Translate

Jumapili, 26 Mei 2019

Ni Ipi Hukumu Ya Kuswali Nyuma Ya Mzushi?


Swali: Ni ipi hukumu ya kuswali nyuma ya mtu wa Bid´ah?

Jibu: Kuna sampuli mbili za Bid´ah:

1- Bid´ah ambayo ni kufuru. Mfano wa Bid´ah hiyo ni kama mti kuamini kuwa walii ananufaisha na anadhuru pamoja na Allaah au pasi na Allaah. Kuswali nyuma ya mtu kama huyu si sahihi ikiwa Bid´ah zake zinamfikisha katika kufuru.

2- Bid´ah ambayo sio kufuru. Ni sahihi kuswali nyuma yake. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Swalini! Wakipatia basi ni kwa manufaa yenu na yao na wakikosea ni kwa madhara yenu na yao.”

Hata hivyo nashauri kwenda katika misikiti ya Ahl-us-Sunnah au kufungua misikiti ya Ahl-us-Sunnah ili wasikutane na wazushi. Watu wa Bid´ah hawatokuacha ueneze Sunnah. Hatuwalinganii watu katika mienendo ya baba zetu na baba zetu mpaka watu wayadharau haya. Tunawalingania watu wote katika Sunnah za Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam); ambaye ndiye kipenzi chetu na kipenzi chao, yeye ndiye mwombezi wetu na mwombezi wao.

Ikiwa unaweza kujitenga mbali na mtu wa Bid´ah bila ya kutokea mitihani fanya hivo. Vinginevyo nende katika misikiti ya Ahl-us-Sunnah. Hii ni kwa minajili tu ya nasaha, vinginevyo kuswali nyuma yake ni sahihi midhali Bid´ah yake haijamfikisha katika kufuru.

Kujipambanua ni jambo muhimu. Hata swalah ya ´iyd ikiwa Ahl-us-Sunnah wanaweza kuswali kivyao na kuitendea kazi Sunnah basi wafanye hivo. Ahl-us-Sunnah sio walinganizi wa fujo. Lau tutapigwa na kutimuliwa nje ya misikiti tunavumilia. Lau ndugu zetu wakapokonywa misikiti yao tunavumilia. Hatutaki fujo.

Ikiwa unaweza kujenga msikiti au kwenda katika msikiti wa Ahl-us-Sunnah fanya hivo. Vinginevyo swalah yako ni sahihi. Nakutahadharisha kuswali kwenye pembe ya msikiti peke yako ilihali waislamu wako wanaswali kwa hoja tu eti imamu ni mzushi. Nakutahadharisha kuswali peke yako nyumbani ilihali waislamu wako wanaswali kwa sababu tu eti imamu ni mzushi. Kuswali nyuma yake ni sahihi kama tulivyosema.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

20-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Isti’aadhah Kwa Asiyekuwa Allaah

  إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيم   Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!   20 - Isti’aadhah  (Kuomba Kinga) Kwa Asiyekuwa Allaah   ...