Swali
Kuna tabia ilioenea kati ya watu ambapo wanakwenda katika misikiti ilio mbali na manyumba yao. Hilo ni kwa sababu ya kutafuta maimamu walio na sauti nzuri. Ni yapi maoni yako juu ya tabia hii?
Jibu
Imamu anatakiwa kujaribu kusoma Qur-aan vizuri na atilie umuhimu wa kuimairi Qur-aan kwa njia inayotakikana. Afanye hivo kwa kutarajia ujira kutoka kwa Allaah na isiwe kwa ajili ya kutaka kujionyesha na kusikika.
Jengine ni kwamba anatakiwa kusoma Qur-aan kwa unyenyekevu na kwa kuuhudhurisha moyo ili yeye mwenyewe kwanza aweze kunufaika na kisomo chake na wale wengine wenye kumsikiliza.
Kinachotakiwa kwa kamati za misikiti zote ni wao kuimarisha misikiti yao kwa kumtii Allaah na kuswaliwe ndani yake. Haitakiwi kuzunguka kati ya misikiti na kupoteza muda kwa ajili tu ya kutafuta imamu mwenye sauti nzuri. Haya yanawahusu khaswa wanawake.
Hakika kutanga kwao na kwenda kwao mbali na manyumba yao kuna ukhatari mkubwa. Kwa sababu linalopaswa kutoka kwa mwanamke ni yeye kuswali nyumbani kwake. Endapo atataka kutoka kwenda msikitini, basi atoke kwenda katika msikiti ulio karibu zaidi kwa ajili ya kupunguza ukhatari.
Tabia hii si yenye kufurahisha. Kwa sababu ndani yake kuna kuizorotesha misikiti mingine. Vilevile ni jambo linapelekea katika kujionyesha, ndani yake pia kuna kujikakama ambalo hakukuwekwa katika Shari´ah na kupetuka.
http://bit.ly/2HBLdZe i live islam
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni