Translate

Jumamosi, 18 Mei 2019

Alipe Siku Ambayo Amepata Maumivu Ya Hedhi Kabla Ya Jua Kuzama?

SWALI


Je, Swawm ya mwanamke ni Sahihi, au ni waajib kwake kulipa siku hiyo, ikiwa anadhani (anahisi) atapata hedhi au yuko na maumivu ya hedhi lakini bila ya yeye kupata chochote kabla ya jua kuzama?


JIBU


Ikiwa mwanamke aliye msafi anahisi kwamba damu iko njiani au ana maumivu ya hedhi wakati yeye ni mwenye Swawm bila ya yeye kutokwa na kitu kabla ya jua kuzama, Swawm yake ni sahihi. 


Hana haja ya kulipa siku hiyo ikiwa kama ni Swawm ya waajib, na hatokosa ujira wake ikiwa ni Swawm ya Sunnah.


[Imaam Ibn 'Uthaymiyn - Su-alaat ‘an Ahkaamil-Haydhw uk. 11]


http://bit.ly/2YAMiGq i live islam

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

20-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Isti’aadhah Kwa Asiyekuwa Allaah

  إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيم   Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!   20 - Isti’aadhah  (Kuomba Kinga) Kwa Asiyekuwa Allaah   ...