Translate

Jumamosi, 18 Mei 2019

Mwanamke Kwenda Kuswali Tarawiyh Kwa Kuvunja Amri Ya Mumewe

SWALI

Mwanamke akitoka kwenda kuswali Taraawiyh msikitini na mumewe hayuko radhi naye, kwani alimwambia aswali nyumbani atapata thawabu; je, Swalaah yake imesihi?


JIBU

Tunamuambia mume usimzuie mkewe kwenda kuswali msikitini kwani Nabiy amekataza hivyo. Amesema: ((Msiwakataze wanawake kwenda katika nyumba za Allaah))[Muslim]

Na tunamwambia mke: “Mtii mume wako maana bila shaka amekukataza kwa maslaha au khofu ya fitnah kama alivyosema kuwa Swalaah yako nyumbani ni bora kuliko msikitini kutokana na kauli ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ((Na nyumba zao ni bora kwao))


[Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)]


http://bit.ly/2JrK3lw i live islam

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

20-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Isti’aadhah Kwa Asiyekuwa Allaah

  إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيم   Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!   20 - Isti’aadhah  (Kuomba Kinga) Kwa Asiyekuwa Allaah   ...