Naam, Kwanza kabisa
‘Ulaama wamekhitilafiana kuhusu wakati wa mwanzo kabisa kutoa Zakaatul-Fitwr na kuna rai mbali mbali:
1- Kwamba itolewe siku mbili kabla ya 'Iyd. Hii ni rai ya madhehebu ya ki-Maaliki na ki-Hanbaliy. Wamenukuu dalili ya Hadiyth ya 'Ibn 'Umar (Radhwiya Allaahu anhumaa) ambaye amesema: Walikuwa wakitoa Zakaat al-Fitwr siku moja au mbili kabla (Ya 'Iyd) [Al-Bukhaariy 1511]
Wengineo wamesema inaweza kutolewa siku tatu kabla ya 'Iyd kutokana na masimulizi katika al-Mudawwanah (1/385) ambayo Imaam Maalik amesema: "Naafi' ameniambia kwamba Ibn 'Umar alikuwa akituma Zakaatul-Fitwr aliyokuwa akiikusanya siku mbili au tatu kabla (ya 'Iyd) al-Fitwr.
Rai hii imependekezwa na Shaykh Ibn Baaz (Rahimahu Allaah) kama inavyotaja katika Majmuw' Al-Fataawa (14/216)
2- Inaruhusiwa kuitoa kuanzia mwanzo wa Ramadhwaan. Hii ni rai ya madhehebu ya ki-Hanafiy na ni rai iliyo sahihi kutokana na Shaafi'iy. Taz al-Umm (275), al-Majmuw' (6/87) na Badaa'i As-Sanaa'i (2/74).
Wamesema: Kwa kuwa sababu ya kutoa swadaqa ni kufunga Swawm na kufungua, hivyo ikiwa sababu moja kati ya hizo mbili itakuwa inapatikana, inaruhusiwa kuharakisha kuitoa hiyo Zakaa, ni kama ilivyo rukhsa ya kuharakisha kutoa Zakaah ya mali wakati inapofikia mali hiyo kiwango cha Nisaab na kabla ya kupitwa na mwaka.
3- Inaruhusiwa kuitoa mwanzo wa mwaka. Hii ni rai ya baadhi ya ma-Hanafi na ma-Shaafi'iy. Wamesema: Kwa sababu ni Zakaah na wameihusisha na Zakaah ya mali ya mtu kuhusu kuitoa mapema katika hali zote.
Rai iliyo sahihi kabisa ni ya kwanza.
Ibn Qudaamah kasema katika al-Mughniy (2/676)
“Sababu kuhusu kwa nini ni fardhi wakati wa kumalizika Swawm ambayo inaashiriwa kutokana na suala kwamba imetajwa katika kuambatana nayo. Hikma yake ni kuwafanya masikini wawe wa kujitegemea kwa mahitajio katika wakati maalumu hivyo hairuhusiwi kuitoa mapema zaidi ya wakati huo” [Mwisho wa kunukuu].
Imaam Muhammad bin Swaalih al-'Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) aliulizwa kama ilivyotajwa katika Majmuw' al-Fataawa (18/Zakaatul-Fitwr Swali Namba 180):
Nilitoa Zakaatul-Fitwr mwanzo wa Ramadhwaan Misr kabla ya kuja Makkah, na sasa naishi Makkah al-Mukarramah. Je nilipe Zakaatul-Fitwr tena?
Akajibu:
Ndio, inabidi ulipe Zakaatul-Fitwr kwa sababu ulilipa kabla ya wakati kuwadia.
Ibara ‘Zakaatul-Fitwr’ ni kutokana na maneno mawili, ambayo yanaelezea sababu ya kufuturu (kumalizika Swawm - Fitwr).
Hivyo Zakaatul-Fitwr imetajwa kuambatana na fitwr (kufungulia Swawm) kwa sababu hiyo ndio sababu yake na inajulikana kwamba kufungulia (kumalizika Ramadhwaan) kunakuwa ni siku ya mwisho ya Ramadhwaan. Hivyo haifai kutoa Zakaatul-Fitwr ila baada ya jua kuzama siku ya mwisho, isipokuwa ikiwa kuna hali ambayo shariy’ah inaruhusu kuitoa siku moja au mbili kabla. Ikiwa si hivyo basi wakati wake unaostahiki ni baada ya jua kuzama siku ya mwisho ya Ramadhwaan kwa sababu wakati huo ndio wakati ambao Swawm inafunguliwa (inamalizika msimu wake). Hivyo tunasema kuwa ni bora kutoa asubuhi ya 'Iyd ikiwezekana" [mwisho wa kunukuu]
Pili:
Inaruhusiwa kutoa Zakaatul-Fitwr yako kumpa anayewakilisha kuzigawa kupitia vyama ya ukusanyaji michango ya sadaka au watu wanaoaminika n.k. mwanzo wa mwezi (wa Ramadhwaan) madamu utawasisitiza kuwa itolewe siku moja au mbili kabla ya 'Iyd. Kwa sababu njia iliyo sahihi kuilipa ni kuwapa masikini na wanaohitaji. Hivi ndivyo ilivyotajwa katika shariy’ah kwamba imewekewa mipaka ya siku moja au mbili kabla ya 'Iyd. Kuwakilishwa kwa ajili ya kupokea na kugawa (Zakaatul-Fitwr) inakuja katika mas-alah ya ushirikiano kwa wema na kufadhiliana na hakuna muda wa mipaka kwa hayo.
Na Allaah anajua zaidi
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni