Swali
Kuna mtu amesilimu baada ya kupita masiku kadhaa ya Ramadhaan. Je, ni lazima kwake kulipa masiku yaliyompita?
Jibu
Huyu hahitajii kulipa masiku yaliyompita. Kwa sababu kipindi hicho alikuwa ni kafiri.
Kafiri hahitajii kulipa matendo mema yaliyompita. Allaah (Ta´ala) amesema:
قُل لِّلَّذِينَ كَفَرُوا إِن يَنتَهُوا يُغْفَرْ لَهُم مَّا قَدْ سَلَفَ
“Waambie wale waliokufuru kwamba wakikoma watasamehewa yaliyotangulia.”08:38
Mtume Muhammad(Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakuwa akiwaamrisha wale wenye kusilimu kulipa swawm, swalah au zakaah zilizowapita. Lakini iwapo atasilimu katikati ya mchana ni lazima kujizuia na kuilipa siku hiyo au ajizuie na asilipe siku hiyo au haimlazimu kujizuia wala kulipa?
Wanachuoni wametofautiana juu ya mambo haya.
Maoni yenye nguvu ni kwamba analazimika kujizuia na kutoilipa siku hiyo kwa sababu ameingia miongoni mwa watu ambao wanawajibika, lakini halazimiki kuilipa siku hiyo kwa sababu kabla ya hapo hakuwa miongoni mwa watu wanaowajibika.
Yeye ni kama mtoto ikiwa atabaleghe katikati ya mchana; atalazimika kujizuia siku hiyo na wala hatolazimika kuilipa. Hayo ndio maoni yaliyo na nguvu katika masuala haya.
Rejea Kitab Majmuu´-ul-Fataawaa (19/96-97)
http://bit.ly/2X1Qfnp i live islam
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni