Translate

Jumamosi, 18 Mei 2019

Maana Ya Zakaah

                                                 Maana Ya Zakaah


Zakaah ni ile haki Aliyoifaradhisha Allaah kwa Muislam katika mali yake anayotakiwa kuwapa wanaostahiki. 

Neno Zakaah, katika lugha (katika kamusi ya lugha ya Kiarabu) maana yake ni 'Kujitakasa', kwa sababu anayetoa Zakaah anataraji kuitakasa mali yake, nafsi yake na kupata baraka kutoka kwa Mola wake.
Allaah Anasema:
خُذْ مِنْ أَمْوَالِهِمْ صَدَقَةً تُطَهِّرُهُمْ وَتُزَكِّيهِم بِهَا
"Chukua Swadaqah katika mali zao, uwasafishe na kuwatakasa kwa ajili ya hizo (Swadaqah zao)".
[At-Tawbah: 103]

Zakaah ni nguzo ya tatu ya Uislam iliyofaradhishwa katika Qur-aan tukufu na katika mafundisho ya Mtume mtukufu (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), na kwa sababu ya umuhimu wake, Allaah ameitaja mara themanini na mbili katika Qur-aan kwa kuifuatanisha pamoja na Swalaah.

Imepokelewa kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kuwa amesema:
"Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alipomteua Muadh bin Jabal (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kuwa gavana wa nchi ya Yemen na kadhi wao alimwambia:
"Unakwenda katika nchi ya watu wa Ahlul Kitab, kwa hivyo (kwanza) walinganie katika shahada ya Laa ilaaha illa Allaah na kwamba mimi ni Mtume wa Allaah, wakitii juu ya hilo, wafundishe kuwa Allaah amewafaradhishia Swalaah tano mchana na usiku, wakitii juu ya hilo, wafundishe kuwa Allaah amewafaradhishia Swadaqah (Zakaah) za mali zao, zichukuliwe kutoka kwa matajiri wao na kurejeshewa masikini wao, na kama wakitii juu ya hilo, usije ukachukuwa mali zao zenye thamani, na uiogope dua ya aliyedhulumiwa, kwani hapana kizuizi baina yake (dua hiyo) na baina ya Allaah".
[Imesimuliwa na Ma-Imaamu wote wa Hadiyth]

Imesimuliwa pia na At-Twabaraaniy kutoka kwa ‘Aliy (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kuwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"Allaah amewafaradhishia matajiri wa Kiislam katika mali zao kiasi cha kuwatosha masikini wao. Na (masikini) wasingepata tabu ya njaa na mavazi isipokuwa kutokana na ubakhili wa matajiri wao. Jueni kuwa Allaah atawahesabia hesabu nzito sana na atawapa adhabu iumizayo".




http://bit.ly/2w5miXx i live islam

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

20-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Isti’aadhah Kwa Asiyekuwa Allaah

  إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيم   Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!   20 - Isti’aadhah  (Kuomba Kinga) Kwa Asiyekuwa Allaah   ...