SWALI
Nini hukmu ya mwanamke kutumia dawa za uzazi ili kuzuia kufika kwa damu ya hedhi apate kumaliza swiyaam mwezi mzima? Tufaidisheni, Allaah Akufaidisheni nanyi.
JIBU
Hakuna ubaya kufanya hivyo kwamba atumie vidonge vya kuzuia hedhi ili aweze kuswali na watu na afunge nao kwa sharti kwamba kufanya hivyo kuna usalama kwake na havitomdhuru.
Na pia baada ya kupata ushauri wa daktari ili asije kujidhuru nafsi yake, na pia apate ruhusa kutoka kwa mumewe ili asimuasi mumewe.
Itakapokuwa baada ya kushauriana na kutahadhari upande wa salama kutokana na madhara, basi hakuna ubaya.
Na hali hiyo hiyo iwe katika masiku ya Hajj.
Baaraka Allaahu Fiykum
http://bit.ly/2Qcztix i live islam
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni