Translate

Jumapili, 26 Mei 2019

Baadhi ya Ndugu zetu wengi wanaojiita Muwahideen wanaonekana kuisahau na kuizembea AL WALA  sehemu ambayo ni muhimu sana ya #Al_Wala #Wal_Bara.

Tunashutumiana baina yetu katika masuala madogo madogo kama masuala ya fiqh au usahihi wa Hadithi, aidha kuwekeana fitna katika Maisha na Makazi. Basi tunashikilia kidedea na kudumisha uhasama baina yetu (Wenye kwa wenyewe).

Hata Maswahaba walikuwa na kutoelewana katika masuala fulani flani, lakini hiyo haikuwafanya kuchukuliana kama maadui wa Uislamu kama sisi leo hii tunavyofanya.

Wakati mwingine inakupelekea kumfanyia BARA Muiislam mwenzio kwa ajili ya dhambi anazotenda. Lakini bado unapaswa kumchukulia kama Ndugu yako Muislam na kumpa Dawah.  Hatupasi kuwatangaza na kuyadhihirisha mambo yao.  Bado yatupasa tuwapende kama Waislam.

Ikiwa Muislam huyo hawapotoshi wengine, kwa mfano, kwa kiburi na kwa uwazi anafanya dhambi au kwa kuhubiri vibaya tunapaswa kuwashauri kwa faragha na si kuanza kupigana nao ikiwa hawakubali ushauri.

Umoja na upendo kwa kila mmoja pia ni sehemu ya AL WALA WAL BARA.  Lakini kwa masikitiko makubwa, hatushuhudii umuhimu wowote ukitolewa kuhusu Umoja na upendo.

Tunadhani hatutazingatiwa kama Muwahideen, na wengine, ikiwa hatutojadiliana kiubishi na kutukanana kwa masuala madogo madogo.

Kuna tofauti kati ya kuchukia kwa ajili ya ALLAAH na chuki kwa ajili yangu mwenyewe.

Na pia Kuna tofauti kati ya kupenda kwa ajili ya ALLAAH na upendo kwa ajili yangu mwenyewe.

Kushauriana baina ya Muwahideen lazima kuwe ni kwa njia nzuri. Hakuna sababu ya kutengeneza na kueneza chuki baina YETU. Inatupasa sisi ndio tuwe mfano wa kuigwa na wengine ili kujenga taswira iliyo bora na kufuatwa na wengine.
 
Fikiria, una jirani yako Kafiri na jirani yako Muislam.

Inatokea una mgogoro wa mpaka ya ardhi na jirani yako Muislam na nyote wawili huingia kwenye hoja za mabishano na chuki baina yenu na kupelekea kugombana kila wakati.

Jirani yako kafir yeye mara zote huwa ni mzuri na mwenye huruma kwako na wala hamjawahi kugombana nae hata mara moja.

Kisha siku moja kunatokea mafuriko katika maeneo yenu.

Jirani yako Kafiri na jirani ya Kiislam wote mafuriko yamewaingila ndani. Wewe sasa unao Uwezo wa kumuokowa moja tu kati yao.

Jirani yako Muislam yeye yupo mbali kidogo kuliko jirani yako Kafiri.

Unatakiwa umsaidie jirani yako Muislam kwanza. Utaogelea au vyovyote uwezavyo ilimradi ufike kwake ingawa yeye yu mbali zaidi na wewe kuliko jirani yako Kafiri.

Kwa sababu hii sio dhidi ya chuki binafsi. Hii ni Kwa sababu ya upendo kwa ajili ya ALLAAH.

NDUGU YAKO MUISLAM ana haki zaidi juu yako.  Muislam anafaa zaidi kusaidiwa kwanza kuliko Kafiri.

Ingawa mna mgogoro na chuki binafsi na jirani yako Muislam, ila bado unapaswa kumtanguliza yeye kabla ya jirani yako Kafiri na kuokoa maisha yake.

Kwa nini tushindane na kugombana kwa sababu ya mambo madogo madogo???.  Labda wewe upo sahihi juu ya suala hilo lakini hiyo sio sababu ya kugombana na kutukanana.

JAMBO la msingi la kufahamu ni kwamba sote tumekulia katika malezi tofauti tofauti.  Labda yawezekana upo sahihi katika suala flani dogo/kubwa pia. Na siku za nyuma, hakika haikuwa hivyo kwako. Inaweza kumlazimu ndugu yako Muislam muda ili kuelewa jambo ambalo hata kwako pia lilikuwa ngeni hapo kabla.

Tuwe na uvumilivu baina yetu Muwahideen na tusieneze chuki kwenye vyombo vya habari vya kijamii baina yetu.  ALLAAH Anapenda umoja na upendo unaodumu kati ya Waislam.

Na ALLAAH Atuzidishie ufahamu SAHIHI, mapenzi na mshikamano baina yetu Muwahideen.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

20-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Isti’aadhah Kwa Asiyekuwa Allaah

  إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيم   Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!   20 - Isti’aadhah  (Kuomba Kinga) Kwa Asiyekuwa Allaah   ...