Translate

Alhamisi, 23 Mei 2019

060-Asbaab-Nuzwul: Al-Mumtahinah Aayah: 10

 أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya  Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)

 

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

 

060-Al-Mumtahinah Aayah: 10

 

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

 يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِذَا جَاءَكُمُ الْمُؤْمِنَاتُ مُهَاجِرَاتٍ فَامْتَحِنُوهُنَّ ۖ اللَّـهُ أَعْلَمُ بِإِيمَانِهِنَّ ۖ فَإِنْ عَلِمْتُمُوهُنَّ مُؤْمِنَاتٍ فَلَا تَرْجِعُوهُنَّ إِلَى الْكُفَّارِ ۖ لَا هُنَّ حِلٌّ لَّهُمْ وَلَا هُمْ يَحِلُّونَ لَهُنَّ ۖ وَآتُوهُم مَّا أَنفَقُوا ۚ وَلَا جُنَاحَ عَلَيْكُمْ أَن تَنكِحُوهُنَّ إِذَا آتَيْتُمُوهُنَّ أُجُورَهُنَّ ۚ وَلَا تُمْسِكُوا بِعِصَمِ الْكَوَافِرِ وَاسْأَلُوا مَا أَنفَقْتُمْ وَلْيَسْأَلُوا مَا أَنفَقُوا ۚ ذَٰلِكُمْ حُكْمُ اللَّـهِ ۖ يَحْكُمُ بَيْنَكُمْ ۚ وَاللَّـهُ عَلِيمٌ حَكِيمٌ﴿١٠﴾

10. Enyi walioamini! Wanapokujieni Waumini wa kike waliohajiri basi wajaribuni. Allaah Mjuzi zaidi wa iymaan zao. Kisha mkiwatambua kuwa ni Waumini basi msiwarejeshe kwa makafiri. Wao si wake halali kwao, na wala wao waume hawahalaliki kwao. Na wapeni (makafiri mahari) waliyotoa. Na wala si dhambi kufunga nao nikaah mkiwapa mahari yao. Na wala msiwaweke wanawake makafiri katika fungamano la ndoa; na takeni mlichotoa (katika mahari), nao watake walichotoa. Hiyo ndio hukumu ya Allaah, Anahukumu baina yenu, na Allaah ni Mjuzi wa yote, Mwenye hikmah wa yote.

 

 

Sababun-Nuzuwl:  

 

حَدَّثَنَا يَحْيَى بْنُ بُكَيْرٍ، حَدَّثَنَا اللَّيْثُ، عَنْ عُقَيْلٍ، عَنِ ابْنِ شِهَابٍ، قَالَ أَخْبَرَنِي عُرْوَةُ بْنُ الزُّبَيْرِ، أَنَّهُ سَمِعَ مَرْوَانَ، وَالْمِسْوَرَ بْنَ مَخْرَمَةَ، رضى الله عنهما يُخْبِرَانِ عَنْ أَصْحَابِ، رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم قَالَ لَمَّا كَاتَبَ سُهَيْلُ بْنُ عَمْرٍو يَوْمَئِذٍ كَانَ فِيمَا اشْتَرَطَ سُهَيْلُ بْنُ عَمْرٍو عَلَى النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم أَنَّهُ لاَ يَأْتِيكَ مِنَّا أَحَدٌ وَإِنْ كَانَ عَلَى دِينِكَ إِلاَّ رَدَدْتَهُ إِلَيْنَا، وَخَلَّيْتَ بَيْنَنَا وَبَيْنَهُ‏.‏ فَكَرِهَ الْمُؤْمِنُونَ ذَلِكَ، وَامْتَعَضُوا مِنْهُ، وَأَبَى سُهَيْلٌ إِلاَّ ذَلِكَ، فَكَاتَبَهُ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم عَلَى ذَلِكَ، فَرَدَّ يَوْمَئِذٍ أَبَا جَنْدَلٍ عَلَى أَبِيهِ سُهَيْلِ بْنِ عَمْرٍو، وَلَمْ يَأْتِهِ أَحَدٌ مِنَ الرِّجَالِ إِلاَّ رَدَّهُ فِي تِلْكَ الْمُدَّةِ، وَإِنْ كَانَ مُسْلِمًا، وَجَاءَ الْمُؤْمِنَاتُ مُهَاجِرَاتٍ، وَكَانَتْ أُمُّ كُلْثُومٍ بِنْتُ عُقْبَةَ بْنِ أَبِي مُعَيْطٍ مِمَّنْ خَرَجَ إِلَى رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم يَوْمَئِذٍ وَهْىَ عَاتِقٌ، فَجَاءَ أَهْلُهَا يَسْأَلُونَ النَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم أَنْ يَرْجِعَهَا إِلَيْهِمْ، فَلَمْ يَرْجِعْهَا إِلَيْهِمْ لِمَا أَنْزَلَ اللَّهُ فِيهِنَّ((‏إِذَا جَاءَكُمُ الْمُؤْمِنَاتُ مُهَاجِرَاتٍ فَامْتَحِنُوهُنَّ اللَّهُ أَعْلَمُ بِإِيمَانِهِنَّ))‏ إِلَى قَوْلِهِ: ((‏وَلاَ هُمْ يَحِلُّونَ لَهُنَّ‏))

