Swali
Kuna kijana amejitoa manii mchana wa Ramadhaan. Ni lipi la wajibu kwake?
Jibu
Naam ama Punyeto mchana wa Ramadhaan inaharibu swawm ikiwa mtu atakusudia kufanya hivo na akatokwa na manii.
Ni lazima kwake kulipa ikiwa swawm yake ni ya faradhi.
Ni lazima vilevile kutubu kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala).
Kwasababu kujitoa manii haijuzu sawa katika hali ya funga na hali isiyokuwa ya funga.
Rejea Kitab Majmuu´-ul-Fataawaa (15/267)
http://bit.ly/2HKcW9a i live islam
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni