Translate

Jumamosi, 18 Mei 2019

Kuomba Du’aa baada ya Kutoa Zakaah

Kuomba Du’aa baada ya Kutoa Zakaah


Inapendeza kumuombea dua mtoaji Zakaah, pale anapoitoa.
Allaah Anasema:
خُذْ مِنْ أَمْوَالِهِمْ صَدَقَةً تُطَهِّرُهُمْ وَتُزَكِّيهِم بِهَا وَصَلِّ عَلَيْهِمْ إِنَّ صَلاَتَكَ سَكَنٌ لَّهُمْ
"Chukua Swadaqah katika mali zao, uwasafishe na kuwatakasa kwa ajili ya hizo (Swadaqah zao) na kuwataja kwa vizuri (mbele yangu) na uwaombee du'aa. Hakika kuwaombea kwako kutawapa utulivu. "
[At-Tawbah: 103]

Kutoka kwa ‘Abdullaah bin Abi ‘Awfiy amesema:
“Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa anapoletewa mali ya Zakaah akisema: "ALlaahumma salliy ‘alayhim". Na baba yangu siku moja alimpelekea mali ya Zakaah akasema: "Allaahumma salliy ‘alaa aali Abi ‘Awfiy".
[Ahmad na wengineo].

Imepokelewa kutoka kwa Waail bin Hujr kuwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alimuombea mtu mmoja aliyeleta ngamia wa Zakaah akasema:
"Allaahumma Baarik fiyhi wa fiy ibilihi". (Allaah mbariki yeye na katika ngamia wake)

Anasema Imaam Ash-Shaafi’iy:
"Ni Sunnah kwa Imaam anapopokea mali ya Zakaah kumuombea dua mtoaji kwa kumwambia: "Aajaraka Allaahu fiyma a’atwayta, wa baarik laka fiyma abqayta".
(Allaah akupe ujira mwema katika ulichotoa na akubarikie katika kilichobaki).


http://bit.ly/2VAMjIK i live islam

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

20-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Isti’aadhah Kwa Asiyekuwa Allaah

  إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيم   Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!   20 - Isti’aadhah  (Kuomba Kinga) Kwa Asiyekuwa Allaah   ...