Ametuhadithia Yahyaa bin Bukayr, ametuhadithia Al-Layth toka kwa ‘Uqayl toka kwa bin Shihaab amesema, amenieleza ‘Urwah bin Az-Zubayr ya kuwa amemsikia Marwaan na Al-Mis-wara bin Makhramah (Radhwiya Allaahu ‘Anhumaa) wakielezea kuhusu Maswahaba wa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu álayhi wa aalihii wa Sallam) amesema, Suhayl bin ‘Amri alipoandikishiana mkataba siku hiyo, kati ya shuruti alizomwekea Suhayl bin ‘Amri Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihii wa Sallam) ni kwamba asikujie yeyote kutoka kwetu hata kama ameiamini Dini yako ila utamrejesha kwetu, na utatuachia sisi uamuzi wa nini cha kumfanya. Waislamu walilichukia hilo, na halikuwafurahisha, na Suhayl hakukubali jingine lolote isipokuwa hilo tu. Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihii wa Sallam) akaandikishiana naye mkataba kuhusiana na hilo. (Rasuli) akamrejesha siku hiyo Abuu Jandal kwa baba yake Suhayl bin ‘Amri, na hakumjia mwanaume yeyote ila alimrejesha hapo hapo hata kama ni Muislamu. Wakaja wanawake Waumini waliohajiri, na Ummu Kulthuwm bint ‘Uqbah bin Abiy Mu’aytw ni kati ya hao waliotoka kuja kwa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihii wa Sallam) siku hiyo akiwa binti ndiye kwanza amevunja ungo. Watu wake wakaja kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihii wa Sallam) wakimtaka awarejeshee (binti yao huyu), na Rasuli hakuwarejeshea kwa sababu ya Aliyoyateremsha Allaah kuhusiana na akina mama hao:

 

 إِذَا جَاءَكُمُ الْمُؤْمِنَاتُ مُهَاجِرَاتٍ فَامْتَحِنُوهُنَّ ۖ اللَّـهُ أَعْلَمُ بِإِيمَانِهِنَّ ۖ  

Wanapokujieni Waumini wa kike waliohajiri basi wajaribuni. Allaah Mjuzi zaidi wa iymaan zao.

 

Mpaka kauli Yake:

  وَلَا هُمْ يَحِلُّونَ لَهُنَّ ۖ  

wala wao waume hawahalaliki kwao.

 

 



http://bit.ly/2W52jIc

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

20-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Isti’aadhah Kwa Asiyekuwa Allaah

  إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيم   Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!   20 - Isti’aadhah  (Kuomba Kinga) Kwa Asiyekuwa Allaah   ...