Translate

Jumanne, 28 Mei 2019

Hukmu ya Zakaatul-Fitwr, na ni Kiasi gani Ilipwe?

SWALI


Ikiwa Muislamu anayefunga ni muhitaji asiye miliki Niswaab (Kiwango chenye kuhitajika kutolewa Zakaah) ya Zakaah, je anawajibika kulipa Zakaatul-Fitwr kwa sababu ya usahihi wa Hadiyth hiyo au shariy’ah iliyo sahihi nyingine iliyothibitika katika Sunnah?


JIBU

AlhamduliLLaah

Swadaqah ya Al-Fitwr (Zakaatul-Fitwr) ni wajibu kwa Muislamu mwenye uwezo wa kujitegemea mwenyewe ikiwa anayo swaa’ (pishi) moja au zaidi ya mahitajio yake ya chakula chake na familia yake mchana na usiku ya 'Iyd.

Hii ni kutokana na usimulizi uliosimuliwa na Ibn 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) amesema: "Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliwajibisha kutoa swaa’ (pishi) ya tende au swaa’ ya shayiri (ngano) kuwa ni Zakaatul-Fitwr iliyowajibika kwa Waislamu wote, mtumwa aliye huru, mwanamke na mwanamume, kijana na mzee, na akaamrisha kwamba itolewe kabla ya watu kwenda kuswali (Swalaatul-'Iyd) [Al-Bukhaariy 1503]

Abuu Sa'iydAl-Khudriyy (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: "Tulikuwa tukilipa Zakaatul-Fitwr swaa’ (pishi) moja ya chakula, au swaa’ ya shayiri (ambacho ndicho kilichokuwa chakula chao zama hizo) au swaa’  ya tende au swaa’ ya zabibu au swaa’ ya aqit" (mtindi mkavu) [Al-Bukhaariy Na Muslim]


Inakubalika kutoa swaa’ ya chakula wanachotumia sana watu wa mji kama mchele n.k. Lililomaanishwa kwa swaa’ hapa ni swaa’ ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ambayo ni mara nne ya kipimo kitakachojaza vitanga viwili vya mikono vya mtu wa umbo la kawaida. (takriban ni kilo 2½ mpaka 3). Ikiwa mtu hatolipa Zakaatul-Fitwr atakuwa anafanya dhambi hivyo itabidi ailipe.

Na Allaah ni Mweza wa yote.


[Fataawaa Al-Lajnah Ad-Daaimah]


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

20-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Isti’aadhah Kwa Asiyekuwa Allaah

  إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيم   Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!   20 - Isti’aadhah  (Kuomba Kinga) Kwa Asiyekuwa Allaah   ...