Swali
Maiti akifa na baada ya kumuogesha na kumvisha sanda wanakuja ndugu na marafiki zake kumsalimia na kumbusu. Je, kitendo hicho kina msingi katika Shari´ah?
Jibu
Hakuna ubaya kufanya hivyo.
Ni aina fulani ya kumuaga na kumuombea du´aa. Hakuna neno.
Wakati Mtume Muhammad(Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipokufa, Abu Bakr (Radhiya Allaahu ´anh) aliingia ndani mwake, akamfunua uso wake na akambusu.
Rejea Kitab Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (96)
http://bit.ly/2WjYvlD i live islam
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni