Swali
Inafaa Kuswali Sunnah Kabla Ya Swalah Ya Magharibi?
Jibu
Hakuna makatazo ya kuswali Sunnah kabla ya Magharibi au baada ya Maghrib bali inapendekezeka kufanya hivyo.
Ila huenda imefahamika kwa aliyemkataza kuswali, kuwa ni kabla ya kuadhiniwa Magharibi, kwa maana baada ya Swalaah ya Alasiri.
Ikiwa hivyo basi itakuwa haifai kwani wakati huo ni miongoni mwa nyakati ambazo makruuh (zinazochukiza kuswali), hivyo hakuna Swalaah ya Sunnah.
Lakini baada ya kuadhiniwa Magharibi inafaa kuswali Sunnah ambayo inajulikana kuwa Sunnah Ghayr Muakkadah (Sunnah isiyosisitizwa).
Na Allaah anajua zaidi
http://bit.ly/2HXYMkK i live islam
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni