SWALI
Mwenye kumuingilia mke wake kwa nyuma (kitendo cha liwati) katika mchana wa Ramadhwaan; je, Swawm yake inaharibika na inamlazimu kutoa kafara?
JIBU
Ndio, Swawm yake inaharibika bila ya khilaaf na inamlazimu kutoa kafara, na juu yake huzingatiwa ni mwenye kuasi mtendaji dhambi mkubwa ikiwa yuko katika swawm au hayuko katika swawm.
Alipoulizwa Ibn ´Umar (Radhwiya Allaahu ‘ahumaa) kuhusiana na kitendo hichi akasema "Ni kufru".
Mwenye kufanya hilo kwa kulihalalisha kakufuru. Na Kauli ya Allaah (´Azza wa Jalla):
نِسَاؤُكُمْ حَرْثٌ لَّكُمْ فَأْتُوا حَرْثَكُمْ أَنَّىٰ شِئْتُمْ ۖ وَقَدِّمُوا لِأَنفُسِكُمْ ۚ وَاتَّقُوا اللَّـهَ
223. Wake zenu ni konde kwenu. Basi ziendeeni konde zenu (panapotoka kizazi) vyovyote mpendavyo. Na kadimisheni (mema) kwa ajili ya nafsi zenu. Na mcheni Allaah [Al-Baqarah : 223]
Kuhusiana na "mcheni Allaah" Ibn Kathiyr (Rahimahu-Allaah) ametaja Hadiyth nyingi na Athar za kuharamisha hilo na wengineo pia.
Athar sahihi kutoka kwa Ibn ´Umar (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kutokana na uovu mkubwa wa hili, na hapakuthibiti kauli inayoenda kinyume na hii. Basi amche Allaah. Lina madhara pia kama ilivyo katika "Zaad Al-Ma´aad" lina madhara tendo hili chafu.
Muulizaji: Vipi ikiwa atafanya lakini hahalalishi tendo hili?
Ni mwenye kuasi, fasiki, mtendaji dhambi mkubwa. Ni waajib kwa mke wake kutoka kwake na walii wake wamsaidie kutoka. Wakiwa na uhakika wa hilo, asiridhie yeye kwa uovu huu wala walii wake asiridhie uovu huu.
Yeye (walii wa mwanamke) kamuoza kwa Sunnah ya Allaah na Rasuli Wake, kamuoza kama Alivyoliruhusu Allaah (´Azza wa Jalla). Allaah Kasunia hilo na Kaliwekea Shariy´ah kwa waja Wake, na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Rusuli waliosalia walikuwa na wake na watoto. Sunnah na neema kama hii, kuikufuru ni kama mfano wa kitendo hichi.
http://bit.ly/2YHJW95 i live islam
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni