Translate

Jumamosi, 18 Mei 2019

Je, I’tikaaf Inasihi Katika Misikiti Mingineyo Isiyokuwa Ile Mitatu?

Je, I’tikaaf Inasihi Katika Misikiti Mingineyo Isiyokuwa Ile Mitatu? (Masjid Al-Haraam (Makkah), Masjid An-Nabawiy (Madiynah), Masjid Al-Aqswaa (Palestina).

Imaam Ibn Baaz (Rahimahu Allaah) amesema:

a. I’tikaaf inasihi katika Misikiti mingineyo isiyokuwa katika mitatu isipokuwa ikiwa mtu ametoa nadhiri kutekeleza I’tikaaf katika Misikiti mitatu basi hapo inamlazimu atekeleze I’tikaaf humo ili atimize nadhiri yake. 

b. Isipokuwa ikiwa haiswaliwi Swalaah ya jamaa’ah humo basi I’tikaaf haisihi kutekelezwa humo. 


[Majmuw’ Al-Fataawaa (15/444)]


Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) amesema:

Inajuzu I’tikaaf katika Misikiti mingineyo isiyokuwa ile mitatu na ikiwa Hadiyth hii ni swahiyh “Isifanywe I’tikaaf isipokuwa Misikiti mitatu”, basi iliyokusudiwa ni kwamba I’tikaaf humo ni yenye ukamilifu na bora zaidi. 


[Majmuw’ Al-Fataawa 20/160)]


http://bit.ly/2w5uKGa i live islam

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

20-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Isti’aadhah Kwa Asiyekuwa Allaah

  إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيم   Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!   20 - Isti’aadhah  (Kuomba Kinga) Kwa Asiyekuwa Allaah   ...