Translate

Jumanne, 28 Mei 2019

Je Zakaatu-Fitwr apewe nani?

SWALI

Zakaatul-Fitwr apewe nani? Je, inaruhusiwa kuituma mfano kwa Mujaahidiyn waliko vitani? Au kuitoa katika vyama vinavyokusanya sadaka au kujengea msikiti?

JIBU

AlhamduliLLaah

Zakaatul-Fitwr inapaswa kupewa maskini Waislamu katika nchi au mji ambao inatolewa kwa sababu ya usimulizi wa Abuu Daawuwd kutoka kwa Ibn 'Abbaas (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) ambaye amesema: "Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ameamrisha Zakaatul-Fitwr ilipwe Ramadhwaan kuwalisha watu masikini…."

Inaruhusiwa kuituma kwa masikini wa nchi nyingine ambao watu wake wanahitaji zaidi. Hairuhusiwi kujengea msikiti au kuitoa katika miradi ya sadaka.


[Fataawaa Al-Lajnah Ad-Daaimah]




Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

20-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Isti’aadhah Kwa Asiyekuwa Allaah

  إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيم   Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!   20 - Isti’aadhah  (Kuomba Kinga) Kwa Asiyekuwa Allaah   ...