Swali
Inajuzu kwa mfungaji kumbusu mke wake na kufanya naye michezo ya kitandani?
Jibu
Ndio, inafaa midhali hachelei kuiharibu swawm yake kwa kutokwa na manii. Akitokwa na manii basi swawm yake inafisidika. Ikiwa amefanya hayo mchana wa Ramadhaan basi ni lazima kwake kujizuia mchana uliobaki na atalazimika kuilipa siku hiyo.
Ikiwa ni nje ya Ramadhaan basi ameiharibu swawm yake na wala halazimiki kujizuia mchana uliobaki.
Lakini ikiwa ni swawm ya wajibu basi ni lazima kuilipa siku hiyo na ikiwa ni swawm ya sunnah hakuna neno juu yake.
Rejea Kitab Majmuu´-ul-Fataawaa (19/358)
http://bit.ly/2EqeWTi i live islam
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni