SWALI
Je, mwanamke ambaye anayetwaharika baada tu ya alfajiri atafunga siku inayobaki, au ni juu Yake kulipa siku hiyo?
JIBU
Ikiwa mwanamke atatwaharika baada tu ya Alfajiri, Wanachuoni wana kauli mbili kuhusiana na Swawm yake:
Rai ya kwanza: Anapaswa kufunga siku iliyobaki bila ya kupewa thawabu ya siku hiyo. Kisha baadaye ni waajib kwake kulipa siku hiyo. Hii ni kauli maarufu katika madhehebu ya Imaam Ahmad (Rahimahu Allaah).
Rai ya pili: Hana haja ya kufunga siku iliyobaki. Swawm yake ni batili (ikiwa atafunga) siku hiyo kwa kuwa alianza siku hali ya kuwa ni mwenye hedhi na si kama mwenye Swawm. Kwa hiyo hali kama hii Swawm yake si sahihi, hakuna faida yoyote ya yeye kufunga.
Wakati huo hauna faida kwake. Kaamrishwa kujiepusha na kufunga katika siku za mwanzo ya siku hiyo. Kwa kuwa amekatazwa kufunga wakati huo (wa hedhi). Msingi wa Shariy’ah kuhusiana na Swawm kama tujuavyo sote ni kuacha chakula na kunywa kuanzia Alfajiri mpaka jioni tukiwa na niyyah ya kumuabudu Allaah kwa hilo.
Tunaamini kuwa mtazamo huu ni wenye nguvu zaidi kuliko mtazamo unaosema afunge siku nzima iliyobaki. Hata hivyo maoni zote mbili ni waajib kwake kulipa siku hiyo.
[Imaam Ibn ‘Uthyamiyn - Sualaat ‘An Ahkaamil-Haydhw, uk. 9-10]
http://bit.ly/2HqxeFR i live islam
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni