Nifasi na eda ya talaka
Hukumu za nifasi ni zile zile kama hukumu za hedhi isipokuwa katika mambo yafuatayo:
Jambo la kwanza Eda inaisha kwa kuzaa na sio kwa nifasi. Talaka ikipitika kabla ya kuzaa basi eda inaisha kwa kuzaa na si kwa nifasi.
Na ikiwa talaka itapitika baada ya kuzaa, basi itabidi asubiri mpaka pale atapopata hedhi halafu aangalizie hapo.
Jambo la pili Kipindi cha Ilaa´ kiko pamoja na hedhi na si nifasi. Ilaa´ maana yake ni mume kuapa kuwa hatofanya jimaa na mke wake kabisa au chini chini miezi mine.
Akifunga kiapo hicho na mke akamtaka wafanye jimaa ambapo akakataa, ana miezi mine kuanzia ile siku alipofunga kiapo. Baada ya muda kutimia atalazimika kufanya naye jimaa.
La sivyo mke ataomba talaka. Ikiwa ndani ya muda huu atapata nifasi, muda huu hauhesabiki kwa mume.
Miezi minne hiyo itakuwa ni ya kipekee pasi na nifasi. Tofauti na hedhi ambayo miezi mine hiyo itahesabika kwa mume.
Jambo la tatu Kubaleghe kunajulikana kwa hedhi na si kwa nifasi. Kwa kuwa mwanamke hawezi kushika mimba mpaka amwage usingizini.
Anabaleghe kwa kumwaga usingizini kabla ya kushika ujauzito.
Jambo la nne Damu ya hedhi ikikatika kisha ikarejea katika ada basi inahesabika bila ya shaka kuwa ni damu ya hedhi. Mfano wa hilo ada ya mwanamke ni kwa siku nane. Baada ya siku nne damu yake ikakatika kwa siku mbili na halafu siku ya saba na ya nane ikarudi tena. Damu hii iliyorudi ni hedhi pasina shaka yoyote na kutathibiti hukumu za hedhi.
Ama kuhusu nifasi, damu ikikatika kabla ya siku arubaini kisha ikarudi tena ndani ya siku arubaini, damu hii itazingatiwa ni yenye kutia shaka. Kwa hivyo itakuwa ni wajibu kwa mwanamke kuswali na kufunga faradhi kwa wakati wake na ni haramu kwake kufanya yale ambayo ni haramu kwa mwanamke mwenye hedhi mbali na mambo ya wajibu.
Baada ya kutwaharika atalipa zile ´ibaadah alizofanya katika kipindi cha damu hii yenye kutia shaka kama jinsi ni wajibu kwa mwanamke mwenye hedhi kulipa yale yaliyompita. Haya ndio maoni yanayojulikana kwa wanachuoni wa Hanaabilah.
Hata hivyo kauli sahihi ni kuwa maadamu damu inatoka katika kipindi cha nifasi inahesabika kuwa ni nifasi. Vinginevyo ni damu ya hedhi. Damu ikiendelea kutoka pasina kukatika inahesabika kuwa ni damu ya ugonjwa. Haya yanashabihiana na yale Ibn Qudaamah aliyotaja katika “al-Mughniy”[al-Mughniy (1/349).] kutoka kwa Imaam Maalik ambaye amesema:
“Akipata damu siku mbili au tatu baada ya kuwa imekatika, inahesabika kuwa ni nifasi. Vinginevyo ni damu ya hedhi.”
Maoni haya ndio muqtadha wa chaguo la Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah. Uhakika wa mambo ni kuwa hakuna damu yenye kutia mashaka. Mambo yote yako wazi wazi kwa kutegemea ujuzi na uelewa wa watu. Qur-aan na Sunnah imebainisha kila kitu.
Allaah (Subhaanah) hakumuwajibishia yeyote kufunga mara mbili au kufanya Twawaaf mara mbili ikiwa matendo hayo hayakufanywa kimakosa na hapo yakahitajia kurudiliwa. Pindi mja anapofanya kiasi na anavyoweza basi ameitakasa dhimma yake.
Allaah (Subhaana wa Ta´ala) amesema:
لَا يُكَلِّفُ اللَّـهُ نَفْسًا إِلَّا وُسْعَهَا
“Allaah Hakalifishi nafsi yoyote ila kwa kadiri ya uwezo wake.” (02:286)
فَاتَّقُوا اللَّـهَ مَا اسْتَطَعْتُمْ
“Basi mcheni Allaah muwezavyo.” (64:16)
Jambo la tano Mwanamke damu yake ikikauka ndani ya ada, inafaa kufanya jimaa na mume wake. Ni jambo ambalo halikuchukizwa kabisa. Hata hivyo ni jambo lenye kuchukiza kufanya naye jimaa akikauka katika damu ya uzazi wake ndani ya siku arubaini. Hii ndio kauli yenye kujulikana katika madhehebu [ya Hanaabilah].
Kauli sahihi ni kuwa haikuchukizwa kabisa kufanya naye jimaa. Hii ndio kauli ya wanachuoni wengi. Machukizo ni hukumu ya Kishari´ah inayohitajia dalili ya Kishari´ah. Hakuna katika masuala haya dalili isipokuwa ile aliyotaja Imaam Ahmad kutoka kwa ´Uthmaan bin Abiyl-´Aasw na kwamba mke wake alimjia ndani ya zile siku arubaini ambapo akasema:
“Usinikaribie.”
Hili halilazimishi kuwa imechukizwa. Huenda alisema hivo kwa njia ya usalama kwa kukhofia kwamba hakuwa na yakini juu ya kutwahatika kwake, damu yake kurudi kwa sababu ya jimaa au sababu nyengineyo na Allaah ndiye anajua zaidi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni