.Aina ya tano ya majina ya haramu
5- Majina ya kigeni kama ya kituruki, ya kifursi na ya kishenzi yasiyopata nafasi katika kiarabu. Mfano wa majina hayo ni Nariymaan, Sherihaan, Shaadiy (likiwa na maana ya ngedere kwenye lugha yao) na Jiyhaan.
Kuhusu majina yanayoisha kwa herufi “t” kama Hikmat, ´Iswmat, Najdat, Hibat, Mirfat na Ra-fat, asli ni ya kiarabu. Lakini kwa vile yanaisha kwa “t” badala ya “h” sio ya kiarabu tena.
Hali kadhalika majina ya kuisha kwa herufi “iy” kama Ramziy, Husniy, Rushdiy, Haqqiy, Majdiy na Rajaaiy. Asli ya majina haya ni ya kiarabu. Midhali yanaisha kwa “iy” sio ya kiarabu tena kwa sababu iy hii ni jambo la kifursi na kituruki.
Kuhusu jina Faqiy Misri, ni ufupisho wa “Faqiyh”.
Mfano wa majina ya kifursi ni yale yenye kuisha kwa “uuyah” kama Siybuuyah. Kuna ambao wamefikisha mpaka majina tisini na mbili yenye kuisha kwa “uuyah”.
Katika kiurdu wanaweka herufi “iy” ikiwa jina ni la kike. Rahmaan inakuwa Rahiyman naa Kariym inakuwa Kariyman.
6.Aina ya sita ya majina ya haramu
6- Jina lisiloendana na yule mpewaji kwa sababu ima ni madai, kujitakasa au uongo ambalo halikubaliki kabisa. Mfano wa hayo ni yale yaliyotajwa katika Hadiyth iliyothibiti kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliyesema:
“Jina lenye kutwezwa zaidi kwa Allaah ni mtu mwenye kujiita “Mfalme wa wafalme”…. “
Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim.
Hali kadhalika majina kama hayo yaliyoharamishwa na Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kama Mfalme wa wafalme, Hakimu wa mahakimu na Qaadhiy wa maqadhiy.
Humo kunaingia vilevile majina kama Bwana wa watu, Bwana wa wote, Bwana wa mabwana na bwana wa wanawake. Ni haramu pia mbali na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuitwa “Bwana wa wanaadamu”. Zaynab bint Abiy Salamah (Radhiya Allaahu ´anhaa) ameeleza kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Msizitakase nafsi zenu. Allaah ndiye anawajua wema zaidi katika nyinyi.”
Ameipokea Muslim.
Rejea Kitab Tasmiyat-ul-Mawluwd, uk. 24-25
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni