Aayah Na Mafunzo
Aal-‘Imraan
Mkiwa Mnampenda Allaah Basi Mfuateni Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم):
قُلْ إِن كُنتُمْ تُحِبُّونَ اللَّـهَ فَاتَّبِعُونِي يُحْبِبْكُمُ اللَّـهُ وَيَغْفِرْ لَكُمْ ذُنُوبَكُمْ ۗ وَاللَّـهُ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿٣١﴾
31. Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): “Mkiwa mnampenda Allaah, basi nifuateni mimi, Atakupendeni Allaah na Atakughufurieni dhambi zenu. Na Allaah ni Mwingi wa kughufuria, Mwenye kurehemu.
Mafunzo:
Aayah hii tukufu inathibitisha kuwa mapenzi ya Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) hayawezi kutimia isipokuwa kwa kufuta Sunnah zake, na ni hoja ya wazi kwa wanaodai wanampenda Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) lakini wakafanya bid’ah katika Dini kama kusoma Mawlid, Khitmah, Talqiyn, Du’aa za uzushi n.k. na hali yeye mwenyewe Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ameonya katika Hadiyth aliyohadithia Mama wa Waumini ‘Aaishah (Radhwiya Allaahu ‘anhaa) kwamba: ((Atakayetenda ‘amali isiyokuwa yetu (katika Dini yetu) basi kitarudishwa)) [Al-Bukhaariy].
Hadiyth ifuatayo ni dalili ya jinsi Maswahaba Walivyompenda Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم):
Katika Hadiyth iliyopokelewa na ‘Abdu-Rahmaan bin Quraad (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kuwa “Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa anatawadha, na Maswahaba wakaanza kukinga maji yaliyokuwa yanatiririka kutoka katika wudhuu wa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na wakijifutia katika miili yao kutafuta baraka za wudhuu ule kutoka kwa Nabiy. Kisha Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akawauliza; ((Kwa nini mnafanya hivi?)) Wakasema; ni kwa ajili ya kumpenda Allaah na Rasuli Wake. Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)) akawaambia: ((Anayetaka kumpenda Allaah na Rasuli Wake, au kupendwa na Allaah na Rasuli Wake, basi aseme ukweli anapozungumza, na atekeleze amana yake anapoaminiwa, na awe jirani mwema kwa jirani yake)) [Al-Albaaniy ‘Mishkaatul Maswaabiyh’]
http://bit.ly/2HNujGe
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni