SWALI
Kuna mtu kamwingilia mke wake katika mchana wa Ramadhwaan ambaye alikuwa katika swawm. Hii ilikuwa kabla ya miaka kumi na tano [iliyopita], na kwa sasa ni mgonjwa na anatumia dawa lakini anafunga Ramadhwaan; Kafara ya Swawm miezi miwili ni ngumu kwake. Je, inajuzu kwake kulisha masikini badala ya swawm au ni lazima afunge? Je, na mkewe naye anapaswa kafara? Pamoja na kuwa hakuridhia hilo bali alikuwa akichukizwa na hilo.
JIBU
Mke wake hana kafara katika hali hii. Ama yeye ni juu yake swawm (ya miezi miwili mfululuzo) kutokana na kauli yake kaweza swawm Ramadhwaan. Bila shaka Anayeweza swawm Ramadhwaan anaweza kufunga miezi miwili isipokuwa kama ana maradhi na uzito unaomuathiri akifunga au kutokuweza kutokana na uzee. Kwa hali hio hakuna ubaya akalisha.
http://bit.ly/2YtVQ6e i live islam
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni